Mahakama ya Kadhi yalitafuna Bunge

Mahakama ya Kadhi yalitafuna Bunge

Miaka ya nyuma hali ya chuki za kutisha kiasi hiki haikuwepo kabisa. Watanzania walipendana na kuheshimiana bila ya kujali huyu ni dini gani na yule ni gani. Sasa hivi pamoja na hali kuzidi kuwa ya kutisha kutokana na ombwe kubwa la uongozi nchini hakuna anayekemea chuki hizi ambazo zimeshaanza kuleta mitafaruku mikubwa sehemu mbali mbali nchini.

Bubu,

Miaka nyuma malalamiko yalikuwapo ila kilichokuwa kikitumika ni propaganda ambazo kwa bahati mbaya kutokuwa na elimu na kutojitambua vilichangia zikawa zikiendelea kukandamiza jamii moja dhidi ya nyengine. Zama za sasa waislamu waliosoma ni wengi sana na wengine wanauza karanga lakini wamesoma hadi degree. Dhulma imeongezeka mara dufu imefika stage sasa inafanyika wazi kabisa. Mtu anasimama anadai waislamu wanataka mahakama ya kadhi ilipiwe na kodi za wakristo ambao wengi ni wanauza pombe na nguruwe anayasema hayo mbele za watu na bungeni wakati anasahau kuwa waislamu ni walipa kodi vile vile tena walipa kodi wakubwa na pia waislamu wanaolipa kodi wana haki ya kikatiba kupatiwa huduma za kisheria ambazo for 50 years zimekuwa hazipo badala yake Bakwata imekuwa mshauri tu na hivyo kupelekea mambo mengi ya waislamu yanakwama.

Tukitaka suluhu ya haya mambo tubalance wapewe waislamu mahakama ya kadhi, wakristo wakitaka wawe na mahakama zao kidini. Vyenginevyo hapa shughuli ni pevu na tunalekea kugawana mbao
 
Wewe nikuulize Bugando na Mission Mbweni si wanapewa ruzuku? Sasa kwanini basi wanalipisha watu. Na kwanini tulinganishe na Mbweni kwanini tusichukue Hospitali ya KCMC Moshi na TMJ halafu tuzilinganishe?

Usiwe mwehu.. Kwani muhimbili hutozwi hela?? si inaendeshwa kwa kodi za serikali?????

Then kcmc na bugando serikali ilijipendekeza yenyewe kuingia ubia kwa sera yake ya PPP lakin kanisa halijawahi onekana limeahindwa kuendesha hospitali zake na huduma zingine za jamii

nyie mnashindwa nini??? mnaendekeza udini tu badala ya kufanya mambo ya maana kwa maendeleo ya kijamii

yani badala ya kujenga vituo vya huduma za msingi mnajenga vyuo mafunzo ya karate.. Mnajiaandaa kupigana na nani
 
Kwaiyo nyinyi wawakilishi wenu hawana ajenda mle ndani siyo??

Mmewatuma tu wakakae kusubiri waislam wanataka kusema nin kisha wao wasimame juu na kusema hawataki si ndiyo??

Mambo ya kwetu sisi na iman yetu nyinyi yanawahusu kitu gani??

Ni kweli nchi haina dini.

Ila wananchi wana dini tatizo liko wapi.

Then unachoshindwa kuelewa ni kwamba hilo la kusema nchi haina dini limeshapitwa na wakati hilo lilikuwa kwenye katiba ile iliyochakaa na inayotaka kufanyiwa marekebisho.

Na ukileta maandiko ya katiba ambayo hiv sasa inataka kuboreshwa au kuandika upya kama gia ya kupinga matakwa yetu ya leo ni uwendawazimu.

Litambue hilo.

Sisi mahakama ya kadhi tutaipata mtake msitake

Unless otherwise hakuna katiba mpya itayopatikana.

Its now freedom for everybody in this country or freedom to nobody.

Siku na mashoga nao watakavyotaka ndoa ya jinsia moja kwenye katiba ndo mtajua kuwa si kila jambo linakaa kwwnye katiba ya nchi yetu

kadhi jambo la kidin wwkwn kwenye vitabu vya dini
 
Waislamu hawawezi kuunda mahakama ya kadhi kwa utaratibu wao kwa sababu sio wamoja, ndio maana wanadandia kwenye mgongo wa serikali ( SUNI VS SHIA). Ni wakwepaji wa kulipa sadaka na zaka katika nyumba zao za ibada( USHAHIDI: ni wakati wa sakata la mwembechai; wakati wenzao wanasota lupango walishindwa hata kusaidia ndugu zao waliobakia majumbani). Si watu wa kujitolea ni watu wa kukwepa majukumu yao. wanaishi kijanja kijanja tu ndo maana hapa Dar utawaona kama wako kipopopopo tu!! Mara CCM nzuri, mara CUF nzuri na mara CDM nzuri. Wako kidini dini saana kutegemea mdini mwenzao yuko upande upi!!

(1) Kama wameshindwa kujua kitendo tu cha kudai mahakama ya kadhi iendeshwe na serikali ambayo sio ya kiisilamu ni haramu ujue wanamatatizo makubwa!

(2) Mahakama hiyo kudai iendeshwe na pesa ambazo ni kodi za vitu halali na haramu kwa imani ya dini yao; ujue uislamu una matatizo.

Ushauri:

Waislamu wengi ni matajiri sana na kwa suala la mahakama ya kadhi ni vema mkasimama wenyewe ili kuitimiza kweli ya dini yenu kwa vitu halali na pesa halali! mtakuja daiwa siku moja na Allah wenu kwa mambo kama haya!!
 
Mkuu hivi ndivyo Allah anakufundisha?

Allah ametufundisha tuwe na Mahkama ya kadhi ili waislamu haki zao ziwe zinaamuliwa huko kisheria sasa unaposema mahakama ya kadhi ni najis ni vyema ukafahamishwa kilicho Najis. bila shaka umeelewa
 
Wewe nikuulize Bugando na Mission Mbweni si wanapewa ruzuku? Sasa kwanini basi wanalipisha watu. Na kwanini tulinganishe na Mbweni kwanini tusichukue Hospitali ya KCMC Moshi na TMJ halafu tuzilinganishe?


Kwanza ni kiri kuwa uzoefu wangu nilisha shuhudia huduma ya tmj na mbweni. Kwa huduna hiyo hiyo tmj gharama yake ilikuwa x 8 zaidi ya mbweni, sawa.


pili wewe ndio unanifungua macho leo kuwa bugando na kcmc zipo jiji dsm hilo nilikuwa silijui lazima nikiri.
 
Wewe acha ujinga watu wa mwanzo kupeleka MOU serikalini walikuwa akina Sheikh Ponda na walikataliwa na walipokuja makanisa MOU ikapita kwa vigezo kuwa imefikia vigezo husika. Na pili ficha ujinga wako wamiliki ya Bugando na KCMC ni akina nani? Je gawio la pato au dividend kutoka katika hospitali au shule kuna msikiti gani umefaidika? Wafanyakazi waislamu wangapi Bugando na KCMC. Tuondolee upuuzi wako hapa hakuna mjinga kadanganye wengine.
Ninaona unapiga kelele hutoi hoja! Haujajibu hoja zaidi ya kutukana na kujificha nyuma ya Sheik Ponda. Je huyo Ponda ni kitu gani hasa amewai kufanya kina faida kwa umma au hata waislamu wenyewe zaidi ya siasa zake za mapambano Kati yake na waislamu wenziwe na Kati yake na Serikali?
 
Ninaona unapiga kelele hutoi hoja! Haujajibu hoja zaidi ya kutukana na kujificha nyuma ya Sheik Ponda. Je huyo Ponda ni kitu gani hasa amewai kufanya kina faida kwa umma au hata waislamu wenyewe zaidi ya siasa zake za mapambano Kati yake na waislamu wenziwe na Kati yake na Serikali?

Hoja gani unayoitaka wewe:-

Hoja ya kwanza:-
Kwanini waislamu wanaitaka mahakama ya kadhi nishakuelezeni kuwa waislamu wanataka mahakama ya kadhi kama njia moja ya kutatua migogoro ya mirathi na ndoa inayoendelea nchini. Ili kuweza kuwasaidia watanzania waislamu waweze kuwa na jamii bora na kuweza kukwamuka kimaisha.

Hoja ya pili:-
Kwanini iwe mahakama na sio taasisi ya kidini ni kwasababu mahakama ya kadhi ni mahakama kamili legal jurisdiction na hivyo inahitaji iwe na jurisdiction ili iweze kuwa na meno ya kisheria. Na pia iwe na mfumo kuanzia mahakama ya chini mpaka mahakama ya juu.

Hoja ya 3:-
Na atalipia ? Jibu ni simple serikali kwavile moja ya kazi za serikali ni kugharimia huduma za kisheria zinazotolewa kwa walipa kodi? Na waislamu nchini kwakuwa ni watanzania na walipa kodi basi wanahitaji kugharamiwa mahakama zao zenye kusimamia ndoa na mirathi.

Hoja ya nne:
Serikali haina dini: Jibu ni kuwa ni kweli serikali yetu haina dini ila mfumo wetu wa kisheria nchini ni wa kufuata mfumo wa kisheria wa waingereza na nchi nyenginezo za ulaya. Mfumo wao kisheria (Philisophy of law and History of Law) inatokana na mfumo wa imani ya kikristo ndio maana sheria zetu nchini nyingi zinaenda tofauti na mfumo wa kisheria wa kiislamu or islamic law. Sasa kama sheria tulio nazo zinatambua ukristo but uislamu hautambuliki inakuwaje unadai serikali haina dini? Marriage Act ya 1970s inasema kuwa mke halali anayetambulika kisheria ni mmoja wakati waislamu wanaruhusiwa kuoa zaidi ya wawili hadi 4, wapagani hata wake 100 sasa sheria hapa ndio tuseme haina dini kwasababu mke mmoja ni philosophy ya ukristo kuweka utakatifu wa ndoa na mke mmoja ila hilo halipo katika uislamu wala ukristo utasemaje serikali haina dini?

Hoja ya tano:
Inakuwaje kodi za wakristo wakati wao hawafaidiki? Jibu la hili ni kuwa sio lazima wakristo wafaidike kwasababu sio waathirika wa mfumo uliopo? Watafaidika wakristo kuwa na majirani wa waislamu ambao watakuwa na uwezo sawa na wao kwani sasa hivi waislamu wengi ni mafukara kwasababu ya mali walizochuma nyingi zinapotea kwa kusimamiwa na taasisi kama Bakwata badala ya kusimimamiwa na Waqfu na mali ya amana ambayo ni taasisi itakayokuwa chini mahakama ya kadhi yenye nguvu ya kisheria kusimamia mirathi. Kwa maana hiyo watuvumilie kama sisi tunavyowavumilia na Memorandum of Understanding ambayo ni ufisadi wa mchana kweupe. Kila mwaka serikali inatoa Billioni 91 kwenda katika mashule na mahospitali ya kanisa. Pesa hizi hutoka katika kodi ya watanzania ambapo mwislamu hafaidiki kwalolote zaidi kubaki anashangaa na kupumbazwa ati anatibiwa na kusomeshwa. Hoja hii ni mfu kwasababu mahospitali binafsi na mashule binafsi nchini mbona yanaendeshwa kwa faida licha ya kuwa hawapati chochote kutoka serikali kama ruzuku? Kama wao wanaweza watashindwa vipi makanisa kuendesha taasisi zao kama sio wizi wa mchana huu?

Hoja ya sita:
Huu ni udini? Jibu ni simple kudai haki ya kisheria ni udini tangu lini? Je waislamu wakisema serikali ina udini kuwapendelea wakristo na MOU watakosea nao? Udini gani kusema kuwa tunataka huduma ya kisheria kutoka serikalini kwa kupitia katiba?

Haya leta hoja zako?
 
Kwanza ni kiri kuwa uzoefu wangu nilisha shuhudia huduma ya tmj na mbweni. Kwa huduna hiyo hiyo tmj gharama yake ilikuwa x 8 zaidi ya mbweni, sawa.


pili wewe ndio unanifungua macho leo kuwa bugando na kcmc zipo jiji dsm hilo nilikuwa silijui lazima nikiri.

Kwanza nikusahihishe ,

Bugando hospitali ipo Mwanza, KCMC ipo Moshi ila hizi ni hospitali kubwa sawia na TMJ, Aga Khan hivyo gharama zao zinatakiwa zinalingana na ikiwa basi Bugando wanapewa ruzuku na serikali au KCMC wanatakiwa wawahudumie watanzania wote bure au kwa bei ya chini sana je wanayafanya hayo?

Ukija kwenye mashule ndio aibu kabisa ada ni ya juu mno lakini unasikia shule inapata ruzuku ya serikali kama sio ufisadi huu ni nini?
 
Hii ndiyo taabu ya kuchukua neno juu-juu bila kulielewa na kuwa msemaji walo ukiulizwa unaanza kubwabwaja kama unavyofanya sasa nakushauri UKIAMBIWA NENO TUMIA NA AKILI YAKO kuliangalia na kuliamua ona sasa unaonekana MBUMBUMBU wa kutupwa kwa sababu tu ya kukaririshwa Jitambueni.
Sasa kabla sijawauliza masheikh ngoja nikuulize wewe ni kitu gani kinawafanya mpewe hela kutoka kwa sisi waislamu wakati tukienda hospitali tunatibiwa kwa kulipa hela zetu wenyewe mfukoni? Na sio hivyo tu mbona kuna hospitali za watu binafsi kama TMJ, Agakhan, Burhani hazipewi huo mlungula mnaotafuna.

Na kama mnachangiwa na serikali kwanini msitibu au kusomesha bure kama sio ufisadi huo ni nini?
 
Hii ndiyo taabu ya kuchukua neno juu-juu bila kulielewa na kuwa msemaji walo ukiulizwa unaanza kubwabwaja kama unavyofanya sasa nakushauri UKIAMBIWA NENO TUMIA NA AKILI YAKO kuliangalia na kuliamua ona sasa unaonekana MBUMBUMBU wa kutupwa kwa sababu tu ya kukaririshwa Jitambueni.

Mbumbumbu ni wewe usiye na hoja Jibuni hoja zangu au kaa kimya ficha upumbavu wako kama huna cha kujadili
 
Kwanza nikusahihishe ,

Bugando hospitali ipo Mwanza, KCMC ipo Moshi ila hizi ni hospitali kubwa sawia na TMJ, Aga Khan hivyo gharama zao zinatakiwa zinalingana na ikiwa basi Bugando wanapewa ruzuku na serikali au KCMC wanatakiwa wawahudumie watanzania wote bure au kwa bei ya chini sana je wanayafanya hayo?

Ukija kwenye mashule ndio aibu kabisa ada ni ya juu mno lakini unasikia shule inapata ruzuku ya serikali kama sio ufisadi huu ni nini?

Jenga yko na ww upewe ruzuku
 
Kwanza nikusahihishe ,

Bugando hospitali ipo Mwanza, KCMC ipo Moshi ila hizi ni hospitali kubwa sawia na TMJ, Aga Khan hivyo gharama zao zinatakiwa zinalingana na ikiwa basi Bugando wanapewa ruzuku na serikali au KCMC wanatakiwa wawahudumie watanzania wote bure au kwa bei ya chini sana je wanayafanya hayo?

Ukija kwenye mashule ndio aibu kabisa ada ni ya juu mno lakini unasikia shule inapata ruzuku ya serikali kama sio ufisadi huu ni nini?


Ustadhi inavyo onyesha hili la mou lina kukera sana. Sasa inawezekana unafahamu labda kuna taasisi za kislamu ambazo zina vigezo vya kupata ruzuku zimenyimwa na serikali. Ingekuwa vema kama ungeweka wazi.

Labda tungeishauri serikali kama itawezekana waweke idadi ya wake mtu anao waoa iwe kigezo cha kupewa ruzuku ya mou.
 
sawa mkuu #THE BIG SHOW pamoja na kwamba serikali haina dini mnataka serikali iingize mahakama ya waislamu katika katiba. labda nikuulize swali lingine... unadhani hiyo mahakama itakuwa na msaada wowote au tija kwa taifa na serikali yake? nadhani serikali sikivu ya jakaya imeshajiuliza maswali mengi na imejiridhisha kuwa mahakama ya kadhi itaingilia sheria za mahakama rasmi za serikali, na pia itaiongezea mzigo serikali katika kuwatumikia wananchi. kwanza ni haramu kodi za mabucha ya kitimoto na bia kutumika katika kuendesha mamnbo ya waislamu sasa sijui mnangangania nini... au ni kwakuwa watakaoajiriwa kwenye hizo mahakama ni masheikh (waislamu) peke yenu??

Bakwata gani unayoizungumzia.

Hiyo aliyoianzisha nyerere au ipi hiyo.

Ni nyinyi na chuki zenu tu.

Kwamba mahakama ya kadhi hii isiendeshwe kwa gharama ya serikali hii kwa kodi ya watanzania hiyo ni chuki yenu nyinyi wakristo wa tanzania.

Kwani mfano wa nchi nyingine kama kenya na uganda kwenye wakristo na waislam na zinakoendeshwa mahakama hizo kuna shida gani??

Na waislam hawalipi kodi ndan ya nchi hii??

Kwa kodi zao hizo hizo wanazokatwa je haziwezi kuendesha mahakama ya kadhi??

Mahakama ya kadhi inagharimu sh ngapi kuendesha??

Hata sisi wenyewe waislam tutakuwa tayari kukatwa kodi zitazosaidia kuendeshs mahakama hiyo hatushindwi.

Hiyo hoja yenu ni mufilisi.

mkuu naomba unieleweshe sababu za waislamu kutaka mahakama ya kadhi iwe kwenye katiba. Mi huwa naona watu wanabishana sana lakini sielewi tatizo ni lipi hasa. Je ninyi waislamu mnataka mahakama ya kadhi iwe kwenye katiba ili hao masheikh watakaosimamia mahakama hizo walipwe na serikali? Na kama watakuwa wanalipwa na serikali sasa hilo si tatizo? Maana hiyo mishahara yao na bajeti za kuendesha mahaka za kadhi zitatoka katika kodi ambazo ni jasho la wakristo, waislamu na wasio na dini. Kama kweli mnataka mahakama ya kadhi iwepo na itategemea mapato yenu wenyewe basi hiyo mahakama ya kadhi itambuliwe kwenye sheria za bakwata na mruhusiwe kuzitengeneza nyingi kadri muwezavyo. Tena mkitaka mwaweza kusema kila msikiti wa ijumaa uwe na mahakama hapo hapo. Si imani yenu? Nani atawazuia kama mnafanyia katika maeneo yenu ya misikiti au majengo mliyonunua kwa fedha zenu wenyewe au za udhamini kutoka arabuni?

Kwaiyo nyinyi wawakilishi wenu hawana ajenda mle ndani siyo??

Mmewatuma tu wakakae kusubiri waislam wanataka kusema nin kisha wao wasimame juu na kusema hawataki si ndiyo??

Mambo ya kwetu sisi na iman yetu nyinyi yanawahusu kitu gani??

Ni kweli nchi haina dini.

Ila wananchi wana dini tatizo liko wapi.

Then unachoshindwa kuelewa ni kwamba hilo la kusema nchi haina dini limeshapitwa na wakati hilo lilikuwa kwenye katiba ile iliyochakaa na inayotaka kufanyiwa marekebisho.

Na ukileta maandiko ya katiba ambayo hiv sasa inataka kuboreshwa au kuandika upya kama gia ya kupinga matakwa yetu ya leo ni uwendawazimu.

Litambue hilo.

Sisi mahakama ya kadhi tutaipata mtake msitake

Unless otherwise hakuna katiba mpya itayopatikana.

Its now freedom for everybody in this country or freedom to nobody.
 
sasa nadhani kila mwana JF ameamini nisemayo mimi gogo la shamba kwamba waislamu wengi ni wanafiki,wepesi wa kudanganywana kama kungekuwa na umoja ndani ya uislamu ungeanzia tanzania na hapo dunia nzima ingewaogopa waislamu lakini kwa yaliyotokea bungeni jana usitegemei waislamu kupata hadhi tena mbele ya ukiristo maana dunia nzima ilikuwa inawaangalia waislamu wa tanzania watafanya nini kwenye hili suala la mahakama ya kadhi.
 
wakati mwingine ushabiki wa kisiasa unaweza kutupeleka kusiko katiba iliyosifiwa hata kabla haijaanza kutumika tayari inalalamikiwa
 
izi post zilishawekwa sana. angalia walivyoweka wenzio.

KHIDMAT DWAAT LISIAMIYAT CENTRE REGISTERED TRUSTEES
P. O. BOX 16106, MOB. 0713-290272, 0784-403020.


1. Uanzishaji wa Mahakama ya Kadhi utaleta madahara makubwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa vile Wakristo hawagawanyiki katika suala la kuipinga, lakini sisi Waislamu tunagawanyika katika suala hilo. Kwa taarifa yako napenda nikuhakikishie kuwa Waislamu wa Madhehebu ya AnsarSunna HAWAIKUBALI Mahakama hiyo kwa vile wanaelewa kuwa itakuwa chini ya BAKWATA.

2. Pia wanaelewa kuwa miongoni mwa mamlaka ya Kadhi ni kutangaza mwezi wa Ramadhani kufunga na kufungua na wao wanaye Amir wao ambaye hutangaza mwezi kwa kufuata mwezi unaoandama Saudia (Saud Arabia). Kwa maana hiyo katika nchi yenye Kadhi kutokea mtu mwingine nje ya Kadhi kutangaza mwezi ni kosa la jinai.

3. Kitu ambacho kitaleta madhara makubwa kuliko mafanikio ingawa AnsarSunna ni kundi dogo lakini wanaburuza kundi kubwa sana la Waislamu, kuliko Taasisi yoyote ya Kiislamu hapa Tanzania kwa vile ushawishi wao ni mkubwa sana katika jamii ya Kiislamu.

4. ANSAR SUNNA ndio wanaoendesha Shuura ya Maimam, GAZETI LA AN-NUUR, AL-HUDA, NASAHA na RADIO IMANI. Pia wana ushawishi mkubwa TIMES FM. Je, BAKWATA wana uwezo wa kupambana na vyombo hivyo?

5. Je, Serikali inaweza kukabidhi Mahakama ya Kadhi kwa wanaharakati wa Kiislamu? Nina hakika haiwezi kufanya jambo hilo na kama haitofanya hivyo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaweza kupata hasara zifuatazo:
(a) Wakristo wote wanaweza kujitoa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga katika chama cha CHADEMA ambacho hakina Mahakama ya Kadhi katika Ilani yake.
(b) Waislamu wote walioko chini ya Shuura ya Maimamu ambayo ni Mpinzani Mkuu wa BAKWATA wataendelea kuipinga Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa kuikumbatia BAKWATA na huku wakiendelea kuiunga mkono CUF, hivyo CCM itajikuta imebakia na Waislamu wanaoiunga mkono BAKWATA tu. Suala la wanaharakati kuipinga Mahakama ya Kadhi ni jambo rahisi sana kwa vile Mahakama ya Kadhi sio madai yao ya msingi.

6. Waislamu (wanaharakati) dai lao la msingi ni MGAWANYO SAWA WA MADARAKA. Hivyo Serikali inapounda Wizara, wao hutizama Baraza la Mawaziri, WAISLAMU NI WANGAPI NA WAKRISTO NI WANGAPI NDIO MAANA WANAIUNGA MKONO CUF, KWA VILE CUF IMEELEWA TATIZO LAO NA WAO WAKAJA NA KAULIMBIU YA HAKI SAWA KWA WOTE, yaani kwa Wakristo na Waislamu, wala Ilani ya Uchaguzi ya CUF haisemi lolote kuhusu Mahakama ya Kadhi WALA HAITOSEMA!!

7. Pia Waislamu wanaharakati wanaelewa kuwa Mahakama ya Kadhi haina manufaa yoyote kwa Waislamu, kwa vile Zanzibar ipo na WAISLAMU WA ZANZIBAR HAWANA MAENDELEO YOYOTE KUWAPITA WALE WA BARA, NA UISLAMU SI NDOA NA MIRATHI TU WALA MUNGU HASEMI "SOMETHING IS BETTER THAN NOTHING." Huu ni msemo wa Wazungu.

8. Mwenyezi Mungu anasema: INGIENI KATIKA UISLAMU WOTE NA MSIFE BALI MMEKUWA WAISLAMU KAMILI (Surat Baqarah ya 2 aya ya 208). Kwa hiyo mimi nikiwa kama Mwislamu nashauri kuwa Mahakama hiyo ISIWEPO kwani haitakuwa na manufaa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) na italeta mgawanyiko miongoni mwa wanachama wako, chukulia mfano Zanzibar, Mufti na Kadhi wanavyopingwa na wanauamsho ambao wanaongozwa na Sheikh Farid hali wanauamsho ndio Shura ya Maimam na Shuura ya Maimam ndiyo Uamsho.

KWANINI MASHEIKH WA BAKWATA WANAITAKA?
9. Wanaelewa wanachokifanya, wao wanajua fika kuwa Serikali itakapoanzisha Mahakama ya Kadhi watakuwa wamepata AJIRA, kwa hiyo wao wanapigania maslahi yao tu, hawawezi kuangalia madhara yatakayokikumba Chama Cha Mapinduzi (CCM) na huku wakijua kuwa ushawishi wao ni mdogo katika Jamii ya Kiislamu na hawana hata Miundumbinu ya kuwashawishi Waislamu wote waweze kumkubali Mufti, na hali ya Mufti ameshaweka wazi milango kwa Taasisi zote za Kiislamu na Waislamu waje washirikiane naye.

10. Masheikhe hawa wanaelewa kuwa hakuna Hakimu anayehukumu makosa mawili tu, yaani NDOA na MIRATHI, ukiletewa mzinifu huruhusiwi kumhukumu, ukiletewa mwizi huruhusiwi, nk. lakini wanang'ang'ania hivyo hivyo kwa ajili ya mishahara tu na hiyo ni hatari.

11. Hujaribu kutoa hata mifano ya Serikali ya Uingereza kwamba mwaka 1920 iliweka Mahakama hizo, ukweli ni kwamba Serikali ya Uingereza haikuweka Mahakama za Kadhi tu bali za Maakida na Maliwali, lakini pia sababu ya kuziweka Mahakama hizo siyo kwa ajili ya kuutunza Uislamu au uliwali bali ilikuwa ni mbinu ya kuwatuliza Viongozi hao ili waweze kuwatawala bila vurugu kwani mkoloni aligundua kuwa ni watu wenye ushawishi katika jamii kwa hiyo ile ilikuwa ni mbinu ya kiutawala ili Masheikhe, Maliwali na Maakida wajione kuwa na wao ni sehemu ya Serikali ya Muingereza, kumbe ni watawaliwa, hivyo bado hoja hiyo haina msingi wowote wala haina maana kwamba Serikali ya Mkoloni ilikuwa nzuri kwa Waislamu kuliko hii ya CCM, na huku tukiambiwa kuwa Waislamu ndiyo walioanzisha harakati za kudai Uhuru, kama walikuwa wazuri kwa nini tuliwaondoa.

12. CCM inayo mambo mengi ya kujivunia kwa Waislamu kama vile kuwapatia Chuo Kikuu, na hilo ni jambo muhimu na la msingi kwa maendeleo ya Uislamu na Waislamu, kwa hiyo JAMBO HILO LA MAHAKAMA YA KADHI mnapaswa kuliangalia kwa umakini ijapokuwa limo ndani ya Ilani yenu. Lakini si kila jambo lililomo ndani ya Ilani litekelezwe, mengine yanaweza kushindikana kwa matatizo mbalimbali na hili ni tatizo kubwa KWANI LINAWEZA KUZAA MGOGORO WA KIDINI!!

WAKRISTO WANA HAKI YA KUPINGA MAHAKAMA YA KADHI
13. Sehemu kama Zanzibar ni rahisi kuweka Mahakama ya Kadhi kwa vile Waislamu kule ni asilimia 99.99 hali kama hiyo Wakristo kule ni kama hawapo wamemezwa kwa uchache wao. Lakini BARA NI PAGUMU kwa vile HUENDA WAKRISTO NI WENGI KULIKO WAISLAMU. KWA VILE WAISLAMU KWA UHAKIKA HUPATIKANA MIKOA ISIYOZIDI SITA AMBAYO NI DAR ES SALAAM, LINDI, TANGA, MTWARA, KIGOMA NA TABORA, pia katika mikoa hiyo siyo Wilaya zote, kwa mfano Mkoa wa Kigoma ni Ujiji na Kigoma Mjini tu.

14. Pamoja na hayo Masheikhe wa BAKWATA wanaoshikilia suala la kuwepo kwa Mahakama ya Kadhi bado hawajafahamu nini tatizo la Wakristo, hata hawakubali kuwepo kwa Mahakama hiyo, siyo kweli kabisa kwamba Wakristo hudhani Mahakama hizo zitawahukumu wao, la hasha na Masheikhe hutumia muda mwingi kuwaelimisha juu ya hilo, wakati hilo sio tatizo lao, na ni udhaifu wa kutokujua madai au matatizo ya mpinzani wako, ni nini tatizo la Wakristo ni hili:
(a) Mkumbuke kwamba mwaka 1993 hapa Tanzania kulikuwa na mgogoro wa bucha za nguruwe, mgogoro huo ulizaa harakati kubwa za Waislamu ambazo makao yake makuu yalikuwa msikiti wa Mtoro na kiongozi mkuu alikuwa marehemu Kasim bin Juma. Waislamu walipinga kuwepo Ubalozi wa Vatican hapa Tanzania na bado wanaendelea na msimamo huo hadi leo, wakati ubalozi huo hauendeshwi kwa Fedha za walipa kodi wa Tanzania bali ni Vatican yenyewe. JE, ITAKUWAJE LEO WAKRISTO WAKUBALI ZIWEPO MAHAKAMA AMBAZO ZITATOA AJIRA KWA WAISLAMU, KUANZIA MTAA, KATA, TARAFA, WILAYA, MKOA HADI TAIFA, TENA KWA FEDHA ZA WALIPA KODI WA TANZANIA WAKIWAMO NA WAO WAKRISTO? Hilo ndilo tatizo lao na hapo ndipo BAKWATA wanatakiwa wapatolee maelezo.
(b) Kwamba, mabilioni ya Watanzania yatakayowalipa Masheikhe kila mwezi nao wao watanufaikaje? Huo ndio mgogoro uliotengenezwa na Ilani yenu na ambao unaweza kuwagharimu katika uchaguzi ujao wa mwaka 2010 ENDAPO WAKRISTO WAKIIGA MFANO WA WAISLAMU WA MSIKITI WA MTORO walipoamua kukusanya Kadi za CCM mwaka 1993 ingawa jaribio hilo lilizimwa na Viongozi wa CCM.

HOJA ZA SHEIKH BASALEH
15. Sheikh Ali Basaleh ndiye ambaye amelielewa tatizo la Maaskofu ingawa ametoa mfano mzuri wa kuwatuliza katika kipeperushi chake cha Wito cha tarehe18/08/2006. Ijumaa kuwa kama mtu ana watoto wawili mmoja anakula sana na mwingine hali sana, Je, baba atamzuia yule anayekula sana ili alingane na yule asiyekula sana? Mfano wake ni mzuri lakini haufanani na tatizo lililopo kwani fedha za baba hazichangiwi na watoto wake, bali baba huzitafuta yeye mwenyewe kwa nguvu zake, LAKINI FEDHA ZA BABA SERIKALI ZINATOKANA NA KODI YA WAISLAMU NA WAKRISTO, HIVYO SERIKALI HAIPASWI KUTUMIA FEDHA NYINGI KWA DINI MOJA LAZIMA ITALETA MGOGORO NA NDIYO MAANA SISI WAISLAMU TUMEKUWA TUKIDAI HAKI SAWA!

16. Katibu Mkuu ni matumaini yangu kuwa hekima itatumika katika kulitatua tatizo hilo kwani ni rahisi kuziba ufa kuliko gharama za kujenga ukuta mwisho nakutakia kazi njema pamoja na afya njema.

WABILAH TAUFIQ,
ASANTE.
USTADH A. S. MKAMBAKU,
KATIBU MKUU.
 
Back
Top Bottom