Mahakama ya Kadhi pinda hakusema ukweli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahakama ya Kadhi pinda hakusema ukweli

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Marunde, Dec 20, 2010.

 1. Marunde

  Marunde JF-Expert Member

  #1
  Dec 20, 2010
  Joined: Jun 9, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 60
  Wana JF mhe Pinda alionekana kuwahakikishia watz kuwa mahakama ya kadhi itaundwa chini ya system za dini ya kiisilam,laki makamu wa Rais Dr Bilal aliwahakikishia waisiilamu kuwa kiliochao kitaisha hivi karibuni na watafurahia matunda ya mahakama hiyo.Sasa mbona hawa viongozi wa juu wa serikali wanapishana kauli?.mwenye taarifa kamili atoe.
   
 2. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #2
  Dec 20, 2010
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Uncoordinated Government ambayo kila mtu akiamka anasema lake!!!! Kumbuka matamshi ya waziri wa sheria juu ya katiba mpya na tamko la waziri mkuu baada ya siku mbili kuhusu suala hilo hilo la katiba mpya. Sishangai kwamba Pinda anasema yake na makamu wa rais anasema vya kwake juu ya mahakama ya kadhi!!!

  Hiyo ndio serikali ya JK Bwana!!!!

  Tiba
   
 3. G

  George Jinasa JF-Expert Member

  #3
  Dec 23, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 393
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Mimi sioni msigano wowote kati ya kauli ya Waziri Mkuu na Makamu wa Raisi. Hamna hata mmoja aliyesema kwamba muundo wa mahakama ya kadhi utakuwaje wala hamna alisema kwamba suala la mahakama ya kadhi limeshafikia finality. Waziri Mkuu alisema kwamba bado serikali itaendelea kujadiliana na wawakilishi wa waislamu kuona inavyoweza kuanzishwa bila kuathiri sheria za nchi.
   
 4. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #4
  Dec 23, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Sina tatizo na uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi Tanzania,hii ni sehemu ya Ibada ya dini ya kiislamu ni vyema na haki waislamu wakatendewa haki kwani ni waTanzania kama walivyo wakristo.

  Kwakuwa Mahakama ya Kadhi ni Ibada ya dini ya KiIslamu ni vyema ikanzishwa na ikaendeshwa na waislamu wenyewe itakuwa jambo la ajabu kweli ikiwa mahakama ya Kadhi itaendeshwa na serekali kwa kutumia kodi za wananchi ambao wote si waislamu.Inasikitisha kusikia kuna watu wenye akili ndogo kuliko za kuku wanaotaka serekali ijishughulishe na Ibada za dini ya kiislamu.
   
 5. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #5
  Dec 23, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,504
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280

  Kumbe MS bado upo!!!!! Watu walikupakazia kuwa umekula ban la kudumu........Umechakachua nini??
   
 6. P

  Pamba Member

  #6
  Dec 23, 2010
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wote wmesema sawa mchakato unaendelea ili mahakama hiyo iendeshwe bila kuvunja sheria za nchi.ila itaanzishwa tu hata miaka mitano ijayo.
   
 7. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #7
  Dec 23, 2010
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Hii nchi si genge la wahuni! Kila kitu kina mpangilio wake na mwisho wa siku ni Serikali inayobeba jukumu ya mambo yote yawe ya muislamu au kristo. Umeshasema mahakama ,sasa una maanisha kuwa hii nchi itakuwa na aina yoyote ya mahakama bila ya serikali kuwa muangalizi. Hivyo kwa fikira yako pale serikali inapoingilia mila za makabila inafanya hivyo kwa minajili gani?

  Unafikiri bila ya Serikali kuweka mipaka na wajibu wa mahakama ya Kadhi kitu gani kitakuwa? Waislamu wanaweka mabomba kuitana kwa ibada mnakuja juu jee pale watoto wa nje ya ndowa watakapokataliwa urithi kwa kutokuwa na haki kidini mtanyamaza kimya? Msifikiri kuwa Waislamu wanahitaji kuhudumiwa katika kuendesha mahakama hizi bali wanachotaka ni kuhakikishiwa kuwa mahakama ya Kadhi ipo kisheria na haiwezi kupuuzwa inapotowa maamuzio yake. Nali hili linawasumbua?
   
 8. O

  Omulangi JF-Expert Member

  #8
  Dec 23, 2010
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 1,026
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Ndugu zangu mimi ni mkristo. Kama suala la mahakama ya kadhi hata kama ingekuwa kuingizwa katika sheria za nchi lingekuwa na lengo na mipaka kama tunayoambiwa mimi ningeunga mkono. Maana hadi hapo inaonekana harmless.

  Tatizo kubwa nyuma ya pazia ni hadith ya Mwarabu na ngamia. Kinachotafutwa ni serkali ya kiislamu. Ndivyo jihad ilivyo ina stages. Soma vizuri hata katika maisha ya mtume alianza kidogo kidogo. wakati mwingine alikuwa na torelance ya hali ya juu kwa waliokuwa kinyume naye ki imani. Lakini kwa kadri alivyopata nguvu ndivyo torelance ilivyokwisha. Hatimaye wasiokubali imani yake walikuwa wahanga wa upanga wake. Na kumbuka katika Koran aya mpya ilifuta aya za kale. Hivyo mtu aki quote aya inayoonyesha urafiki na ushirikiano mzuri lazima uangalie hakuna nyingine iliyofuta aya hii baadaye?

  Kutokana na utata huu waislamu wote wapenda amani na wakristo wenye uvumilivu kwa imani nyingine tusikubali kuingiza itikadi za dini katika utawala wa nchi. TUTAUMIA.:redfaces::redfaces::redfaces:
   
 9. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #9
  Dec 23, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  PInda ni kipaza sauti tu
   
 10. T

  Topical JF-Expert Member

  #10
  Dec 23, 2010
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  CCM hawawezi kukubali uwepo wa mahakama ya kadhi

  wanadanganywa tu hawa jamaa..kila siku wanadanganywa halafu hawaelewi..sheikh wenyewe wa Bakwata what do you expect wanataka kwenda kunywa chai kwa PM na Ikulu period! nothing serious will come out of it.

  waislamu watasubiri sana mahakama hiyo..siyo ccm itakayopa may be cdm//cuf can!
   
 11. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #11
  Dec 23, 2010
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Kadhi si mali kitu, watasubiri mpaka kihama
   
 12. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #12
  Dec 23, 2010
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Jambo la ajabu ni hilo la kutoa "Ultimatum" ya kuwa kodi isitumike, hivi hiyo kodi mnalipa nyie tu katika nchi hii ?, inaelekea kuna jamii mnaiona kama secon class citizen ! Ni hulka mbaya ya kibaguzi mnajijengea. Misamaha ya Kodi inayo wanufaisha nyie pekee ilipo pendekezwa kufutwa, ndio tulijua siri ya jinsi inavyo wanufaisha, wote mlihamia DODOMA. pengine choyo cha kutaka mfaidike nyie tu, ndio kinawasumbua
   
 13. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #13
  Dec 23, 2010
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Inshaallah Mwenyezi Mungu atahukumu juu ya hili baina yetu na wewe!
   
 14. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #14
  Dec 23, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  mkuuuuu upooo! Unaleta udini tena mkuu!
   
 15. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #15
  Dec 23, 2010
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Tatizo lenu kubwa ndio hilo, kuchukua maneno ya kijiweni kuleta humu. Ni kitabu gani wewe umewahi kusoma juu ya Uislaam cha aina yoyote au muandishi yoyote !?
  Labda kwa kukusaidia, wakati wa Mtume Muhammad s.a.w watu wa jamii nyingine na dini nyingine walikuwa wakienda kwake kuomba upatanishi au hifadhi. hayo yako umeyatowa wapi ? hebu tujuze kwa ushahidi tujifunze. Aya ipi imefuta ipi?
  Unajitosa kwenye bahari usiyo na ujuzi nayo ndugu yangu!
   
 16. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #16
  Dec 23, 2010
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Mnafurahisha sana ! mkitolewa mlango wa mbele, mnarudi tena kupitia wa nyuma! sijui vp ndugu zangu?
   
 17. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #17
  Dec 23, 2010
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Una sound kama "mtoa maamuzi" vile! jichunge ndugu yangu usijisahau hivyo!
   
 18. G

  George Jinasa JF-Expert Member

  #18
  Jan 24, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 393
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Wananchi wengine tunaojadili suala hili tunalijadili bila kuwa na uhuru. Ni kama vile tunashindana kwa misingi ya dini zetu zaidi kuliko maana na makusudi ya jambo lenyewe. Kama suala la mahakama ya kadhi lingekuwa ni suala ambalo halina maana yoyote kisheria na kisiasa bali ni suala la waislamu tu, lisingeanzishwa na Mrema ambaye ni Mkristo. Lisingekuwa katika Katiba ya Kenya ambako waislamu ni minority. Lisingekuwa katika mfumo wa sheria wa Uganda.

  Jambo ambalo wengi tunasahau kulifikiria kwa uzito wake ni kwamba Tanzania ni nchi yenye mchanganyiko wa watu wa mila, desturi, dini, kabila na siasa tofauti. Serikali pamoja na mfumo wake wakisheria na utawala kwa ujumla haitoki juu. Inatoka katika jamii ya watu hao hao mkanganyiko. Siri ya mafanikio ya serikali yoyote ni kuweza kuowanisha maslahi mbalimbali kinzani ndani ya nchi bila kuathiri mshikamano wa jamii. Ndio maana leo unasikia sheria za mila ni sehemu ya sheria halali za nchi, sheria za kiislamu ni sehemu ya sheria za nchi nk. Mtu mwingine angesema kuruhusu matumizi ya sheria za kiislamu Tanzania ni udini au sheria za kimila ni ukabila. Lakini hiyo ndiyo siasa. Ndio maana Pinda japo ni mukristo safi hachoki kushirikiana na waislamu kuona namna mahakama ya kadhi inavyoweza kuundwa na kutumika bila matatizo.

  Suala ambalo kwa wale wasiohusika na mahakama ya kadhi wangependa kulizingumza ni mbinu zitakazotumika ili Mahakama hizi zisiingiliane na maslahi yao na wala sio kupinga uwepo wake. Hata ile kufanya Jumapili na Jumamosi siku ya mapumziko wakati ijumaa ni siku ya kazi mtu mwenye tafsiri ya haraka haraka ya mambo kama wengi wetu tulivyo anaweza kusema udini kama yule anaedai kwamba kutumika kodi za wananchi kugharamia mahakama za kadhi ni udini. Siku mbili tunazokaa bila kazi zinalipotezea taifa kiasi gani cha fedha? Nani anaenufaika na mapumziko ya Jumapili? Nani anayenufaika na mapumziko ya Pasaka, Xmas na Idi? Xmas ni sikukuu ya waislamu, wapagani, wahindu na wasabato? Idi ni sikukuu ya wakristo, wapagani na wahindu? Hapo vipi?

  Msingi wa amani, upendo na utulivu wa watanzania na jamii nyingine yoyote ya kistaarabu ni kuvumiliana kutokana na tofauti zetu za kijamii, kiuchumi, kiimani na kadhalika. Ndio maana masikini wasio na magari hawalalamiki kulipa kodi zao na zikatumika kujenga barabara japo hawana magari wala hawasafiri safiri? Mimi sipendi mpira, lakini kodi yangu inatumika kujenga uwanja wa mpira. Mimi sipendi siasa lakini kodi yangu inatumika kulipa ruzuku katika vyama vya siasa. Kwa nini? Kwa sababu japo mimi spendi mpira wapo watanzania wenzangu wengi wanaopenda mpira. Japo mimi sipendi mahakama ya kadhi wapo watanzania wenzangu wengi wanapenda. Japo mimi sipendi kutofanya kazi jumapili wapo watanzania wenzangu wengi wanapenda kuitumia siku hiyo kumuabdu mungu na kupumzika. Waislamu wangependa ijumaa iwe siku ya mapumziko, wapagani labda wangependa j tatu. Lakini siku ziko saba tu katika wiki. Kwa kuwa nchi ilizaliwa ikakuta jumapili ni siku ya mapumziko, inabidi tuache hivyo bila kuleta kinyongo kwamba wakristo wanafaidi zaidi kiimani. Huo ndio upendo bwana Yesu alitufundisha kwamba 'Mpende jirani yako kama nafsi yako". Waislamu ni majirani kwa wakristo na kinyume chao. Hata kama kuna wengine kwa tafsiri zao za haraka haraka watasema vinginevyo, maandiko pia yanasema "mpende adui yako". Hapo vipi?
   
Loading...