Mahakama ya Kadhi: Mtikila kushindwa kesi, ndio mwisho wa mjadala?

NakuliliaTanzania

JF-Expert Member
Sep 24, 2007
555
7
Wakuu, wakati tunaendeela na mijadala ya mafisadi, kuna hili la mahakama ya kadhi

Nakumbuka siku zilizopita hapa tulikuwa na mjadala mzito kuhusu hili, na reent development zinaonyesha kuwa kesi hii aliyokuwa amefungua Mtikila, imefutwa na mahakama kuu,

Kilichonifanya nilete hii hoja hapa ni kutaka ufafanuzi wa maana na implication ya hii hukumu,

Je, ndo kusema mjadalaumefungwa,?

Kwa vile kesi imefutwa, bila kusikiliza hoja za mtikila za kwa nini mahakama hiyo isiwepo, na hasa uwepo wake ukiwa na mkono wa serikali isiyo na dini,na

Kwa vile Mtikila katika utetezi wake inaonekana alikosa milioni 4 za kumilipa wakili, na

kwa vile wanaharakati hawakujitokeza kumtetea/kumsaidia katika hili,

Ndio kusema kuwa:

Serikali sasa inaweza kuendela na mchakato wa kuanzaisha mahakama hiyo? au wakuu am missing apoint? naombeni msaada wenu maana honestly mi sio mwanasheria.
Mahakama Kuu yafuta Kesi ya Mahakama ya Kadhi Tanzania Na Tausi Ally

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam imeifuta kesi ya kikatiba ya kupinga kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi iliyofunguliwa na Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila.


Uamuzi wa kufuta kesi hiyo, ulifanywa na jopo la majaji watatu wa mahakama hiyo wakiongozwa na Jaji Kiongozi, Salum Masati aliyesaidiwa na Jaji Robert Makaramba na Jaji Aisha Nyerere baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwasilisha pingamizi la kutaka kesi hiyo ifutwe.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, aliwasilisha ombi la kufutwa kwa kesi hiyo, Novemba 15, mwaka jana akitaka kesi hiyo ifutwe na pia kumtaka Mchungaji Mtikila kujibu hoja hiyo.


Naye Mchungaji Mtikila aliwasilisha ombi katika mahakama hiyo, kuongezewa muda ili aweze kujibu hoja ya kufutwa kwa kesi hiyo na majaji walimruhusu na kupanga kusikilizwa maombi yake ya kutaka kuongezwa muda Februari 26, mwaka huu.


Baada ya ombi la Mchungaji Mtikila la kuongezewa muda, alifika katika mahakama hiyo na kuomba aongezewe muda mwingine kwa madai kuwa alikuwa hana wakili.


Wakili wa Serikali, Nickson Ntimbwa aliiomba mahakama itupilie mbali maombi ya Mtikila kwa madai kuwa ombi lake la kutaka aongezewe muda lilipangwa vibaya.


Mbali na ombi hilo, Ntimbwa aliiomba mahakama imwajibishe kwa kutofuata taratibu za kimahakama na kwamba ikiwezekana atiwe hatiani kwa kuidharau mahakama na kulipa faini.


Mchungaji Mtikila alijitetea akisema kuwa alijitahidi kufuata taratibu za mahakama, lakini alikuwa hana Sh4 milioni kwa ajili ya kumlipa wakili wa kumsaidia katika kesi hiyo.

Mtikila alidai kuwa mbali na ukosefu wa fedha mawakili na taasisi za haki za binaadamu walikuwa hawajisikii kumwakilisha katika kesi hiyo kwa ajili ya kumtetea.


Mchungaji Mtikila alifungua kesi hiyo, Oktoba 23, 2007 dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, akipinga kuanzishwa kwa mahakama hiyo.


Mtikila alifungua kesi hiyo kufuatia suala la kuanzishwa Makahama ya Kadhi kuwemo kwenye ilani ya uchaguzi (ya CCM) ya mwaka huu, ambayo inatumiwa na Serikali ya Awamu ya Nne kufikia malengo yake ya kuwapa maisha bora Watanzania.


Suala hilo pia liliwahi pingwa na maaskofu wote nchini kwa maelezo kuwa lina mwelekeo wa upendeleo kwa dini moja na kwamba linaweza kusababisha mgawanyiko wa kidini nchini

http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=4856
 
Atakata rufaa huyo, bila kesi hizi mtikila tutamsahau katika siasa za bongo!
 
Mahakama ya Kadhi ipatiwe ufumbuziMobini SaryaJUMATANO ya Machi 5, mwaka huu, Mahakama Kuu ya Tanzania ilitupilia mbali kesi ya kikatiba kupinga uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi hapa nchini, ambayo ilifunguliwa na Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila.

Ni wazi kuwa kuanzia sasa mjadala wa kuanzishwa Mahakama ya Kadhi utaanza upya baada ya Mahakama Kuu kutupa shauri hilo lililokuwa limefunguliwa na kusababisha mijadala yote kufungwa.

Jopo la majaji watatu, Robert Makaramba na Aisha Nyerere ambao waliongozwa na Jaji Kiongozi, Salum Masati, walitupilia mbali kesi hiyo, kwa kile walichokieleza kuwa ni mlalamikaji kutojitayarisha.

Wakati mjadala ukianza upya kati ya wale wanaopinga uanzishwaji wa mahakama hiyo, hasa Wakristo na wale wanaoitaka, maswali yameanza kuibuka kama kweli Mtikila kashindwa kuendesha kesi hiyo kama alivyonukuliwa au amerubuniwa.

“Baada ya kupitia kwa kina hoja za pande zote mbili, jopo hili linaamua kutupilia mbali kesi hii, kwa sababu mlalamikaji ameonyesha hajajitayarisha kuendelea na kesi hii,” alisema Jaji Masati wakati akisoma hukumu hiyo.

Kauli ya jopo hilo la majaji ndio inazidi kuibua hisia nzito kwenye jamii kama hiyo kesi haikuwa na msukumo wowote wa kisiasa na wa kimaslahi yaliyoifikisha hapo ilipofika.

Oktoba mwaka jana, Mchungaji Mtikila alifungua kesi ya kikatiba namba 80/2007 katika mahakama hiyo, dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, akitaka mahakama hiyo iwaadhibu watu waliopo serikalini wanaokiuka katiba kwa kushiriki kwao katika harakati za kuanzisha Mahakama ya Kadhi.

Kwa mujibu wa hati ya madai, walalamikaji walieleza kuwa, Wizara ya Katiba na Sheria na Bunge kujihusisha kwa namna yoyote na masuala ya Mahakama ya Kadhi ni kinyume cha katiba, kwa sababu mahakama hiyo ni chombo cha Kiislamu.

Kutokana na kesi hiyo, mijadala yote ilipigwa marufuku, hata kwenye vyombo vya habari, hapo ndipo zikaibuka habari za chini chini kuwa huenda Serikali ya Rais Jakaya Kikwete ilikuwa imemtumia Mtikila kwenda mahakamani kufungua kesi hiyo ili kumuokoa na hasira za Wakristo ambao walikuwa wameanza kuja juu.

Na hasira za Wakristo zilidhihirika baada ya Mtikila kufungua kesi hiyo na kukumbana na vitisho vya Waislamu, wakimtuhumu kuingilia mambo yao, hali iliyofanya Wakristo nao waje juu kabla mahakama haijaingilia kati na kuzima huo mjadala.

Wakati tukijiuliza sababu ya Mtikila kushindwa kuendelea na kesi, huku yeye akinukuliwa akilalama kwamba hakuwa na uwezo wa kuwalipa mawakili wake - kiasi cha sh milioni moja, bado kuna masuala mengine yanajitokeza.

Kwanza, Mchungaji Mtikila amekuwa na uzoefu wa kufungua kesi za kikatiba kwa muda mrefu, kwa hiyo anafahamu gharama zake, ilikuwaje afungue kesi anayojua kuwa atashindwa kuiendesha kwa maana ya kukosa pesa?

Pili, wakati Mtikila alipofungua kesi, walijitokeza watu waliojiita Umoja wa Wakristo aliosema kwamba wangemsaidia kwa kila hali, wako wapi sasa?

Mtikila anataka umma umwamini kuwa amekosa mtu wa kusaidia gharama za kesi, kwani ni mara yake ya kwanza kufungua kesi?

Lakini kwa upande wetu sisi tumeweka macho, ipo siku ukweli utabainika na umma utakijua kilichomtuma Mtikila afungue kesi hiyo halafu baadaye ashindwe kuendelea nayo.

Lakini muhimu hapa tunalotakiwa kulijadili ni hoja ya msingi kuhusu kuanzisha Mahakama ya Kadhi ambayo imo kwenye Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakati wakimnadi mgombea wao Rais Kikwete.

Tuijadili hoja hiyo kwani sasa fikra zetu zimefunguliwa ziko huru kufanya hivyo kutokana na kesi hiyo kuwepo mahakamani.

Tunataka Rais Kikwete atamke wazi mkakati alionao juu ya uanzishwaji wa mahakama hiyo bila kupoteza muda na kama haiwezekani.

Pia katika hili suala la uanzishwashi wa mahakama inayoshughulikia masuala ya dini ya Kiislamu, viongozi wa Kikristo wanapaswa kutojiingiza kwenye swala hilo wakaonekana vigeugeu.

Kwani itakumbukwa kuwa Agosti mwaka jana, magazeti kadhaa ya Wakristo yaliwanukuu viongozi wa madhehebu ya Kikristo wakimnadi Kikwete kwenye madhabahu kuwa ni ‘Masiha’, yaani mti wa mafuta ya bwana wao, wakitumia neno rahisi kuwa ni chaguo la Mungu.

Leo inakuwaje mtu ambaye ni chuguo anayefanya kazi kwa muongozo wa Mungu aingiliwe kwenye shughuli zake za kiutendaji, wakimuonya kuwa asijishughuliushe kuirejesha Mahakama ya Kadhi?

Viongozi wa Kikristo wangeonekana wana hoja kama Rais Kikwete angekuwa na mpango wa kupitisha sheria ya kuruhusu ndoa za ushoga, hapo tungesema kuwa kiongozi wa Mungu hawezi kubariki mambo ya kishetani.

Lakini kwa suala la Mahakama ya Kadhi ambayo ipo kwa mujibu wa maandiko ya dini ambayo yanaaminika kuwa ni maagizo ya Mungu kuja kwa wanadamu, Kikwete anapaswa kuachwa alitekeleze kwani viongozi hao ndio walituambia kuwa alitumwa na Mungu.

Hebu tujiulize kama kiongozi aliyetajwa na kushuhudiwa jana kuwa ametumwa na Mungu, leo anataka kufanya yale ya Mungu anazuiliwa, tutawaelewaje wale mashuhuda wake? Ni vigeugeu.

Kama walitaka kupata chochote kutoka kwake na sasa wamekwisha kupata wanamgeuka, waseme wazi ili tuwapige mawe mchana kweupe.

Mahakama ya Kadhi lazima ianzishwe kwenye utawala huu wa Kikwete, kwani kila kiongozi wa serikali hii amekuwa akijinadi kuwa wanatekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ambayo kwayo twapata maandiko yanayoitaja mahakama hiyo.

Hata yale matamshi aliyoyatoa Kikwete katika Kanisa la Kilutheri Tanzania, Azania Front, siku aliposimikwa Askofu Mkuu Alex Malasusa, kwamba yeye hakuhusika kutengeneza hiyo Ilani, yanapaswa kupuuzwa.

Kikwete akijua kuwa yeye ni Muislamu, alikwenda kupanda kwenye jukwaa la Wakristo na kujinadi sawa na mtu anayeomba kura kwao kuwa, wanaopaswa kulaumiwa kuhusu Ilani ya CCM ni Rais mstaafu Benjamin Mkapa na Kingunge Ngombale Mwiru, kwamba ndio waliingiza suala la kadhi kwenye ilani.

Kwa mtu mwengine anapaswa kurudi nyuma na kujihoji kuwa, Mkapa na Kikunge waliitengeneza ilani hiyo ili wamnadi nani? Bila shaka jibu linakuja kuwa ni Kikwete. Je, Kikwete anataka kutuambia kuwa alikabidhiwa Ilani bila kuipitia? Tunataka sasa suala la Mahakama ya Kadhi lipatiwe ufumbuzi.

0753 399 579
mobinsons@yahoo.com
www.mobiday.blgogspot.com

http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/3/8/makala3.php
 
Kutokana na kesi hiyo, mijadala yote ilipigwa marufuku, hata kwenye vyombo vya habari, hapo ndipo zikaibuka habari za chini chini kuwa huenda Serikali ya Rais Jakaya Kikwete ilikuwa imemtumia Mtikila kwenda mahakamani kufungua kesi hiyo ili kumuokoa na hasira za Wakristo ambao walikuwa wameanza kuja juu.

Tna safari ndefu kwenye taaluma ya uandishi Tanzania, lakini tutafika tu....
 
KHIDMAT DWAAT LISIAMIYAT CENTRE REGISTERED TRUSTEES
P. O. BOX 16106, MOB. 0713-290272, 0784-403020.


1. Uanzishaji wa Mahakama ya Kadhi utaleta madahara makubwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa vile Wakristo hawagawanyiki katika suala la kuipinga, lakini sisi Waislamu tunagawanyika katika suala hilo. Kwa taarifa yako napenda nikuhakikishie kuwa Waislamu wa Madhehebu ya AnsarSunna HAWAIKUBALI Mahakama hiyo kwa vile wanaelewa kuwa itakuwa chini ya BAKWATA.

2. Pia wanaelewa kuwa miongoni mwa mamlaka ya Kadhi ni kutangaza mwezi wa Ramadhani kufunga na kufungua na wao wanaye Amir wao ambaye hutangaza mwezi kwa kufuata mwezi unaoandama Saudia (Saud Arabia). Kwa maana hiyo katika nchi yenye Kadhi kutokea mtu mwingine nje ya Kadhi kutangaza mwezi ni kosa la jinai.

3. Kitu ambacho kitaleta madhara makubwa kuliko mafanikio ingawa AnsarSunna ni kundi dogo lakini wanaburuza kundi kubwa sana la Waislamu, kuliko Taasisi yoyote ya Kiislamu hapa Tanzania kwa vile ushawishi wao ni mkubwa sana katika jamii ya Kiislamu.

4. ANSAR SUNNA ndio wanaoendesha Shuura ya Maimam, GAZETI LA AN-NUUR, AL-HUDA, NASAHA na RADIO IMANI. Pia wana ushawishi mkubwa TIMES FM. Je, BAKWATA wana uwezo wa kupambana na vyombo hivyo?

5. Je, Serikali inaweza kukabidhi Mahakama ya Kadhi kwa wanaharakati wa Kiislamu? Nina hakika haiwezi kufanya jambo hilo na kama haitofanya hivyo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaweza kupata hasara zifuatazo:
(a) Wakristo wote wanaweza kujitoa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga katika chama cha CHADEMA ambacho hakina Mahakama ya Kadhi katika Ilani yake.
(b) Waislamu wote walioko chini ya Shuura ya Maimamu ambayo ni Mpinzani Mkuu wa BAKWATA wataendelea kuipinga Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa kuikumbatia BAKWATA na huku wakiendelea kuiunga mkono CUF, hivyo CCM itajikuta imebakia na Waislamu wanaoiunga mkono BAKWATA tu. Suala la wanaharakati kuipinga Mahakama ya Kadhi ni jambo rahisi sana kwa vile Mahakama ya Kadhi sio madai yao ya msingi.

6. Waislamu (wanaharakati) dai lao la msingi ni MGAWANYO SAWA WA MADARAKA. Hivyo Serikali inapounda Wizara, wao hutizama Baraza la Mawaziri, WAISLAMU NI WANGAPI NA WAKRISTO NI WANGAPI NDIO MAANA WANAIUNGA MKONO CUF, KWA VILE CUF IMEELEWA TATIZO LAO NA WAO WAKAJA NA KAULIMBIU YA HAKI SAWA KWA WOTE, yaani kwa Wakristo na Waislamu, wala Ilani ya Uchaguzi ya CUF haisemi lolote kuhusu Mahakama ya Kadhi WALA HAITOSEMA!!

7. Pia Waislamu wanaharakati wanaelewa kuwa Mahakama ya Kadhi haina manufaa yoyote kwa Waislamu, kwa vile Zanzibar ipo na WAISLAMU WA ZANZIBAR HAWANA MAENDELEO YOYOTE KUWAPITA WALE WA BARA, NA UISLAMU SI NDOA NA MIRATHI TU WALA MUNGU HASEMI "SOMETHING IS BETTER THAN NOTHING." Huu ni msemo wa Wazungu.

8. Mwenyezi Mungu anasema: INGIENI KATIKA UISLAMU WOTE NA MSIFE BALI MMEKUWA WAISLAMU KAMILI (Surat Baqarah ya 2 aya ya 208). Kwa hiyo mimi nikiwa kama Mwislamu nashauri kuwa Mahakama hiyo ISIWEPO kwani haitakuwa na manufaa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) na italeta mgawanyiko miongoni mwa wanachama wako, chukulia mfano Zanzibar, Mufti na Kadhi wanavyopingwa na wanauamsho ambao wanaongozwa na Sheikh Farid hali wanauamsho ndio Shura ya Maimam na Shuura ya Maimam ndiyo Uamsho.

KWANINI MASHEIKH WA BAKWATA WANAITAKA?
9. Wanaelewa wanachokifanya, wao wanajua fika kuwa Serikali itakapoanzisha Mahakama ya Kadhi watakuwa wamepata AJIRA, kwa hiyo wao wanapigania maslahi yao tu, hawawezi kuangalia madhara yatakayokikumba Chama Cha Mapinduzi (CCM) na huku wakijua kuwa ushawishi wao ni mdogo katika Jamii ya Kiislamu na hawana hata Miundumbinu ya kuwashawishi Waislamu wote waweze kumkubali Mufti, na hali ya Mufti ameshaweka wazi milango kwa Taasisi zote za Kiislamu na Waislamu waje washirikiane naye.

10. Masheikhe hawa wanaelewa kuwa hakuna Hakimu anayehukumu makosa mawili tu, yaani NDOA na MIRATHI, ukiletewa mzinifu huruhusiwi kumhukumu, ukiletewa mwizi huruhusiwi, nk. lakini wanang'ang'ania hivyo hivyo kwa ajili ya mishahara tu na hiyo ni hatari.

11. Hujaribu kutoa hata mifano ya Serikali ya Uingereza kwamba mwaka 1920 iliweka Mahakama hizo, ukweli ni kwamba Serikali ya Uingereza haikuweka Mahakama za Kadhi tu bali za Maakida na Maliwali, lakini pia sababu ya kuziweka Mahakama hizo siyo kwa ajili ya kuutunza Uislamu au uliwali bali ilikuwa ni mbinu ya kuwatuliza Viongozi hao ili waweze kuwatawala bila vurugu kwani mkoloni aligundua kuwa ni watu wenye ushawishi katika jamii kwa hiyo ile ilikuwa ni mbinu ya kiutawala ili Masheikhe, Maliwali na Maakida wajione kuwa na wao ni sehemu ya Serikali ya Muingereza, kumbe ni watawaliwa, hivyo bado hoja hiyo haina msingi wowote wala haina maana kwamba Serikali ya Mkoloni ilikuwa nzuri kwa Waislamu kuliko hii ya CCM, na huku tukiambiwa kuwa Waislamu ndiyo walioanzisha harakati za kudai Uhuru, kama walikuwa wazuri kwa nini tuliwaondoa.

12. CCM inayo mambo mengi ya kujivunia kwa Waislamu kama vile kuwapatia Chuo Kikuu, na hilo ni jambo muhimu na la msingi kwa maendeleo ya Uislamu na Waislamu, kwa hiyo JAMBO HILO LA MAHAKAMA YA KADHI mnapaswa kuliangalia kwa umakini ijapokuwa limo ndani ya Ilani yenu. Lakini si kila jambo lililomo ndani ya Ilani litekelezwe, mengine yanaweza kushindikana kwa matatizo mbalimbali na hili ni tatizo kubwa KWANI LINAWEZA KUZAA MGOGORO WA KIDINI!!

WAKRISTO WANA HAKI YA KUPINGA MAHAKAMA YA KADHI
13. Sehemu kama Zanzibar ni rahisi kuweka Mahakama ya Kadhi kwa vile Waislamu kule ni asilimia 99.99 hali kama hiyo Wakristo kule ni kama hawapo wamemezwa kwa uchache wao. Lakini BARA NI PAGUMU kwa vile HUENDA WAKRISTO NI WENGI KULIKO WAISLAMU. KWA VILE WAISLAMU KWA UHAKIKA HUPATIKANA MIKOA ISIYOZIDI SITA AMBAYO NI DAR ES SALAAM, LINDI, TANGA, MTWARA, KIGOMA NA TABORA, pia katika mikoa hiyo siyo Wilaya zote, kwa mfano Mkoa wa Kigoma ni Ujiji na Kigoma Mjini tu.

14. Pamoja na hayo Masheikhe wa BAKWATA wanaoshikilia suala la kuwepo kwa Mahakama ya Kadhi bado hawajafahamu nini tatizo la Wakristo, hata hawakubali kuwepo kwa Mahakama hiyo, siyo kweli kabisa kwamba Wakristo hudhani Mahakama hizo zitawahukumu wao, la hasha na Masheikhe hutumia muda mwingi kuwaelimisha juu ya hilo, wakati hilo sio tatizo lao, na ni udhaifu wa kutokujua madai au matatizo ya mpinzani wako, ni nini tatizo la Wakristo ni hili:
(a) Mkumbuke kwamba mwaka 1993 hapa Tanzania kulikuwa na mgogoro wa bucha za nguruwe, mgogoro huo ulizaa harakati kubwa za Waislamu ambazo makao yake makuu yalikuwa msikiti wa Mtoro na kiongozi mkuu alikuwa marehemu Kasim bin Juma. Waislamu walipinga kuwepo Ubalozi wa Vatican hapa Tanzania na bado wanaendelea na msimamo huo hadi leo, wakati ubalozi huo hauendeshwi kwa Fedha za walipa kodi wa Tanzania bali ni Vatican yenyewe. JE, ITAKUWAJE LEO WAKRISTO WAKUBALI ZIWEPO MAHAKAMA AMBAZO ZITATOA AJIRA KWA WAISLAMU, KUANZIA MTAA, KATA, TARAFA, WILAYA, MKOA HADI TAIFA, TENA KWA FEDHA ZA WALIPA KODI WA TANZANIA WAKIWAMO NA WAO WAKRISTO? Hilo ndilo tatizo lao na hapo ndipo BAKWATA wanatakiwa wapatolee maelezo.
(b) Kwamba, mabilioni ya Watanzania yatakayowalipa Masheikhe kila mwezi nao wao watanufaikaje? Huo ndio mgogoro uliotengenezwa na Ilani yenu na ambao unaweza kuwagharimu katika uchaguzi ujao wa mwaka 2010 ENDAPO WAKRISTO WAKIIGA MFANO WA WAISLAMU WA MSIKITI WA MTORO walipoamua kukusanya Kadi za CCM mwaka 1993 ingawa jaribio hilo lilizimwa na Viongozi wa CCM.

HOJA ZA SHEIKH BASALEH
15. Sheikh Ali Basaleh ndiye ambaye amelielewa tatizo la Maaskofu ingawa ametoa mfano mzuri wa kuwatuliza katika kipeperushi chake cha Wito cha tarehe18/08/2006. Ijumaa kuwa kama mtu ana watoto wawili mmoja anakula sana na mwingine hali sana, Je, baba atamzuia yule anayekula sana ili alingane na yule asiyekula sana? Mfano wake ni mzuri lakini haufanani na tatizo lililopo kwani fedha za baba hazichangiwi na watoto wake, bali baba huzitafuta yeye mwenyewe kwa nguvu zake, LAKINI FEDHA ZA BABA SERIKALI ZINATOKANA NA KODI YA WAISLAMU NA WAKRISTO, HIVYO SERIKALI HAIPASWI KUTUMIA FEDHA NYINGI KWA DINI MOJA LAZIMA ITALETA MGOGORO NA NDIYO MAANA SISI WAISLAMU TUMEKUWA TUKIDAI HAKI SAWA!

16. Katibu Mkuu ni matumaini yangu kuwa hekima itatumika katika kulitatua tatizo hilo kwani ni rahisi kuziba ufa kuliko gharama za kujenga ukuta mwisho nakutakia kazi njema pamoja na afya njema.

WABILAH TAUFIQ,
ASANTE.
USTADH A. S. MKAMBAKU,
KATIBU MKUU.

Aisee umeelewela hii post ingebandikwa kila mtaa ni ilmu tosha
 
Nikiwa kama miislamu.......
Nakubaliana 100% na hili bandiko. Kila nikitafakari sioni uhitaji wa mahakama ya kadhi kwa waislamu. Naona tu jinsi tunavyopeleka mambo kwa kuiga nchi nyingine bila kuangalia maxingira ya kwetu.
Hata ije leo... mimi sitakuwa miongoni mwa wahukumiwa wake na ninahisi hii ni mbinu ya baadhi ya wanazuoni wa bakwata na kundi fulani la wanasiasa kutaka kumega mnofu wa taifa ambao wanahisi WAKRISTU wanaumega zaidi. Sina uhakika sana na uwepo au kutokuwepo kwa MFUMO KRISTO hapa tanzania ila najua kwa dhati kabisa kuwa Kadhi hataleta mabadiliko yoyote yatakayouondoa huo mfumo kristo unaoongelewa.
Ki ujumla, mahakama ya kadhi haitakuwa na -ve wala +ve impact kwa watanzania wa dini yoyote zaidi ya kuleta mtafaruku wa wale wasio waislamu kuona kuwa waislamu wanapendelewa.
Haka ka nchi kana matatizo ya ki-utumwa. Watu wako tayari kugombana kwa sababu ya imani zilizoletwa na MAJAHAZI na mungu ambaye hatujawahi kuona uwezo wake zaidi ya kukaririshwa uwezo wake ulioshukia mashariki ya kati. Amkeni...... jifungueni minyororo ya utumwa wa kiimani,kiakili na kifikra
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom