Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu yamthibitisha Benjamin Sitta kuwa Meya wa Kinondoni

dr.malulu

Senior Member
Jun 26, 2013
133
60
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemtambua Mh. Benjamin Sitta kuwa meya wa Kinondoni. Hukumu hiyo imetolewa leo baada ya mahakama kutupilia mbali hoja za upande wa pili (Ukawa).

Kama mnakumbuka siku ya uchaguzi polisi waliwakamata baadhi ya viongozi na wajumbe wa UKAWA sambamba na ongezeko la wajumbe batili upande wa CCM akiweno Dr. Tulia.

Kesi hii ilifunguliwa dhidi ya Afisa Utawala wa Manispaa ya Kinondoni, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamini Samweli Sita ( aliyetangazwa kuwa Meya) na Manyama Mangaru ( aliyetangazwa kuwa Naibu Meya)

Rejea uzi: CHADEMA imefungua kesi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kupinga ushindi Meya wa Kinondoni
 
Kwani hapo kabla nani alikuwa Meya, toa maelezo ya kutosha kuhusu mwenendo wa mgogoro hadi kufungua kesi ilikuwaje hadi wapokonywe huo Umeya.

Sio wote tunaufahamu huo mgogoro.!
 
Mahakama za nanihii anaitwa nani vile?? Utategemea nini??
 
Mahakama ya hakimu mkazi kisutu imemtambua Mh. BENJAMIN MITTA kuwa meya wa kinondoni. Hukumu hyo imetolewa leo baada ya mahakama kutupilia mbali hoja za upande wa pili. Ukawa.

Kama mnakumbuka siku ya uchaguzi police walisakamata baadhi ya viongoz na wajumbe wa ukawa, sambamba na ongezeko la wajumbe batili upande wa ccm akiweno Mh. TULIA

Kwisha kabsaa....
Wakate rufaa. Waachane na mahakama uchwara zilizoamua kusaliti taaluma na utu kwa sababu ya unafiki na kujipendekeza. Wanasahau kwamba unafiki hauna furaha wa amani na amani ni bora kuliko sifa.
 
Hakika nimeshtushwabna hukumu ya kesi ya kupinga matokeo ya Uchaguzi wa Meya wa Manispaa ya Kinondoni iliyotolewa Leo ktk Mahakama ya Kisutu.Pamoja Na Wajumbe wa Ukawa kukamatwa, Mjumbe asiye mkazi wa Kinondoni kuruhusiwa kupiga kura, kikao kuvurugika Na kubaki wanaccm Na kumteua Mh.Sitta kuwa Meya wa Kinondoni Mahakama Leo imebariki uchaguzi huo Na kumthibitisha Mh.Sutta kuwa in Meya wa kinondoni.Hongera sana CCM Kwa ushindi.
 
Hivi kama yale mapungufu yote yaliyozingira mchakato wa uchaguzi wa umeya wa Kinondoni Mahakama inaona hakuna shida, ni njia gani nyingine unayoweza kumshawishi mwananchi mwenye fikra huru kuipenda nchi kama hii!?
Kama ni hivi basi tungojee na tamko la mahakama kuwa 'hakuna njaa' na atakayesema ipo ni jela siku 93 bila faini.
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemtambua Mh. Benjamin Sitta kuwa meya wa Kinondoni. Hukumu hiyo imetolewa leo baada ya mahakama kutupilia mbali hoja za upande wa pili (Ukawa).

Kama mnakumbuka siku ya uchaguzi polisi waliwakamata baadhi ya viongozi na wajumbe wa UKAWA sambamba na ongezeko la wajumbe batili upande wa CCM akiweno Dr. Tulia.

Kwisha kabisaa....
KWA MWENDO HUU, MAHAKAMA HIZI, LISU ATAFUNGWA! LISU KAA UKILIJUA HILI
 
Hakika nimeshtushwabna hukumu ya kesi ya kupinga matokeo ya Uchaguzi wa Meya wa Manispaa ya Kinondoni iliyotolewa Leo ktk Mahakama ya Kisutu.Pamoja Na Wajumbe wa Ukawa kukamatwa, Mjumbe asiye mkazi wa Kinondoni kuruhusiwa kupiga kura, kikao kuvurugika Na kubaki wanaccm Na kumteua Mh.Sitta kuwa Meya wa Kinondoni Mahakama Leo imebariki uchaguzi huo Na kumthibitisha Mh.Sutta kuwa in Meya wa kinondoni.Hongera sana CCM Kwa ushindi.

Unajua Mpira wa kona ukitia kichwa tu. Goli.

Ndio nchi yetu hiyo.
 
Ccm hawataacha magoli ya mkono mpaka sisi wananchi tutakapoanza kupiga kura na kulinda kura zetu kwa nguvu zetu zote
 
Kuna mambo mengi mwanadamu huwa anasahau.Moja na kubwa ni hili "Hapa Duniani tunapita,fahari ya mwili na ukwasi wa mali si lolote,vyeo na madaraka ni kama upepo,huvuma na kutoweka"

Mungu aliumba ugonjwa na kifo ili kuwakumbusha wanadamu kuwa hapa duniani si makazi yao ya kudumu.Watende kwa haki na bila dhurma.Lakini wanadamu tunajisahau sana.

Hakuna ulevi mbaya kama ule wa madaraka ya kimwili...Afadhali hata ule wa mvinyo,unawezea kuondoa "hangover" kwa supu au mchemsho.

Bwana mdogo alipaswa kukumbuka...Alipopelekwa Ujerumani alikuwa first Classa...Alivyorudi alikuwa kwenye "hold" ya ndege akiwa amechanganywa na mizigo na mabegi ya abiria.Na juu ya jeneza paliandikwa "The Remains of ..... ".Maana yake yaliyopo pale ni mabaki tu,mwili umeacha roho na kilichobaki ni mzoga tu.

Akiyakumbuka haya,atajifunza kuachana na mtindo wa kujiingiza katika dhurma za kimadaraka angali kijana mdogo.Maana hayo anayoyapapatikia na yale ya ulimwengu wa mwili,ambayo hayadumu milele.
 
Ni mahakama hizi hizi ambazo zinafunga Wapinzani ambao wanaonekana hatari kwa Utawala na kuwapa ushindi wa Mezani watawala katika kesi kama hizi.
 
Back
Top Bottom