Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu imetoa uamuzi wake uliosubiriwa kwa muda mrefu kuhusu shauri lililopinga uhalali wa uchaguzi mkuu wa Tanzania wa mwaka 2020.
Katika hukumu yake, mahakama hiyo imetupilia mbali kesi hiyo kwa kukosa mashiko ya kisheria na ushahidi thabiti.
Wapinga uchaguzi walidai kuwa mchakato wa kura ulikumbwa na dosari na ukiukaji wa misingi ya kidemokrasia.
Hata hivyo, mahakama imebainisha kuwa madai hayo hayakuungwa mkono na vielelezo vinavyokidhi viwango vya kisheria, na hivyo kuyafanya yasiwe na msingi wowote wa kisheria.
Pia soma
Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu kesho Machi 6, 2026, kutoa hukumu ya uhalali wa uchaguzi wa Tanzania 2020
06 March 2026
Arusha Tanzania
Tanzania yaamriwa kurekebisha Katiba ili kuruhusu malalamiko ya uchaguzi wa urai
Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu imeiagiza Tanzania kurekebisha kifungu cha katiba kinachozuia mahakama kusikiliza kesi zinazopinga matokeo ya uchaguzi wa rais.
Katika hukumu iliyotolewa Machi 6, 2026 jijini Arusha, Mahakama iliamua kwamba Kifungu cha 41(7) cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kinakiuka vifungu vya Mkataba wa Afrika kuhusu Haki za Binadamu na Watu, hasa haki ya kutafuta suluhu ya kisheria na kesi kusikilizwa mbele ya vyombo vya kitaifa vyenye uwezo.
Kifungu hicho kinasema kwamba
“Mgombea anapotangazwa na Tume ya Uchaguzi kuwa amechaguliwa ipasavyo kwa mujibu wa Kifungu hiki, basi hakuna Mahakama ya sheria itakayokuwa na mamlaka yoyote ya kuchunguza uchaguzi wa mgombea huyo.”
Kesi hiyo iliwasilishwa Mahakamani na waombaji Ado Shaibu na wenzie 6 waliodai kwamba kifungu hicho kinawanyima raia fursa ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais kupitia mahakama.
Kulingana na waombaji Ado Shaibu & Wenzie 6, kuendelea kuwepo kwa Kifungu cha 41(7) kunakiuka haki ya kutobaguliwa, ulinzi sawa wa sheria na haki ya kusikilizwa kwa kesi, ikiwa ni pamoja na haki ya kukata rufaa dhidi ya vitendo vinavyokiuka haki za msingi.
Katika uamuzi wake, Mahakama ya Afrila ilikubaliana na waombaji na kugundua kuwa kifungu hicho kinapunguza upatikanaji wa haki na kinawanyima raia fursa ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais kupitia njia za kisheria.
Kwa hivyo Mahakama iliamua kwamba Tanzania lazima irekebishe kifungu cha katiba ili kuhakikisha kwamba matokeo ya uchaguzi wa rais yanaweza kupingwa mbele ya mahakama, sambamba na kanuni za Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu.
Amri ya Mahakama
Katika uamuzi wao, kikao cha majaji saba jijini Arusha kiliamuru Nchi Inayojibu kuchukua hatua zote muhimu za kikatiba na kisheria ili kuhakikisha kwamba Kifungu cha 41 (7) cha Katiba kinarekebishwa na kuendana na vifungu vya Hati.
Mahakama pia iliagiza serikali kuwasilisha ripoti ndani ya miezi kumi na miwili baada ya hukumu iliyotolewa ikielezea hatua zilizochukuliwa kutekeleza uamuzi huo, na baada ya hapo kuwasilisha ripoti za ziada kila baada ya miezi sita hadi Mahakama itakaporidhika kwamba uamuzi huo umetekelezwa kikamilifu.
Tanzania pia iliamriwa kuchapisha hukumu hiyo ndani ya miezi mitatu kuanzia tarehe ya taarifa hiyo kwenye tovuti rasmi za Mahakama na Wizara ya Masuala ya Katiba na Sheria.
Mahakama iliagiza zaidi kwamba hukumu hiyo iendelee kutundikwa / postiwa hadharani kwenye majukwaa hayo kwa angalau mwaka mmoja baada ya kuchapishwa.
Uamuzi huo unatarajiwa kuwa na athari kubwa kwa uwajibikaji wa uchaguzi nchini Tanzania, kwani unafungua mlango wa matokeo ya uchaguzi wa rais kupingwa mahakamani, jambo ambalo limepigwa marufuku kwa muda mrefu chini ya mfumo wa sasa wa kikatiba