Mahakama ni kichaka cha serikali cha kujificha

mangifera

Member
Oct 15, 2011
47
34
[h=2]Mahakama ni kichaka cha serikali cha kujifichia[/h]
Kuna imani kuwa taifa limeundwa na mihimili mitatu mikuu yaani BUNGE, MAHAKAMA na EXECUTIVE(BARAZA LA MAWAZIRI) ambalo rais ndo mwenyekiti. Tunadanganywa kuwa mihimili hii ni huru, yaani haiingiliani katika maamuzi na kazi zake. Lakini tunachoshuhudia si kweli. Ni vigumu mtanzania kutofautisha kati ya katibu mkuu wa CCM, jaji wa mahakama, waziri au spika wa bunge. Wote wanafanana kiitikadi kisera na kimtizamo. Na huenda wanakula meza moja.
Ukiangalia upande wa mahakama ndiyo mbaya kabisa, viongozi wote wa juu kuanzia jaji mkuu huteuliwa na Rais ambaye ni mwenyekiti wa chama tawala. Rais huingilia kwa urahisi sana maamuzi ya mahakama kama tulivyoona alivyoingilia mgomo wa madaktari kwa kutoa maamuzi huku akitudanganya kuwa kesi iko mahakamani. Mahakama haijakemea wala kusema lolote. Pia muhimili mwingine wa serikali ambao ni bunge kwa kupitia spika umekuwa ukiilinda sana serikali(executive) pale ambapo amekuwa akiitetea serikali au kuzuia majadiliano yoyote katika hoja ambayo serikali inaelekea kushindwa.
Hata pale ambapo waziri mkuu aliulizwa swali la msingi la kutakiwa ajiuzulu kwa kushindwa kutatua matatizo ya wananchi (mgomo) spika alimlinda kwa kumwambia "hilo usijibu mh. W/K"

Sasa tunashuhudia serikali kuitumia mahakama kama kichaka chake cha kujificha baada ya kushindwa kutatua matatizo ya afya za wananchi na madaktari kwa kufungua kesi za uongo zisizokuwa na kichwa wala miguu, yaani kosa kafanya kenge, anashtakiwa mjusi eti kwa sababu wote ni damu baridi na wana magamba. Kila ikiambiwa jibuni hoja wanasema kesi ipo mahakamani. Lakini wakitaka kujinufaisha huvunja mwiko wa mahakama bila kuulizwa!!

Kwa sababu hii mahakama inatumika kama kichaka cha serikali kujifichia na imeshafanya hivyo mara nyingi hata wakati ule wa mgomo ulioitishwa na TUCTA.​
 
Back
Top Bottom