Mahakama na kesi za UHUJUMU UCHUMI (UFISADI)! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahakama na kesi za UHUJUMU UCHUMI (UFISADI)!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Honey K, Jun 13, 2012.

 1. H

  Honey K JF-Expert Member

  #1
  Jun 13, 2012
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Iko haja ya kuangalia upya mfumo wa mahakama zetu! Kesi za utumiaji mbaya wa madaraka, rushwa, ufisadi na uhujumu uchumi zisichukue muda mrefu bila kutolewa maamuzi. Kwanza ni hasara kwa serikali na nchi na haitoi mafunzo kwa kizazi kichanga kuona kuwa haya ni matendo maovu katika jamii!

  Kama tumeweza kuwa na utaratibu wa kushughulikia kesi za uchaguzi ndani ya muda flani kwanini tushindwe kwenye kesi hizi za uhujumu uchumi?!. Chukua mfano wa Mkurugenzi ambaye amesimamishwa kazi na kupelekwa mahakamani kwa ubadhirifu, kesi ikiendelea kwa miaka sita , anaendelea kupokea mshahara, tunalipa mawakili wa serikali, mtuhumiwa ana dunda tu barabarani!! Ipo haja ya kuangalia upya mfumo wa kushughulikia kesi za namna hii!..

  Ziko taarifa za kesi za wakurugenzi wa wilaya ambao wako mahakamani toka mwaka 2004 maana yake ni zaidi ya miaka nane sasa wako mahakamani tu na kesi zinaendeshwa kwa muda wote huu. Ukiacha hasara kwa serikali na Taifa, ukiacha sura mbaya kwa kizazi kichanga/ kipya, hivi kwanini kesi hii ichukue miaka zaidi ya nane? Ushahidi gani unaosumbua kuhukumu?!! Mwisho wa siku anashinda kesi anaidai serikali.... Huu nao ni ufisadi mwingine.
   
 2. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #2
  Jun 13, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  mfumo uliopo ni wa CCM na serikali yake unaotetea watu wa tabaka tawala

  sasa badala ya kuja hapa kubwabwaja, ni bora ungerudi huko ndani mfanye kazi

  tumechoka na maneno maneno kama vile iko haja, nadhani, tunatathmini, tunatafakari, tumejipanga, tunaandaa nk...

  tatizo ni CCM, ingekua serikali nyingine kesi kama hiyo isingekaa 8 years

  jiulize mramba na yona wameishia wapi?
   
 3. w

  wikolo JF-Expert Member

  #3
  Jun 13, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 801
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mkuu Nape, hii ni namna nyingine tu ya kukiri kwamba serikali inayoongozwa na chama chako imeshindwa kazi na kwa maana hiyo chama chako cha CCM kimeshindwa kazi. Asante kwa kunifanya nilielewe hilo. Unachokifikiria ndicho kinavyotakiwa kuwa lakini wenye mamlaka ya kufanya hivyo wameshindwa.
   
 4. h

  hoyce JF-Expert Member

  #4
  Jun 13, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 1,119
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Hoja ya kupekeka kwenye vikao na kuiagiza serikali unaleta hapa? Tafakari. Chukua hatua.
   
 5. m

  muheta Member

  #5
  Jun 13, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi haya mawazo hujapewa na Makamanda mlipokutana juzi kwenye msiba wa Bob Makani?????
   
 6. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #6
  Jun 13, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Nape ndo maana unalaumiwa kwa kauli zako na kusema ukweli inabidi uwe makini.

  Ni nani aliamua kesi za uchaguzi ziishe baada ya miaka 2?mwenyekiti wako ana madaraka makubwa sana na wewe ndo mshauri wake katika chama.

  Sheria ya uhujumu uchumi ya mwaka 1981 iliishia wapi? Kwanini isitumike? Haya unayosema ndo yanaipatia credit CHADEMA fanya kazi badala ya kuwa mshauri upande mmoja na kuwa mtekelezaji upande mwingine.

  Hivi ukiwa mpinzani utafanya kazi gani? Kwasababu unafanya kazi ya kipinzani zaidi badala ya kufanya kama uliyepewa dola. Au anajaribu kufanyia mazoezi upinzani?
   
 7. BUBE

  BUBE JF-Expert Member

  #7
  Jun 13, 2012
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 844
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mkuu Nape, hapo umenena!

  Binafsi nadhani sio mfumo, bali kuna namna! Kuna tatizo lililoota mizizi kuhusu mali za umma, na pale inapomhusisha mwenye fedha. Ni mwaka juzi (I think) niliposikia bwana mmoja alikuwa Kigoma (r) kama DED alihukumiwa miaka kadhaa. But kesi yake ilikula miaka mingi na pengine yeye kilichomponza ni kutoroka, otherwise asingehukumiwa!

  Nilikuwa nafanya utafiti binafsi kuhusu kesi za umma na umuhimu wa serikali zote (kuu na serikali za mitaa) kuwaajiri wanasheria. Wakati mwingine nadhani hakuna sababu. Niulize kwa nini? Kati ya kesi 100 zenye kuhusu ulaji mkubwa wa mali za umma, serikali zote (kuu na za mitaa) huwa inaweza kushinda labda 2-5%. The rest serikali huwa inashindwa. WHY? MImi nadhani kuna conspiracy kati ya wahujumu na wenye kusimamia kesi (upande waserikali) na ndo maana huwa kesi za umma zinatupiliwa mbali, au serikali inashindwa. Sasa jiulize kuna haja gani ya kuwa na mwanasheria? Kuna baadhi ya maeneo wanasheria wa umma wanalalamikiwa kuwasaidia watoa huduma na makandarasi kuweka clauses kwenye mikataba inayoibana serikali mwisho wa siku kiasi kwamba hata kama aki-mess up nyinyi mnashindwa kumchukulia hatua.

  Kwa hiyo, ni vizuri kuwa na mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa Mahakama na kesi za Uhujumu uchumi, but ni vema pia wanasheria wetu wakapewa targets! Kama watu wa WB wanalipwa kulingana na contract kiasi gani za mikopo wamesaidia kusaini, kwa nini wanasheria wetu na mahakimu hawapewi idadi ya kesi za kushinda katika mwaka? Au idadi za kesi za kutolea uhukumu kila mwaka? Au wapelelezi waserikali/kesi idadi za kesi kupeleka mahakamani? Na wale wanaowasimamia wakapewa majukumu ya idadi ya wanasheria, mahakimu ambao wamefanyiwa assessment na kupewa reward (positive or negative) based on their performances?
   
 8. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #8
  Jun 13, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Nape kwa nini hili usilipeleke kwenye vikao vya chama mkajadili na kuchukua hatu, si ninyi ndio mna polisi wanaofanya uchunguzi na mahakama zinazohukumu! Huku kulalama kuishe, tafadhali sana, chukueni hatua. Najua na wewe unajua kesi hizi zinachelewa kwa sababu ya kulindana.

  Tunachotaka kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kwa sasa kutoka kwa viongozi, wewe ukiwa mmoja wapo, ni hatua gani mmezichukua kwenye kadhia mbalimbali zinazoikabili nchi, sio kuja huku kutoa malalamiko ambayo tumeyachoka.
   
 9. D

  Dabudee Senior Member

  #9
  Jun 13, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 156
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Ni utaratibu mahsusi wa kulindana ulioasisiwa na kulelewa na kulindwa kwa ustadi mkubwa na CCM.

  Mwalimu aliyekula karo miaka 300 lakini deep green finance, meremeta, kagoda etc, hao wanaambiwa warudishe kisanii-sanii.Hayo maneno uliyosema ni ya hekaya za abunuwas ya" mwalimu usinibaini, wajinga ndiyo waliwao: nikipata mbili moja yako moja yangu" na unategemea tuitikie amina.

  Tunadhani imetosha, iwekwe serikali iliyo serious siyo hawa wachumia tumbo.
   
 10. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #10
  Jun 13, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,494
  Likes Received: 5,604
  Trophy Points: 280
  Nimefurahi kuona haya yanasemwa na wewe! Ningefurahi kama magazeti yangeweka kauli hii front page kwa msisitizo. Unachosema ni kweli na hili ni tone la matatizo lukuki tena ya msingi kabisa kwa nchi hii iliyoongozwa na CCM kwa nusu karne!

  Umeshapeleka hili kwenye vikao vya chama ikibidi bunge hili linalokaa sasa lichukue hatua? mnao wabunge wengi sana ambao wakikubali kukuunga mkono mnaweza kufanya mabadiliko hata sasa.

  Tukienda kwa hoja namna hii tutaijenga nchi yetu na si propaganda za kisiasa.wakati wenzetu wanapambana na propaganda za kiuchumi sisi hasa CCM wanahangaika na propaganda za kisiasa tena za kujilinda bila kujali maslahi ya taifa.
   
 11. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #11
  Jun 13, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  pale jangwani badala ya kusema hili ukaishia kuita watu majambazi(uamsho) uliitaka serikali iwashughulikie na hili ungelisema siku hiyo
   
 12. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #12
  Jun 13, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Nafurahi sana JF kuwa ndio dira yako, Hoja hii tulishaijadili sana aliianzisha mwanakijiji, Mods iweke tena hapa hiyo thread ili tumfundishe Nepi aache kuwa analopokalopoka ovyo, ajifunze... Uzi huu aniuanzisha MMJ, JF ndio darasa karibu.
   
 13. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #13
  Jun 13, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  We Nape kwani huji tatizo lipo wapi? Je mahaka zinapata bajeti gani? Hilo ni swali la kwanza.

  La pili ni je hao mafisadi waliiba peke yao? Unajua wanaowalinda ni hao unaoshirikiana nao. Zaidi sana ni viongozi wa nyinyiemu. Hao ndiyo wanaowakingia kifua. Hata ukiwekwa mfumo fulani, unaweza usisaidie kwani wakati wa kufanya utafiti ni vigumu sana vigogo waliopo serikalini kutoa ushirikiano kwenye upelelezi.

  Chama lenu limezungukwa na walafi wa ajabu. Hawana aibu, hata maadili hawana. Hivi unakaaje na Chenge kwa mfono. Imewezekanaje Chenge mkamchagua kuwa kiongozi wa kamati ya fedha? Nape acha kutukejeili hapa. Fanya kazi acha kuanika sura!
   
 14. H

  Hute JF-Expert Member

  #14
  Jun 13, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 6,053
  Likes Received: 3,920
  Trophy Points: 280
  NAPE, hakuna mtu anayependa kuchelewesha kesi kwa makusudi, unachotakiwa kuelewa ni kwamba, haki inayoharakishwa inaweza kuwa haki inayoleta madhara kwa upande mwingine.

  Wewe unaongelea upande wako kama mwananchi au ukiwakilisha selikali ya tz, ule upande wa mshitakiwa naye ana ya kwake na ukiharakisha kesi bila msingi, kwanza kabisa unaweza kumdhurumu haki, pia unaweza kuwa umepoteza muda kwasababu unaweza kuta umeweka mianya ya yeye kukata rufaa mahakama ya juu na kuachiwa kabisa, hivyo mbio zote za nyuma unakuwa ulikuwa unapoteza muda na pesa etc.cha muhimu ni kwamba, hata kama inachukua muda kiasi gani, lazima jambo lifanyike kwa umakini wa kutosha ili kuondoa mianya yote ya mshitakiwa ambaye kweli ameiba, kuponyoka.

  Kwa wale wanasheria wanajua hili. Jambo jingine ni kwamba, kitu kinachoitwa kesi ni kigumu sana, na kinahitaji ushirikiano si wa wale wanaoappear mahakamani tu, bali wa wananchi wooote tz, kwasababu pale mawakili wa serikali wanapopambana kumshitaki mtu, kuna watu wengine humo humo kwenye serikali wanapambana kupoteza ushahidi au kupoteza maisha ya wale mawakili wa serikali ambao wanalipwa kwam mwezi hata milioni moja haifiki...wanarisk maisha yao kwenye mikesi hiyo kwa mshahara kidogo sana hivyo ni rahisi yeye kuthamini maisha yake kwanza au hata kujoin mshitakiwa kama atakuta kuna maslahi, hivyo labda serikali ingewajali hawa jamaa, na kuweka pesa nyingi zaidi kwenye vitengo vya upelelezi mfano ile task force etc ingesaidia.

  Polisi ni watu wa ajabu sana, hapa tz hakuna polisi hata mmoja unayetakiwa kumwamini, polisi wapelelezi wanaharibu kesi ajabu, na hawa ndio wanaosababisha hata mawakili wa serikali kupoteza kesi kwasababu wao ndio wanaokamata washitakiwa na kukusanya ushahidi etc. Hakuna kitengo kibaya kama cha polisi kwa rushwa, anaweza akakusanya ushaidi na akaweka mianya ya mshitakiwa kuja kupata nafuu wakati wa prosecution baada ya kupewa kidogo pesa, hivyo utakuta, kuna matatizo sana kwenye prosecution ya kesi si hizi za uchaguzi tu, bali hata zile zingine zote, kwanza, mawakili wa serikali rushwa si sana mfano: pale kwa dpp ambapo mimi nilishafanya kazi, akikugundua tu kuwa unatuhumiwa au una mazingira ya kula rushwa, hakucheleweshi kabisa, hivyo utakuta kesi inaanza kuharibiwa kwa wapelelezi, inakuja kuharibiwa na hakimu na pengine wakili wa serikali ambaye ana maslahi machache hivyo anaogopa kujilipua kupigania kesi hiyo ashinde kwasababu huwezi kurisk maisha yako kwa maslahi madogo...kuna kesi zingine kama hizo za mafisadi wa CCM Rajab Marando etc, nguo zao zilikuwa zinafuliwa kibondo kabla ya kuingia court, hivyo kuna intimidation nyingi, kwa kifupi mawakili wa serikali ambao wanasimama na kuonekana wabaya mbele wananchi, wako ktk mazingira magumu......ukifika court wao ndo wanaonekana wabaya kwasababu wanamshitaki accused kwa nguvu zote utafikiri selikali ndo baba yao.

  HATA WAPELELEZI WA PCCB wanakula rushwa sana, yaani pccb wanakula rushwa sawa tu na polisi wapelelezi....tz imeoza sana ndugu yangu. ukiona kesi imechelewa, ujue kuna sababu kama hizo, pia kesi za uchaguzi kama umefuatilia zinagarimu pesa nyingi sana, sasa sijui nchi yetu ina pesa kiasi gani kushugulikia kila kesi ambazo zipo za ufisadi kila wilaya, pesa hazipo...hii ya uchaguzi tu ilichukuliwa kama first priority, lakini zingine mnasema hamna pesa...achieni madaraka kwa chadema muone kama mambo hayatabadilika.
   
 15. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #15
  Jun 13, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mkuu Nape,

  Kikweli haya ni mawazo mazuri nami nakubaliana na wewe kuwa hoja yako ina mashiko sana. Hata hivyo, kwa kuwa Chama chako ndicho kinachoshika hatamu ya uongozi na kuiagiza serikali kama nilivyokusikia mara nyingi. Napendekeza uanzishe hoja hiyo kupitia vikao vyenu ili iletwe kama hoja binafsi bungeni na wabunge wa ccm. Na mkifanya hivyo, pengine ccm itakuwa imeongeza heshima yake mbele ya jamii.

  Nimesema hivyo kwa sababu, maneno uliyosema yanapaswa kusemwa na vyama vya upinzani lakini mtu mwenye nafasi kubwa kutoka chama chenye wabunge wengi kama wewe una kazi mmoja tu, kufanya maamuzi na kutekeleza. Serikali unayo na Bunge unayo, kwa nini uandike mate?
   
 16. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #16
  Jun 13, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,999
  Likes Received: 2,655
  Trophy Points: 280
  Nape katika siku zote leo umeongea point nzuri sana, ila umekosea ni kwa nini usingemwambia mkuu wa kaya?

  Kwasababu yeye ndio mwenye mamlaka hayo, kama alivyoagiza kwenye kesi ya Lema mshauri afanye hivyo na kwenye kesi za mafisadi.
   
 17. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #17
  Jun 13, 2012
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,653
  Trophy Points: 280
  Kaka muweke MWEKEZAJI wa kuendesha hizi KESI, Kwani hata TAKUKURU wameshindwa kazi.
   
 18. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #18
  Jun 13, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  mpendwa,

  kwa nini unaongea kama kada wa "upinzani"??? viongozi wa ccm lazima mjifunze na kuamini kuwa ccm ndicho chama tawala na hivyo hata maneno yenu yapaswa kueleza ni nini mmefanya kumaliza tatizo fulani, sio kila mara mnaelezea matatizo utadhani nanyi ni wapinzani na hamjawahi kushinda kuunda serikali hata mara moja!

  kwa kweli mienendo kama hii haikisaidii chama cha ccm.

  ubarikiwe sana

  Glory to God!
   
 19. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #19
  Jun 13, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  badilini mfumo wa utawala wote muone kama hizi kesi zitakua zinachukua muda mwingi hivi..serikali imekua inafanya haya makusudi..mfano kuna kesi ya wafanyakazi wa mutex pale musoma wananchi wanadai malipo yao dhidi ya muajiri wao(serikali ya ccm) wameenda mahakamani na wameshinda kesi tangu miaka ya 2004 lakini mpaka leo serikali inakata rufaa na dana dana zinapigwa mpaka nashangaa

  SIJUI UNAONGEA NINI HAPA AU UNALOLIZUNGUMZA HULIJUI??
   
 20. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #20
  Jun 13, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Naona Vua Gamba Vaa Gwanda na Uzalendo vimekukaa mkuu Nape. Leo umenena!
   
Loading...