Kijana Msomali
Member
- May 10, 2012
- 92
- 71
Iko haja ya kuangalia upya mfumo wa mahakama zetu! Kesi za utumiaji mbaya wa madaraka, rushwa, ufisadi na uhujumu uchumi zisichukue muda mrefu bila kutolewa maamuzi. Kwanza ni hasara kwa serikali na nchi na haitoi mafunzo kwa kizazi kichanga kuona kuwa haya ni matendo maovu katika jamii!
Kama tumeweza kuwa na utaratibu wa kushughulikia kesi za uchaguzi ndani ya muda flani kwanini tushindwe kwenye kesi hizi za uhujumu uchumi?!. Chukua mfano wa Mkurugenzi ambaye amesimamishwa kazi na kupelekwa mahakamani kwa ubadhirifu, kesi ikiendelea kwa miaka sita , anaendelea kupokea mshahara, tunalipa mawakili wa serikali, mtuhumiwa ana dunda tu barabarani!! Ipo haja ya kuangalia upya mfumo wa kushughulikia kesi za namna hii!..
Ziko taarifa za kesi za wakurugenzi wa wilaya ambao wako mahakamani toka mwaka 2004 maana yake ni zaidi ya miaka nane sasa wako mahakamani tu na kesi zinaendeshwa kwa muda wote huu. Ukiacha hasara kwa serikali na Taifa, ukiacha sura mbaya kwa kizazi kichanga/ kipya, hivi kwanini kesi hii ichukue miaka zaidi ya nane? Ushahidi gani unaosumbua kuhukumu?!! Mwisho wa siku anashinda kesi anaidai serikali.... Huu nao ni ufisadi mwingine.