Mahakama Kuu yazuia uharibifu wa vifaa vya uchaguzi katika maombi yaliyofunguliwa na wagombea 17 wa ACT Wazalendo majimbo ya Unguja

Mahakama Kuu yazuia uharibifu wa vifaa vya uchaguzi katika maombi yaliyofunguliwa na wagombea 17 wa ACT Wazalendo majimbo ya Unguja

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,437
Reaction score
5,234
Mahakama Kuu ya Zanzibar, Masjala ya Tunguu, mbele ya Mheshimiwa Jaji Salma Hassan, leo imetoa Amri ya Muda ya Kusitisha Kitendo (Status Quo) katika Maombi Madogo ya Madai Na. 18 ya Mwaka 2026.

Amri hiyo imesimamisha rasmi mpango wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) wa kuharibu vifaa na nyaraka za uchaguzi.

Chimbuko la Shauri


Waombaji, ambao ni wadai katika Mashauri ya Uchaguzi Na. 2, 3, 4, 5, 6, 7, 8, 9, 10, 11, 12, 13, 14, 15, 16, 17 na 18 ya Mwaka 2025, waliwasilisha maombi hayo chini ya Hati ya Dharura.


Hatua hiyo imekuja kufuatia tangazo la ZEC kwa umma likielezea nia ya kuteketeza nyaraka zote za uchaguzi wa mwaka 2025.

Uamuzi wa Mahakama


Akizingatia uzito wa suala hilo na uwezekano wa kutokea kwa madhara yasiyoweza kurekebishika katika mchakato wa utoaji haki, Mheshimiwa Jaji ameamuru kudumishwa hali ya sasa (Status Quo).

Mahakama imeelekeza kuwa nyaraka zote za uchaguzi zibaki kama zilivyo hadi pale maombi hayo yatakaposikilizwa kwa pande zote mbili (inter partes).

Kusoma zaidi
 

Attachments

Sinema Hizo. Tanzania mahakama ipo mfukoni.
 
Hawa jamaa (INEC & ZEC) ni wahuni waliopitiliza...

Yaani Uchaguzi umefanyika karibu miezi mi3 tu iliyopita halafu wao wanataka kuharibu nyaraka zenye kumbukumbu za uchaguzi huo halafu wakati huohuo wakitambua kuwa Kuna watu wameenda mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi huo? Wanaogopa nini kwani kiasi cha kutaka kuharibu ushahidi?

Na wanajua fika kabisa kuwa kesi cha uchaguzi hupaswa kumalizika katika kipindi cha miezi 6 hadi 12..

Wanapaswa kutunza nyaraka hizo mpaka baada ya miezi 12 na pale kesi zote zitakapokuwa zimeisha...

Huku Tanganyika kama ikitokea wagombea walioshindwa wakafungua kesi kupinga matokeo halafu wasimamizi wakatakiwq kuleta ushahidi wa kuthibitisha ushindi wa washindi waliowatangaza, aisee ni madudu matupu, hakuna ushahidi wa nyaraka...!

Washindi wote kuanzia diwani, mbunge na Rais walitangazwa tu bila uwepo wa uthibitisho wa kura zilizopigwa maana hazipo, watu hawakupiga kura. Watangaza matokeo walikuwa wanajitangazia takwimu za kubumba kichwani tu...

Kwa ufupi ni kuwa, Oktoba 29, 2025 hakukuwa na uchaguzi bali kulikuwa na uchafu na mauaji ya watu tu...!!
 
Back
Top Bottom