Mahakama Kuu yasitisha bomoabomoa Nyumba za Bonde la Mto Msimbazi

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,485

Waliobomolewa Msimbazi waruhusiwa kufungua kesi ya msingi ndani ya siku 60. Baada ya hapo serikali inaweza kuendelea na zoezi hilo.
Mahakama-KUU.jpg

Mahakama Kuu

Mahakama hiyo imeagiza zoezi la bomoabomoa kusitishwa kwa nyumba zilizoko eneo la bonde la mto Msimbazi Dar, na wamiliki wa nyumba hizo wamepewa siku 60 za kufungua kesi ya msingi Mahakamani kuhusu bomoabomoa hiyo.
 
Leo maeneo ya kiwalani imefanyika bomoa bomoa kwa nyumba zilizo karibu na barabara.
 
hili suala si limalizwe...wakati mwingine sheria nazo zinazingua...watu wanaishi 'mtoni' wakikumbwa na mafuriko wanarudi kuilalamikia serikali
 
This is just a stay of execution!

Kama wana hekima na busara ni vizuri wakaanza kuangalia maeneo mengine ya kuishi!

Hii ni sawa na mtu ambaye amehukumiwa kunyongwa na anasubiri tu siku yoyote ya kunyongwa!

Mwisho wa siku, nyumba zitabomolewa!

This is painful truths coupled with ignorance of law excuses no one!
 
Waliobomolewa Msimbazi waruhusiwa kufungua kesi ya msingi ndani ya siku 60. Baada ya hapo serikali inaweza kuendelea na zoezi hilo.
Mahakama-KUU.jpg

Mahakama Kuu

Mahakama hiyo imeagiza zoezi la bomoabomoa kusitishwa kwa nyumba zilizoko eneo la bonde la mto Msimbazi Dar, na wamiliki wa nyumba hizo wamepewa siku 60 za kufungua kesi ya msingi Mahakamani kuhusu bomoabomoa hiyo.
Naamini sana Mahakama za Tanzania ila sioni hoja za msingi zitakazoridhisha Mahakama ikawaruhusu kubaki mabondeni!!
 
hili suala si limalizwe...wakati mwingine sheria nazo zinazingua...watu wanaishi 'mtoni' wakikubwa na mafuriko wanarudi kuilalamikia serikali
Serikali inaonewa sana, na yote hayo ni kwa sababu ya ubinafsi wa baadhi ya wanasiasa. Na hizi siasa ndizo zinazolikwamisha bara zima la Afrika.
 
This is just a stay of execution!

Kama wana hekima na busara ni vizuri wakaanza kuangalia maeneo mengine ya kuishi!

Hii ni sawa na mtu ambaye amehukumiwa kunyongwa na anasubiri tu siku yoyote ya kunyongwa!

Mwisho wa siku, nyumba zitabomolewa!

This is painful truths!
Watanzania tunapenda kuahirisha matatizo. Mwishowe bomoabomoa Itachukua nafasi yake. Wakati, ni vyema wangeomba wapatiwe maeneo ya kujenga
 
Na ikitokea mafuriko waende wakapate hifadhi kwenye hiyo mahakama siyo waanze kusumbua kamati ya ulinzi na usalama.
 
Hapa tunapoteza muda. Bomoa bomoa iendelee. Serikali iwapatie sehemu mbadala na iwe marufuku narudia marufuku watu kurudi kwenye maeneo yaliyo bomolewa.
 
Bomoabomoa ilianza mwisho wa mwaka 2015 kwenye maeneo mbalimbali ambayo yalitajwa kwamba ni mabondeni, maeneo ya wazi na mengine ambayo kisheria hayakutakiwa kuwa na makazi ya watu.

Zoezi lilisimama kwa muda, baadae zikaanza kupitishwa alama za ‘X’ kwa maeneo ambayo bomoabomoa ingefatia, wapo waliofikisha kesi Mahakamani kupinga zoezi hilo Mahakama Kuu kitengo cha ardhi Dar es Salaam.
Mahakama hiyo imeagiza zoezi la bomoabomoa kusitishwa kwa nyumba zilizoko eneo la bonde la mto Msimbazi Dar, na wamiliki wa nyumba hizo wamepewa siku 60 za kufungua kesi ya msingi Mahakamani kuhusu ishu ya bomoabomoa.
 
Watanzania tunapenda kuahirisha matatizo. Mwishowe bomoabomoa Itachukua nafasi yake. Wakati, ni vyema wangeomba wapatiwe maeneo ya kujenga
Bahati mbaya Rais wetu hana kawaida ya kuingilia matakwa ya sheria, Watanzania tujifunze kuishi kwa kufuata sheria.
 
Waliobomolewa Msimbazi waruhusiwa kufungua kesi ya msingi ndani ya siku 60. Baada ya hapo serikali inaweza kuendelea na zoezi hilo.
Mahakama-KUU.jpg

Mahakama Kuu

Mahakama hiyo imeagiza zoezi la bomoabomoa kusitishwa kwa nyumba zilizoko eneo la bonde la mto Msimbazi Dar, na wamiliki wa nyumba hizo wamepewa siku 60 za kufungua kesi ya msingi Mahakamani kuhusu bomoabomoa hiyo.
Hilo ni pigo jingine kwa wala viwavi
 
Back
Top Bottom