Mahakama kuu ya Uganda yatoa amri kaburi la Ivan lifukuliwe

Ekyoma

JF-Expert Member
Dec 30, 2015
2,177
2,803
Hatimaye Mahakama Kuu ya Uganda yatoa amri kaburi la Ivan Ssemwanga, yule mtalaka wa Zari, ambaye ni mke wa sasa Diakond Platinumz lifukuliwe, ili mamilioni ya pesa alizozikwa nazo zitolewe.

Mahakama imesema imechukua uamuzi huo ili kulinda heshima ya fedha ya nchi hiyo.

Mahakama imechukua uamuzi huo baada ya Mganda mmoja aitwaye Mgugu Abey, kuwashtaki Mahakamani kampuni iliyoraribu mazishi hayo ya A Plus Funeral Management na Benki Kuu ya Uganda,ambayo imeonekana ilizembea kwenye tukio hilo.

Hivyo, mahakama imeamuru kampuni ivunje kaburi kwa gharama zao,ili mlalamikaji achukue pesa hizo kwa niaba ya mataifa yenye fedha hizo, kwani zilikuwepo Rand za Afrika Kusini,Dola za Marekani pamoja na Shilingi za Uganda.

Kisha kampuni ya A Plus imeamriwa ilifukie kaburi hilo kwa gharama zake na kisha kumlipa ndugu Abey gharama zingine za usumbufu.Nakala ya huku inaletwa
Ama kweli mjini shule.
 
wazielekeze kujenga miundo mbinu au kituo cha afya.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Watanzania mmezidi udaku hata kuelewa hamuelewi.

Wapi mmeona mahakama imeamua hilo? Au hamjaelewa kwa sababu mmefikia conclusions zenu haoooo mnadakia.

Tena ni watu wawili ambao ni raia wa kawaida...
hata mmoja alikuwepo msibani navyojua ndio kaenda leo kufile hiyo lawsuit.

Mnatutia aibu wenzenu, napenda kuandika humu kuwa muwe na subira. Hata hiyo doc haina hukumu...

Mnasikitisha nyie wapenda udaku wote wakitanzania.
 
Hawa limbukeni hawaelewi kwamba hela si zako, ni za serikali, inakuazima tu utumie.

Na kuna mipaka ya kutumia hela, kwa maana hela ni katika alama na nyara za serikali ya nchi.

Ndiyo maana ukichoma moto hela "zako mwenyewe" au kuzizika, unashitakiwa.

Umeidharau nchi na umeharibu mzunguko wa fedha, kimsingi umehujumu uchumi wa nchi.

Unaweza kuwa na hela nyingi sana halafu bado ukawa mshamba na vitu hivi huvielewi.
 
IMG-20170602-WA0055.jpeg
 
Kwa kweli wabongo wamezidi umbea. Hiyo ndo amri ya kufukua kaburi?
Jamani kama Kitu hukijui ni vizuri tu ukatulia na kusubiri kukomenti thread za wengine, sio lazima na wewe uwe na ya kwako.
Hizi ni baadhi tu ya threads zinazoishushia hadhi na kuichafua JF, kama vp lipekwe kwenye jukwaa la udaku na utani
 
Mleta mada kakurupuka pale alipoona mhuri wa mahakama kuu. Kwa kutokuwa na uelewa na mambo ya kisheria akashindwa kujua hiyo ni application, akakimbilia kutafsiri maandishi! Mleta mada hiyo ni application siyo judgement.
 
Back
Top Bottom