Elections 2010 Mahakama kuu inashinikizwa kuridhia malipo ya dowans

Byendangwero

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
871
56
Kauli ambazo zimekuwa zikitolewa na baadhi ya viongozi wa ngazi za juu serikalini, zenye kuashiria kwamba serikali ilikuwa tayari kuilipa Dawans, zimetafsiriwa na wadadisi wengi wa habari kuwa zina lengo la kuishinikiza mahakama kuu kuridhia malipo hayo. Kuna ukweli wowote juu ya tafsiri hii?
 
Mbona inawezekana washalipa? ile kauli ya Mura kuwa mjadala wa Dowans umefungwa unabeba uzito mkubwa
 
Lakini jamani tusitoe conclusion tusubiri kwanza tuone maana tanesco kuongeza bei si bure
 
Tz ni mwanachama wa mahakama iliyotoa hukumu, hivyo hamna ujanja hela zitalipwa tu, kinachofanyika hapa ni kiini macho tu. Nchi tunaliwa kilasilimali mchana mchana na tunawachekea viongozi wetu wakati wanafilisi nchi
 
Kumbe serikali haijachukua uamuzi wowote katika suala hili; viongozi waandamizi serikalini waliotoa kauli juu yasuala hili inaonekana walikuwa wanajaribu kulinda maslahi ya Dowans kwa kutumia mgongo wa serikali. Tunashukuru, kutokana na kauli za Sita na Mkullo njama zao zimebainika.
 
Kauli ambazo zimekuwa zikitolewa na baadhi ya viongozi wa ngazi za juu serikalini, zenye kuashiria kwamba serikali ilikuwa tayari kuilipa Dawans, zimetafsiriwa na wadadisi wengi wa habari kuwa zina lengo la kuishinikiza mahakama kuu kuridhia malipo hayo. Kuna ukweli wowote juu ya tafsiri hii?
byandegwaro, hakuna ukweli wowote kuhusu hili. Uamuzi wa ICC ni wa mwisho. Kazi ya Mahakama Kuu sio kujadili wala kuridhia as if ina mamlaka ya kuamua chochote. Kazi ya Mahakama Kuu ni kuisajili tuu hukumu ile kwa ajili ya utekelezaji, nothing more, nothing less. Mkataba ndio umeipa ICC mamlaka ya mwisho.
 
Uhuru wetu hauwezi kuwa uhuru kama tunaweza
kutawaliwa kupitia mikataba ya kina curll-max,
ingekuwa na maana kama hiyo dowans ingekuwepo
kwenye hilo taifa la asili ya biashara yake,
kwa kuwa hakuna dowans hakuna taifa
litakalojaribu kutaka sheria kukaziwa.
'tuliridhia mkataba' ambao ni siri kama ilivyo
mikataba mingine, watanzania haturidhii kodi zetu zitumike kuwalipa wahuni wa kimataifa.
 
Mimi bado naamini kwa kiasi kikubwa Mahakama kuu ya hapa Tanzania bado ipo huru!haki itatendeka!!
 
Kulipa ni lazima hiyo hamna mjadala,nadhani wote tunajua maana ya kuvunja mkataba.Tunachotakiwa kama nchi turudi kinyumenyume wale wote waliotuingiza kwenye kadhia hii tuthubutu kuwachukulia hatua za kinidhamu bila kujali hadhi ya mtu.Uchunguzi wa kina ufanywe mpaka kating zile zitajwe.
 
Uhuru wetu hauwezi kuwa uhuru kama tunaweza
kutawaliwa kupitia mikataba ya kina curll-max,
ingekuwa na maana kama hiyo dowans ingekuwepo
kwenye hilo taifa la asili ya biashara yake,
kwa kuwa hakuna dowans hakuna taifa
litakalojaribu kutaka sheria kukaziwa.
'tuliridhia mkataba' ambao ni siri kama ilivyo
mikataba mingine, watanzania haturidhii kodi zetu zitumike kuwalipa wahuni wa kimataifa.

Mkuu huyo ni Max yupi?
 
Kama ni kweli kuna haja kufanya mabadiliko ya katiba kwa haraka ili kuepusha kuingiliana kwa miili mikuu ya utawala.
 
tushalipwa tunakusanya hela za kampen 2015. Nyie pigen kelele msubiri kuchangishana na misaada ya sabodo mili 100. Achen tunataka maendeleo wabunge
 
that is just a simple arithmetic i.e 1 + 1 = 2!
You dont need to ask, it is obvious, dont u see? These people(viongozi wababaishaji) are :sick::sick::sick: minded!!!
 
Tz ni mwanachama wa mahakama iliyotoa hukumu, hivyo hamna ujanja hela zitalipwa tu, kinachofanyika hapa ni kiini macho tu. Nchi tunaliwa kilasilimali mchana mchana na tunawachekea viongozi wetu wakati wanafilisi nchi

Itakuwa ni muujiza kama tutajinasua kwenye mtego huu maana swali la msingi ni kuwa mkataba umevunjwa au la? kinachofanyika sasa ni kujaribu kujifanya kuwa juhudi zinafanyika ili kujinasua, wakati inaeleweka wazi kuwa kuna makosa ya kisheria yamefanyika ambayo hatuna nguvu kisheria kuyakana. Kinachofanyika sasa ni kujaribu kupoteza muda ili ile bilioni 94 iongezeke wajanja waneemeke.
 
Serikali ya Kikwete iko kama imekaliwa kooni. Wapo wafadhili ambao hawako tayari kuachilia misaada yao ianze kutumika mpaka maswala kadhaa yawe yamepatiwa ufumbuzi. Kama Dowans watalipwa basi inabidi waliohusika wachukuliwe hatua za kueleweka kwa Taifa zima. Kinyume chake itakuwa ni yale yale ya mtu kusemekana kafariki nchi za nje kama Balali. Na hiyo itaeleweka kuwa ni Kagoda nyingine imetengenezwa kwa ajili ya uchaguzi wa 2015. Hakika nchi itaingia kwenye machafuko, CCM inatakiwa sasa iwe na aibu nchi haiwezi kuwa inaendeshwa na magaidi wa kimataifa. Huwezi ingia mkataba na Kampuni isiyoeleweka wala isiyosajiliwa popote. Mwanasheria Mkuu anashangaza dunia anaposhindwa kulieleza Taifa taratibu za kusajili Kampuni inayowekeza nchini, je Mtu anaingia tu na kupewa eneo na kuanza kuajiri na kufanya chochote?? Hata kuingia choo cha stendi au sokoni unalipia kwanza. Ajabu gani hii Tanzania yetu tunajidhalilisha mbele ya uso wa Dunia nzima!! Huyo mtu mwenye hii Kampuni ananguvu gani za kiasi cha kutisha namna hiyo?.
Ama kwa hakika jamnbo hili linatia uchungu. Hili jambo linahitaji maadamano ya nchi nzima. Hawa watu wametishia nini haswa, kutoa watu roho? au kupindua hii nchi? Jiulize kama utapata jibu!
 
Bado ushahidi uliopo unaashiria kwamba serikali ingilipenda mahakama itupilie mbali pingamizi lililowekwa na wanaharakati kupinga malipo haya; hii inadhihirishwa na ukweli kwamba pamoja na rais kutoa kauli kuwa hasingelipenda serikali yake ilipe malipo hayo, mpaka sasa TANESCO na Mwanasheria mkuu wa serikali hawajafungua kesi yeyote kupinga malipo hayo.
 
Back
Top Bottom