Mahakama kuu yawadhulumu wajasilia Mali wa Matofali yaliyotumika kujenga mahakama za wilaya

Vmatongo

Senior Member
Dec 8, 2021
156
237
Mahakama kuu chini ya mtendaji mkuu wa Mahakama bwana Olisante Ole Gabrieli zaidi ya Mwaka sasa ameshindwa kuwalipa wajasilia Mali ambao wamewauzia matofali zaidi ya elfu arobaini ambayo yametumika kujenga mahakama za wilaya katika mkoa wa kigoma wilaya za Uvinza na Buhigwe pia katika mkoa wa Tabora kwenye wilaya ya kaliwa.

Matofali hayo tayari yameshatumika kujenga mahakama hizo ambazo nimezitaja hapo juu, cha kushangaza mara baada ya mahakama hizo kukamilika malipo ya matofali hayo sasa imekuwa ni mtihani kwa wajasiliamali hao Ambao ni Musa Mohamed Salum mkazi wa Uvinza.

Mjasilia mali huyu amekuwa akizungushwa malipo yake zaidi ya mwaka sasa bila mafanikio yeyote. Mahakama ni chombo cha haki ambacho hatutegemei kuendelea kumzungusha mjasiliamali huyu ambaye sasa anakaribia kupelekwa huko huko mahakamani ambako amezulumiwa na watu wanaomdai, kwa sababu hata yeye huyu mjasiliamali alikopeshwa na anadaiwa.

Tunaomba Mahakama hii itende haki na imlipe haraka huyu Bwana Musa mohamedi salum pesa zake.

Tunaposema watu wafanye kazi kwa bidii na wazalishe tunahitaji wajasiliamali wa namna hii ambao wanatakiwa kuungwa mkono,

Ni imani yetu kwamba Mh. Rais anapenda vijana wa namna hii ambao wanafanya kazi kwa bidii.

Tunaomba mamlaka ya Rais iingilie kati suala hili na kusaidia mjasiliamali huyu apewe malipo yake.

Namba za mjasiliamali huyu ni,
0784675844
0767675844
0622675844
0715675844
 
Back
Top Bottom