Mahakama Kuu Dodoma: Joshua Nassari ashindwa kesi yake ya kuvuliwa ubunge

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,131
931
Taarifa za hivi punde kutoka Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma ni kuwa, Joshua Nassari ameshindwa katika Shauri alilofungua Dhidi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya kupinga kuvuliwa Ubunge.

Kesi hiyo ambayo uamuzi wake umetolewa leo katika hatua ya mapingamizi yaliyowasilishwa na upande wa Serikali kupitia Wakili Mkuu wa Serikali imefikia mwisho katika hatua ya Mapingamizi.

Mahakama imefuta kesi hiyo na hivyo, Nassari sio Mbunge tena.

-------
Jaji Mansour ametumia dakika 44 kusoma maelezo yaliyomweka katika wakati mgumu Nassari.

Machi 14, 2019 Ndugai aliiandikia Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) barua akiieleza kuwa Nassari amepoteza sifa ya kuwa mbunge baada ya kutohudhuria mikutano mitatu mfululizo bila kutoa taarifa.

Spika Ndugai aliitaja mikutano hiyo kuwa ni wa 12 ulioanza Septemba 4 hadi 14; Novemba 6 hadi 16, 2018 na wa Januari 29 hadi 9.

Baada ya uamuzi huo, mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema amemuagiza Nassari kuzungumza na wananchi na wanachama wa jimbo lake kuwaeleza kilichotokea.

Akisoma uamuzi wake leo Ijumaa Machi 29, 2019 Jaji huyo ametumia kifungu cha 5 (4) kuwa Nassari alipaswa kupeleka malalamiko yake kwa Katibu wa bunge wala si kama alivyofanya.

Kifungu kingine kilichombana Nassari ni cha kanuni ya 146 (2) kwamba alijifukuzisha mwenyewe kwa kutohudhuria vikao vitatu mfululizo vya Bunge bila taarifa.

Mawakili wa Serikali, Alesia Mbuya, Masunga Kamuhanda na Pius Mboya walipangua hoja za wakili wa utetezi, Fred Kalonga aliyekuwa akipinga kuwa mbunge huyo alifukuzwa bila utaratibu hivyo kuitaka Tume ya Uchaguzi (NEC) isitangaze jimbo kuwa wazi.

Nje ya Mahakama Nassari amesema hakuna dhahabu nzuri isiyopita kwenye moto na kubainisha kuwa alishakoswa risasi iliyompiga mbwa wake, alinusurika ajali ya ndege na kwamba hili la ubunge halimtishi

Chanzo: Mwananchi
 
Kwani bunge si lilimsamehe?
Tuyafuate ya nani mahakama au bunge
 
Huyu Dogo mda c mrefu tutamuona amevaa nguo za rangi ya ukoka
1553845092351.png
 
Back
Top Bottom