Mahakama imewaachia huru Gugai na wenzake

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
4,162
2,000
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru aliyekuwa mhasibu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Godfrey Gugai na wenzake wawili baada ya mahakama hiyo kushindwa kuthibitisha mashtaka yaliyokuwa yakiwakabili.

Gugai na wenzake walikuwa wanakabiliwa na makosa 40, makosa 19 kati ya hayo ni kughushi, 20 ni utakatishaji fedha na moja ni kumiliki mali zilizozidi kipato halali.

Gugai alikuwa anakabiliwa na kosa la kumiliki mali kinyume na kipato chake, ambapo anadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Januari 2005 na Desemba 2015.

Mwananchi
 

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
5,294
2,000
Warudisheni kazini na muwalipe fedha zao kwa muda wote wakiwa segerea. Na wakaendeleze miradi waliyokuwa wanamiliki inayoxidi kipato chao. Utawala huu tutaona na kusikia mengi. Muhimu ccm watoe fomu nyingi kwa wanaotaka kugombea uRais 2025
 

Sukumagang

JF-Expert Member
Jul 4, 2008
20,125
2,000
Awamu ya sita hii,wote wanatoka na wanafungua kesi ya kuidai serikali. Kodi za watanzania zitalipa fidia za watu kibao.
 

funzadume

JF-Expert Member
Jan 28, 2010
12,421
2,000
Huyu jamaa namfahamu. Niliwahi kumtembea Keko. Mungu ni mwema ametolewa aliingia ndichi toka 2017 mwishoni
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom