Mahakama: BAKWATA si Chombo cha Waislam wote

Mahakama: BAKWATA si Chombo cha Waislam wote

ngara23

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2019
Posts
15,774
Reaction score
35,994
Leo waislam wameshinda kesi waliofungua dhidi ya BAKWATA kujipa mamlaka ya kuwaongelea waislam na kukwamisha miradi Kwa ukiritimba ati wao ndo watoe vibali Kwa taasisi zingine za kiislam

Shehe Ponda amesema mahakama katika hukumu hiyo, mahakama imeitamka kuwa BAKWATA sio taasisi inayosimamia Waislam wote Bali wale waliohiari kuwa chini ya taasisi ya BAKWATA

Pia Shehe Ponda ameahidi kuandaa kongamano kutoa elimu juu ya umuhimu wa hukumu ya Leo Kwa waislam
Assalam Alyekum

=======

WAISLAMU WAISHINDA KESI DHIDI YA SERIKALI NA BAKWATA MAHAKAMA KUU LEO 24/12/2025.

Majaji watatu leo wametoa hukumu ya kesi ya kikatiba iliyowasilishwa na Waislamu 12, Novemba 2024. Katika kesihiyo Waislamu hao walikuwa wanadai uhuru kwa Waislamu wa Tanzania wa kujiamulia mambo yao bila ya kulazimishwa kuwa chini ya taasisi nyingine yoyote ikiwemo BAKWATA.

Walioshitakiwa katika kesi hiyo ni Msajili wa Vyama Wizaraya Mambo ya Ndani, RITA, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na pia Bakwata na Baraza Kuu waliunganishwa.

Katika hukumu hiyo (ndefu), Jaji Mkwizu kwa niaba yamajaji wenzake 2, (waliokuwepo Mahakamani), alisema kwamujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Waislamu kama raia wengine, wako huru kuendesha shughulizao za kidini bila ya kulazimishwa kuwa chini ya chombochochote.

Jaji aliyasema hayo baada ya kusoma nyaraka kadhaa za vyombo hiyo vya serikali na Bakwata ambazo maudhui yake yanawalazimisha Waislamu kuwa chini yao kabla ya kupewa huduma zinzotolewa na mamlaka za serikali.

Akifafanua zaidi baada ya kunukuu vifungu vya Katiba ya Bakwata na Katiba ya nchi, alisema kwa mujibu wa sheria hizo Bakwata si Taasisi mama ya taasisi zote za Waislamu wala haina hadhi hiyo kwa Waislamu wote wa Tanzania.

Hukumu hiyo imezitaka mamlaka za serikali RITA na Msajili Wizara ya Mambo ya Ndani kuzingatia uhuru wa Waislamu kama raia wengine wanapohitaji haki zao za msingi kutoka kwao.

Hukumu hiyo iliyotolewa na majaji watatu imewapa uhuru vyombo vya serikali na Bakwata wa kukata rufaa endapo wanahisi hawakuridhika na hukumu hiyo.

Miongoni mwa matatizo wanayoyapata Waislamu waTanzania kutokana na kulazimishwa kuwa chini ya chombo kimoja ni pamoja na kukosa haki sawa na dini nyingine pale panapotakiwa uwakilishi au mgao wa haki mbalimbali zinazotolewa na serikali.

Kutokana na hukumu hii taasisi zilizoingizwa kwa hila bila yahiyari yao chini ya Bakwata au chombo kingine chochote, ziko huru kuendelea kua chini ya Baraza hilo au kujitoa nakuendesha mambo yake zikiwa huru.

Aidha waislamu waliopeleka shauri hilo Mahakamani (chiniya udhamini wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania), wanaandaa utaratibu utakao wezesha Misikiti yote na Taasisizote za Kiislamu Tanzania kupata hukumu hiyo kwa lugha ya Kiswahili na Kingereza ili waweze kuona uhuru wanaoupata kutokana na hukumu hiyo.

Ust. MUSTAFA M. ABEIDI

MSEMAJI WA JOPO LA WALIOSHITAKI - 0785998872
 
Attachments

Leo waislam wameshindwa kesi waliofungua dhidi ya BAKWATA kujipa mamlaka ya kuwaongelea waislam na kukwamisha miradi Kwa ukiritimba ati wao ndo watoe vibali Kwa taasisi zingine za kiislam
Shehe Ponda amesema mahakama katika hukumu hiyo, mahakama imeitamka kuwa BAKWATA sio taasisi inayosimamia Waislam wote Bali wale waliohiari kuwa chini ya taasisi ya BAKWATA
Pia Shehe Ponda ameahidi kuandaa kongamano kutoa elimu juu ya umuhimu wa hukumu ya Leo Kwa waislam
Assalam Alyekum View attachment 3520003
 
Nipo upande wa Sheihk Ponda toka Bakwata walivyouza eneo la waislamu pale Keko niliona ni wahuni tu aisee na eneo lenyewe pana mwislamu alitoa ili hilo eneo lijengwe msikiti mkubwa Daslm Viongozi wa Bakwata waliliuza kwa hela ndogo sana kisa walipewa rushwa kubwa hakuna taasisi ya Waislamu hapo ni wahuni tu.
 
Leo waislam wameshindwa kesi waliofungua dhidi ya BAKWATA kujipa mamlaka ya kuwaongelea waislam na kukwamisha miradi Kwa ukiritimba ati wao ndo watoe vibali Kwa taasisi zingine za kiislam
Shehe Ponda amesema mahakama katika hukumu hiyo, mahakama imeitamka kuwa BAKWATA sio taasisi inayosimamia Waislam wote Bali wale waliohiari kuwa chini ya taasisi ya BAKWATA
Pia Shehe Ponda ameahidi kuandaa kongamano kutoa elimu juu ya umuhimu wa hukumu ya Leo Kwa waislam
Assalam Alyekum View attachment 3520003
Waislam wameshindwa au wameshinda?
 
Hata hamjaelewa maamuzi BAKWATA kosa lao ni kutaka kila muislamu anapotaka kufanya jambo lake labda kuanzisha Taasisi yake lazima aanzie bakwata ambalo sio jambo sahih Bakwata ni taasis kama taasis nyingine zilizosajiliwa...

Katika suala la amani ya nchi hii na kinachoendelea kupambana na huu udini unaondelea ktk hii nchi waislamu wote msimamo wao ni mmoja kaeni mkilijua hili wagalatia...
 
Waislam wana akili hawa Bakwata ndo taasisi ya CCM
Sisi tunayopinga yanawakuta watu wa dini zote na wala hayaulizi dini
Waislam wanatekwa na kuuliwa refer Mzee Ali Kibao
Waislam wanakosa pia huduma ya maji ya kunywa
Waislam pia wanahijumiwa kwenye chaguzi
Waislam pia wanahitaji katiba mpya
Waislam pia wanakosa dawa hospital
Watoto wa waislam wanakosa madawati
 
Hata hamjaelewa maamuzi BAKWATA kosa lao ni kutaka kila muislamu anapotaka kufanya jambo lake labda kuanzisha Taasisi yake lazima aanzie bakwata ambalo sio jambo sahih Bakwata ni taasis kama taasis nyingine zilizosajiliwa...

Katika suala la amani ya nchi hii na kinachoendelea kupambana na huu udini unaondelea ktk hii nchi waislamu wote msimamo wao ni mmoja kaeni mkilijua hili wagalatia...
Wanataka Taasisi ziitambuwe Bakwata kama Supreme authority kwenye katiba zao. Jambo hili sidhani kwamba ni sawa kwa katiba ya nchi.
 
Back
Top Bottom