Mahabusu wajisaidia porini kwa kukosa vyoo

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,172
Mahabusu wajisaidia porini kwa kukosa vyoo



na Stephano Mango, Nyasa




MAHABUSU wa Kituo cha Polisi Lituhi, wilayani Nyasa, mkoani Ruvuma wanajisaidia porini kutokana na ukosefu wa vyoo na maji, hali inayoweza kusababisha mlipuko wa magonjwa mbalimbali.

Wakizungumza na Tanzania Daima jana kwenye eneo la kituo hicho cha polisi, mahabusu hao ambao hawakutaka majina yao yatajwe walieleza kuwa pindi wanapotaka kujisaidia huwajulisha askari waliopo zamu kituoni hapo ili wawapeleke vichakani kujisaidia.

Waliongeza kuwa wakati mwingine hulazimika kuwaomba ndugu zao kuwaletea maji ya kunywa na kuoga kwa madai kuwa kituo hicho hakina maji tangu kilipojengwa wala huduma nyingine muhimu kwa afya za binadamu.

Baadhi ya askari wa kituo hicho ambao hawakutaka kutajwa majina yao gazetini walikiri kuwepo kwa tatizo hilo pamoja na nyumba za kuishi, hivyo wamehifadhiwa kwenye nyumba za raia waliopo jirani na kituo hicho.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Michael Kamhanda, alikiri kuwepo kwa matatizo hayo na kusema kuwa yapo kwenye utekelezaji.
 
MAHABUSU wa Kituo cha Polisi Lituhi, wilayani Nyasa, mkoani Ruvuma wanajisaidia porini kutokana na ukosefu wa vyoo na maji, hali inayoweza kusababisha mlipuko wa magonjwa mbalimbali.

Hivi kweli gharama ya kuchimba choo ni shilingi ngapi???????????????????????????????????????????????

It is pathetic.....................................
 
Au kinachotafutwa ni hiki...................................................

Wanafunzi wawili wafariki dunia kwa kuhara



na Mwandishi wetu, Mbeya




WANAFUNZI wawili wa Shule ya Sekondari ya wasichana ya Samaritan iliyopo katika mji mdogo wa Mbalizi, mkoani hapa, wamefariki dunia na wengine 25 kulazwa kutokana na kukumbwa na ugonjwa wa kuhara na miguu kukosa nguvu.

Mkuu wa Shule hiyo, Faraja Mbwana, alitoa taarifa hiyo kwa Ofisa Elimu wa Mkoa, Juma Kaponda, ambaye alifanya ziara shuleni hapo ili kujionea hali halisi baada ya kutokea vifo hivyo.

Mbwana alisema kuwa tatizo la wanafunzi kukumbwa na ugonjwa huo lilianza mwishoni mwa mwezi uliopita, baada ya mwanafunzi mmoja kuugua na kulazwa.

"Baada ya mwanafunzi huyo kulazwa katika zahanati ya shule, tatizo liliendelea katika siku zilizofuata na idadi iliongezeka na kufikia 25. Hali ilipozidi kuwa mbaya, tuliamua kuwapeleka katika hospitali teule ya serikali ya wilaya Ifisi," alisema mwalimu huyo.

Akitoa ufafanuzi zaidi, mganga wa zahanati ya shule hiyo, Dk. Ernest Mwasaga, alisema wanafunzi hao walikuwa wamekumbwa na matatizo mawili tofauti, ambapo tatizo la kwanza ni kuharisha na tatizo jingine ni kupoteza nguvu ya miguu.

Kwa upande wake ofisa elimu wa mkoa Kaponda baada ya kumaliza ukaguzi aliuagiza shule hiyo kufungwa, kisha kurekebishwa kasoro zilizotolewa na wataalamu ndani ya siku 10 ili wanafunzi waweze kuendelea na masomo.
 
Back
Top Bottom