Mahabusu wagoma, wavua nguo

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Mahabusu wagoma, wavua nguo


Na Muhidin Amri, Songea

MAHABUSU wanaokabiliwa na kesi za mauaji wamegoma kupanda gari la polisi kurudi gerezani na baadhi yao kuvua nguo kwa madai ya kucheleweshewa upelelezi wa kesi zao zinazazowakabili.Tukio hilo lilitokea jana pale
mahabusu hao wapatao 20 walipotolewa na polisi nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Ruvuma, kurudishwa magereza kusubiri tarehe ya kusikilizwa kwa kesi zao.

Mahabusu hao walichukua hatua hiyo kwa madai ya kucheleweshwa kwa kesi zao ambazo ni za muda mrefu huku wengine wakibadilishiwa kesi za awali na kusomewa mpya, tofauti na zile walizokamatwa nazo.

Akizungumza kwa niaba ya maabusu wenzake, Bw. Rashid Gayo alisema kuwa wamefikia uwamuzi huo baada ya kuchoshwa na tabia ya kucheleweshwa kwa kesi hizo ambazo ni za muda mrefu, huku wakimtuhumu kigogo wa polisi anayehusika kwa upeplelezi kwa kuwaomba rushwa.

Alisema kuwa lengo mgomo huo ni kutaka kufikisha ujumbe kwa vyombo vinavyohusika ili vichukue hatua zinazostahili.Alidai kuwa kigogo wa upelelezi mkoani humo amekuwa na tabia ya kuwaomba fedha ili kuharakisha upelelezi wa kesi zao, huku akifahamu kwamba uwezekano wao kupata fedha hizo ni mdogo.

Kamanda wa Polisi mkoa ni Ruvuma, Bw. Michael Kamuhanda alisema kuwa mahabusu kugoma ni haki yao ya msingi lakini, kitendo cha kuvua nguo hakiwezi kuwa ndiyo sababu ya kuharakisha upelelezi wa kesi zinazowakabili.

Akisema mahabusu hao wameshawahi kugoma kula na alikwenda gerezani kuongea nao na aliwahaidi kuchukua hatua kuharakisha upelelezi huo, na kuwataka mahabusu hao kuwa kusubiri upelelezi wa kesi zao.Alisema jeshi lake halina namna ya kuwasaidia mahabusu hao, kwani hata majalada ya kesi zao bado yako kwa Mkurugenzi wa Mashataka (DPP).
 
Mahabusu hao walichukua hatua hiyo kwa madai ya kucheleweshwa kwa kesi zao ambazo ni za muda mrefu huku wengine wakibadilishiwa kesi za awali na kusomewa mpya, tofauti na zile walizokamatwa nazo.

Jaji Mkuu mpya anakaribishwa na haya.....................polisi wanakamata washukiwa kumbe hata ushahidi haujakamilka na hakuna ukomo wa kumshikilia mtuhumiwa kabla ya kumfikisha mahakamani na kesi kuanza kusikilizwa.......................
 
Back
Top Bottom