Mahabusu afariki akiwa Mikononi mwa polisi

Bahati furaha

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2012
Posts
3,077
Reaction score
1,439

wambura.jpg

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura.

Kwa ufupi
Alfred aliyekuwa mkazi wa Sinza jijini hapa, alifikishwa kituoni hapo kwa kosa la wizi wa kuaminiwa na kuwekwa mahabusu wakati akisubiri kufikishwa mahakamani juzi(Jumatatu) ili kusomewa mashitaka yake.

Dar es Salaam
Mahabusi Daniel Alfred katika kituo cha Polisi Urafiki, eneo la Ubungo, amefariki dunia kwa madai ya kupigwa na baadhi ya askari wa kituo hicho.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura jana alithibitisha kutokea kwa kifo hicho, huku akisema kijana huyo alikuwa akifanya fujo na kuwapiga wenzake wakati akiwa chumba cha mahabusu.

Kamanda Wambura alisema kuwa baada ya kifo chake waliupeleka mwili wake hospitali.

Wambura alisema ripoti ya daktari baada ya uchunguzi, ilionyesha kwamba mahabusi huyo alikuwa mgonjwa.

Shuhuda ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini, alisema alikwenda kituo hapo kumuona ndugu yake lakini alikuta askari wakimpiga.

"Mimi sijui kama alikuwa na matatizo ya kiafya, lakini niliona akipigwa sana na askari wa kituo hicho...yaani inasikitisha sana, jamaa alipigwa kama mpira wa gombania goli, mimi nilikuwa najua kituo cha polisi ndiko usalama wa watuhumiwa unapatikana kumbe hapana ndiyo maana nikaja kuwaeleza nilichokiona," alisema mtoa habari huyo.

Alisema hata kama kijana huyo alikuwa mgonjwa, anaimani kuwa aliuawa na polisi kwa kipigo kikali.

CHANZO:Mwananchi.co.tz

Polisi hawana adabu wala utu. Akili zao sijui wamemkabidhi nani yaani wanajiamlia tu kutoa uhai wa raia hata kabla ya kuwafikisha mahakamani na kuhukumiwa
 
ANASEMA:
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura jana alithibitisha kutokea kwa kifo hicho, huku akisema kijana huyo alikuwa akifanya fujo na kuwapiga wenzake wakati akiwa chumba cha mahabusu.
HALAFU ETI:
Wambura alisema ripoti ya daktari baada ya uchunguzi, ilionyesha kwamba mahabusi huyo alikuwa mgonjwa.
Hivi huyu kamanda ni mzima upstair?
 
Ndo maana nasema polisi wote wananuka ukosefu wa utu.
 
Hata mimi nimeshangaa mgonjwa gani anaweza kufanya fujo na kuwapiga wenzie mmh hii kali
ANASEMA:
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura jana alithibitisha kutokea kwa kifo hicho, huku akisema kijana huyo alikuwa akifanya fujo na kuwapiga wenzake wakati akiwa chumba cha mahabusu.
HALAFU ETI:
Wambura alisema ripoti ya daktari baada ya uchunguzi, ilionyesha kwamba mahabusi huyo alikuwa mgonjwa.
Hivi huyu kamanda ni mzima upstair?
 
Hata mimi nimeshangaa mgonjwa gani anaweza kufanya fujo na kuwapiga wenzie mmh hii kali

Watu kama hawa tungepata na CV zao labda huenda wasingetushangaza kwa maelezo kama hayo.
 
polisi hawawezi kuwa na uelewa wa kuchambua mambo analytically kichwani kwa sababu mnajua history ya kuwa polisi ikoje, c lazima ufeli kwanza au? ndo maana sentensi zao ni za ajabu sana, fikiria ile ya arusha, then hii. huyu kasema alikuwa anapiga wenzake ndo wakaamua kumuuua sijui, then doctor anasema alikuwa mgonjwa, polsi nae bila hata kufikir mwanzo kaongea nn anajibu kama alivyosikia, alikuwa mgonjwa ndo akafa. hizi n akili ya samaki et
 
ANASEMA:
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura jana alithibitisha kutokea kwa kifo hicho, huku akisema kijana huyo alikuwa akifanya fujo na kuwapiga wenzake wakati akiwa chumba cha mahabusu.
HALAFU ETI:
Wambura alisema ripoti ya daktari baada ya uchunguzi, ilionyesha kwamba mahabusi huyo alikuwa mgonjwa.
Hivi huyu kamanda ni mzima upstair?

LLB holder ni mwanasheria huyo
 
n
wambura.jpg

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura.

Kwa ufupi
Alfred aliyekuwa mkazi wa Sinza jijini hapa, alifikishwa kituoni hapo kwa kosa la wizi wa kuaminiwa na kuwekwa mahabusu wakati akisubiri kufikishwa mahakamani juzi(Jumatatu) ili kusomewa mashitaka yake.

Dar es Salaam
Mahabusi Daniel Alfred katika kituo cha Polisi Urafiki, eneo la Ubungo, amefariki dunia kwa madai ya kupigwa na baadhi ya askari wa kituo hicho.

Alfred aliyekuwa mkazi wa Sinza jijini hapa, alifikishwa kituoni hapo kwa kosa la wizi wa kuaminiwa na kuwekwa mahabusu wakati akisubiri kufikishwa mahakamani juzi(Jumatatu) ili kusomewa mashitaka yake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura jana alithibitisha kutokea kwa kifo hicho, huku akisema kijana huyo alikuwa akifanya fujo na kuwapiga wenzake wakati akiwa chumba cha mahabusu.

Kamanda Wambura alisema kuwa baada ya kifo chake waliupeleka mwili wake hospitali.

Wambura alisema ripoti ya daktari baada ya uchunguzi, ilionyesha kwamba mahabusi huyo alikuwa mgonjwa.

Shuhuda ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini, alisema alikwenda kituo hapo kumuona ndugu yake lakini alikuta askari wakimpiga.

“Mimi sijui kama alikuwa na matatizo ya kiafya, lakini niliona akipigwa sana na askari wa kituo hicho...yaani inasikitisha sana, jamaa alipigwa kama mpira wa gombania goli, mimi nilikuwa najua kituo cha polisi ndiko usalama wa watuhumiwa unapatikana kumbe hapana ndiyo maana nikaja kuwaeleza nilichokiona,” alisema mtoa habari huyo.

Alisema hata kama kijana huyo alikuwa mgonjwa, anaimani kuwa aliuawa na polisi kwa kipigo kikali.

CHANZO:Mwananchi.co.tz

Nchi hii imelaaniwa.Polisi wako juu ya sheria.Ni polisi hao hao,ni mahakimu hao hao na ni magereza hao hao.Hatuna wa kuwawajibisha hao miungu watu
 
Dawa kuikataa "KATIBA ELEKEZI" ili iandikwe nyingine itakayokuwa na mambo kama hayo.
 
Mtu mgonjwa anawezaje kuwapiga mahabusu wenzake? Tukubali kuwa alikuwa mgonjwa; je, ugonjwa wa akili? Kama alikuwa mgonjwa wa akili, kwanini awekwe mahabusu moja na watuhumiwa wengine? Mtu mmoja, tena wa kawaida, anawezaje kuwashinda nguvu mahabusu wengi hasa ikizingatiwa huyo (marehemu) hakuwa na mafunzo ya ukomando? Kwa haya na mengine, kwanini wananchi wasiamini kuwa polisi wanahusika moja kwa moja kwa kifo hiki? Jamani polisi, fikirieni kama ndo ninyi ambao ndugu zenu wakikamatwa wanauawa kipuuzi namna hii! Kaeni upande wa pili mjiulize kama ni ninyi, mtajisikiaje?
 
Ehheee! Kama nimesoma vizuri Kamanda amesema aliwafanyia wenzake fujo humo mahabusu, hakusema aliwapiga. Sasa kama walikuwa zaidi ya watano walipompiga, sidhani waliangalia ni sehemu zipi za kupiga. Mungu aiweke roho yake peponi
 
Polisi hawana adabu wala utu. Akili zao sijui wamemkabidhi nani yaani wanajiamlia tu kutoa uhai wa raia hata kabla ya kuwafikisha mahakamani na kuhukumiwa

Usisikie ya magazetini na kuhukumu, fuatilia kiundani, lazima kina kitu hakijawekwa sawa.
 
Kuna watu ambao katika dunia hii wanahitaji msaada wa kusemewa kwani wao hata wakiongea hawatasikika na hata wakisimama hawataonekana kamwe.
Watu hawa ni wafungwa na wagonjwa wa akili. Watu hawa wanahitaji msaada wa karibu sana wa wanasheria ili kulinda haki zao.
Gerezani kuna mambo mengi sana...
Rest in Peace.
 
Juzi wamemuua Yahya wa Arusha wakidai alitaka kuwatoroka wao polisi huku akidai wakiwa ktk ulinz mkali, Leo tena eti mahabusu kawafanyia vurugu wenzake, hv solution ilikuwa ni kumtoa uhai? Na je puu... polisi mtatuaminisha vp kuwa ninyi ni wana usalama ili hali mnafanya vitu ambavyo vipo kinyume kabisa na maadili ya kazi yenu? Hakuna viumbe nawachukia kama hawa(police).
Mbona police wa Brazil wao walithubutu tu kuwajeruh waandamanaji na ikasababisha wao kufukuzwa kazi-vp hapa waue na waeendelee kula bata?
 
kuna watu mamburula sana yaani habari ummeichukua gazetini na kuanza kupayuka hovyohovyo tu hivi una uhakika gani na hilo gazeti kuwa limesema ukweli kuwa kamanda wambura ndivyo alivyosema?. kuhusu elimu huyo anashahada ya sheria chuo kikuu cha Dar es salaamm sasa kama chuo hicho kinatoa elimu feki mtuambie pia huyo kamanda kasomea elimu mbalimbali za uongozi na upelelezi ndiyo maana kafikia daraja hilo la kupewa madaraka ya uRPC. tuache kuropokaropoka bila kufanya utafiti wa kina kisa tu hisia zako zinakupeleka unakokuwaza.
 
Back
Top Bottom