Magumu gani umeyapitia/unayapitia katika kutafuta kazi?

Vipajilink hao mkuu....kama sijakosea.

Sijawataja, najua hata humu jukwaani wapo sana tu na wameiona hiyo post yangu. Naomba waache kabisa huo mchezo maana najua "ustaarab wa mtu sio kuvaa nguo nzuri na tai tu!". Proffessional ya mtu ni pamoja na mambo anayotafanya. Sijajua km watakuwa ndio hao jamaa uliowataja au lah! japo hujakosea saaaana!111111
 

aisee! mkuu mbona hapo kama umezidisha chumvi!" ...........

Grand PA
 

mwaka juzi kuna siku niliitwa kwa interview dar nikakopa adi nauli.The interview was okay waliuliza simple questions wakasema majibu watatoa after 2 weeks.Kesho yake nkaanza safar ya kurud mkoan hata kabla hatujafika chalinze nikatumiwa msg'tunapenda kukutaarifu kuwa haukuchaguliwa kweny usaili....etc'...just imagine hio safar ilivokua..ni shiidaa!
 


Hongera yaani wewe miezi mitatu tu.mie miaka 4 ,then nikaja kupata sehemu fulani tena niliingia kwa gia ya kijitolea kwanza, siwezi sema ni kazi ila angalau pesa za matumizi ya kawaida sikosi.loh dunia ina majaribu hii...
 
Hata ukifika kwenye usaili unakutana na vikwazo

unaulizwa maswali ya ajabuajabu ya kukomolewa ili mradi tu ushindwe kujibu

hii ni aina nyingine ya udhalilishaji

Nilihudhuriaga oral intetview ya post ya Network Specialist. Cha ajabu niliulizwa maswali ya Programming. Mpaka nikawauliza mbona mnaniuliza maswali ya Programming na wkt post ni networking. Wakajibu,ww si IT utashindwaje kujua programming bwana. Nilichoka kwa kweli..
 

Hiyo ya mtu wa interview panel kusoma maswali ktk karatasi ipo sana kwa oral interview za secretariat ya ajira. Inaboa kweli,mana huyo anakuwa na jibu lake/marking. Ukiende tofauti na yy inambulia marks chache.
Nilipenda ule usahili wa PCCB kwa upande wa IT. Panel ilikuwa na watu 9,ila hauhulizwi maswali na watu wote km ilivyo kwa secretariat. Na anayekuliza maswali ya technical,alikuwa anayatoa kichwani kutokana na experience yake. Kweli jamaa walijipanga vzr sana.
NB: Ingawa nadhani walikuja kuchakachua majina ya kuitwa kazini.
 

Duh..!! Ilimradi tu ushindwe kujibu.
 
vijana wengi tunakua na mawazo ya kujiajri suala linakuja mitaji tutapata wapi? pia kuna baadhi ya NG'OS hapa nchini ambazo zinasema zipo kwa lengo la kusaidia vijana wajikwamue na umaskini na zinapata misaada kutoka mashirika ya nje lakini kinyume chake hiyo misaada haiwafikii walengwa,mfano mzuri mimi pamoja na rafiki zangu tuliitwa na hiyo NG'O tukahudhuria semina ya wiki moja ambayo walitufundisha masuala ya customercare na jinsi ya kuandaa business plan then wakasema tuandike business plan ili tuweze kupata mkopo, kweli tuliandika business plan tukawapelekea wakaikubali kua ni nzuri na watatupa mkopo lakini cha ajabu kila tukifuatilia mara njooni kesho mara mkurugenzi kasafiri mara hatuwezi kumpa kijana fedha nyingi atazitumia vibaya!!! yaan ni usumbufu kiasi kwamba hata member wengine washaanza kukata tamaa ya kupata huo mkopo,swali tukajiuliza kama waliona hawawezi kumpa kijana kiasi kikubwa cha pesa kwanini walituita na kusema tuandike bussiness plan
 

Walidhani hamtaweza kuandaa plan... Hao hela washatafuna
 

Kwel kabisaaa!
 
nadhani tuanzishe chama cha wasio na ajira tanzania(ccwt) kupitia hicho chama tuchague uongozi na kupitia michango midogo midogo tutaweza kufungua hata fixed account bank yoyote baadaye tukajiajiri tuko wengi jaman na ajira ngumu sana,ntasikitika sana waliosababisha haya wakirudi madarakani mwaka 2015,wameshindwa kupanga sera za kumkomboa kijana kwa miaka mingi,wanadai tujiajiri wao waajiriwa wa serikali,tunazunguka na vyeti barabarani wao wanazungusha viuno bungeni it real pain.....
 

Mwansile
Wazo zuri
Je? sis wenyewe tuna umoja?
 
Sitakuja kusahau usaili wa bugando medical centre. ..

Yan wale jamaa live walikuwa na Watu wa kuwaweka ktk administrative posts..

Eh eti mtu anakuuliza

1. taja madirector 5 wa bugando wa miaka iliyopita
2. taja mawaziri 5 wa afya wa miaka iliyopta
3. jieleze kwa maneno 5. , yan from nowhere.......
 

Kweli hapo mkuu bora niache,yaani nakuwa kama shule ya msingi daaa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…