Magufulification ni kishindo kipya Malawi

Mugabe one

JF-Expert Member
Nov 15, 2016
2,327
1,681
Huko Nchini Malawi kuna operation inaitwa Magufulification imeanza kazi rasmi watumishi wote wa Serikali wametakiwa kupeleka na kuonesha vyeti vyao Halisi walivyoajiriwa navyo.

Aliyekuwa mkuu wa Kitengo cha ulinzi wa Rais ametiwa nguvuni kwa kosa la nyuma la tabia ya kuingia bidhaa na vitu mbalimbali bila kulipa kodi yoyote!

Baadhi ya wafanyabiashara pia nao wametiwa nguvuni kwa kosa la kutolipa kodi.

Thank you President Magufuli umeiamsha Afrika.
 
Waswahili wanasema, punda haendi bila mchapio. Lele mama, yaani yaani, msalie Mtume, tafadhali n.k. sio lugha ambazo sisi waafrika tunazielewa.

Awamu ya kwamza ya Baba wa taifa kulikuwa hakuna yaani yaani ila kukaza boot tu na mambo yalionekana na sina haja ya kuyarudia yote hapa. Udokozi ulikuwepo kwa kiwango cha chini sana kwani Azimio la Arusha lilikuwepo hivyo kuzuia ufisadi usitokee. Udokozi ulikuwa kwa ajili pesa ya kula tu kwani vitu vya anasa havikuwepo.

Awamu ya pili ya mzee Ruksa ikapandisha wizi kutoka kwenye udokozi kwenda kwenye wizi wa mamilioni kwa ajili ya kujenga nyumba na kusomesha watoto shule za private. Awamu hii watoto wengi wa wakubwa tuliwaona wakipelekwa kusoma Kenya na nchi za ulaya.

Uwepo wa uchumi huria uliongeza tamaa ya watendaji wa serikali kijilimbikizia mali kwani Azimio la Arusha lilianza kufutika na ufuatiliaji wa wezi wa mali za uma na wakwepa kodi haukuwepo kwa kiwango kinachostahili.

Magari, televisheni, friji n.k. viliongeza rushwa makazini na kuwafanya wafanya kazi wa serikali wote kuwa waomba rushwa kwa kila aina ya huduma.

Awamu ya tatu ilikuwa ni muendelezo wa rushwa kwa kiwango cha juu zaidi. Mali za serikali ziligawanwa na kuuzwa hovyo kwa kisingizio cha privatization na serikali kujitoa kwenye shughuli za biashara. Hapa wizi ukawa ni wa mabilioni kwani mafisadi wakaanza kumiliki majumba ya kifahari na money laundering ndio ilishamiri. Viongozi sasa kumiliki majumba kwenye world capitals kama Nairobi, Johannesburg, Dubai, London n.k.

Kashfa kubwa za ufisadi kama radar, meremeta, benki kuu n.k.

Awamu ya nne ndio ufisadi ulivuka mipaka na kashwa zao nyingi tu zikiwemo za Richmond, Tegeta Escrow, ma- container yasiyo lipiwa kodi n.k.

Hapa watu walikuwa wanafanya kufuru. Walikuwa wanaiba mpaka kwa ajili ya wajukuu zao wasipate shida wakati wenyewe wameisha fariki. Fikiria mfanyakazi wa serikali ana nyumba sabini na watoto wa vigo go kwenda likizo London na Dubai.

Kwa hiyo basi, bila MAGUFULIFICATION, Africa haiwezi kwenda popote and that's the only language that Africans can understand.

Raisi lelema, lakhe lakhe, yaani yaani, mpole mpole au wasukuma wanasema, a gentleman president, hawezi kuleta maendeleo na swindlers will take advantage of him. Kikwete alilaumiwa sana kwa hili kwa kuwa too nice and lack of action when it comes to graft.

Hussein Mwinyi kidogo tu akose nomination as a CCM flag bearer in Zanzibar presidential election due to alleged weakness.

Kama Magufuli ndio muarubaini wetu, time will tell but so far we can see the light at the end of the tunnel.
 
Back
Top Bottom