Kenya wametupiga kwenye mshono tena

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,337
KENYA WAMETUPIGA KWENYE MSHONO TENA.

Kenya umepiga marufuku mahidi ya Tanzania kwa kuwa Yana sumu inayosababisha Cancer na wametangaza hadharani na wameitangazia Dunia.

Mwaka 1776 Jasusi wa Kimarekani William Carmichael alitumwa na Taifa lake kwenda kutafiti na kujua ni kwa namna gani USA inaweza kuteka soko la Tumbaku Duniani ambalo lilikuwa limeshikiliwa na bara Ulaya. Kipindi hicho Ukraine ilikuwa ikizalisha tumbaku Bora kabisa na nyingi Duniani.

Jasusi huyu alitokea kwenye kitengo Cha Economic intelligence. Economic intelligence ni kitengo katika mashirika ya kijasusi mengi duniani lakini department hii hudili na kuangalia threats za nchi husika kiuchumi. Hawa hutafiti, huchunguza mataifa Mengine kuhusu Uchumi wao na namna ya kuudidimiza. Marekani wao kwa Sasa Taifa ambalo linachunguzwa Sana ni China na Korea Kaskazini. Lengo ni kuwadhibiti wasiliteke soko la Dunia kwa bidhaa zao au wasiibuke Kama super power duniani.

Sio nchi kwa nchi tu huchunguzana Bali hata Kampuni na Kampuni zinazozalisha bidhaa za aina Moja huchunguzana. Nafikiri unakumbuka mgogoro wa Simu za Huwawei na Kampuni la Google.

Kwa Africa Mashariki Kenya ni mojawapo ya Taifa ambalo limewekeza kwenye Economic intelligence, na Taifa tishio kwao ni Tanzania. Tukumbuke Tanzania ina rasilimali nyingi kuliko Kenya, ina nufaika na Geographical location yake na pia hatuna ukame Sana.

Kenya wanajua wazi kuwa isingelikuwa bandari ya Daresalam na Tanga Basi wao wangenufaika Sana kupitia bandari ya Mombasa. Bandari zetu zinapunguza Sana bidhaa za mataifa Mengine kupitia Kenya hili kwao ni tishio.

Kenya wanajua kabisa Kama sio vivutio vyetu tulivyo navyo Basi wao wangeongoza kwa utalii Africa Mashariki na wangelipiga pesa nyingi Sana kwenye utalii.

Mwaka juzi madereva wa Tanzania wa utalii pamoja na kuwa walifuata taratibu zote walinyimwa kuchukua watalii waliokuwa wanakuja Tanzania kutalii ambao walishukia Kenya. Tanzania ilivumilia kwa Muda lakini ilifika mahali tukajibu kwa kupunguza trip za Kenya airways kuja nchini. Walipoona hivyo wakaondoa lile zuio la madereva wetu wa utalii kuingia Kenya. Ndio maana nchi iliwekeza Sana kwenye Kununua ndege kwa kuwa ili ujitawale vizuri lazima uwe na uwezo wa kushindana angani, ardhini na majini.

Mwaka 2018 tuliingia nao tena Mzozo wa kiuchumi tukigombea bomba la mafuta toka Uganda lipitie wapi. Wakenya walipiga trip Sana kwenda Uganda kwa mzee Museven hatimaye tukawashinda Tena kwenye Vita ile.

Mwaka 2020 wakati wa Corona Madereva wote wa Tanzania ilikuwa hawaruhusiwi kuingia Kenya lakini wa Kenya walikuwa wakiruhusiwa Hadi tulipifunga mipaka ya Hororo kule Tanga na Namanga Arusha ndio walitia akili wakatuachilia.

Mwaka 2021 mwanzoni kule Rombo ilikuwa dereva wa Bodaboda akivuka Kwenda Kenya alikuwa akishikwa na kufungwa au kufunguliwa Kesi. Mkuu wa Mkoa Wa Kilimanjaro alipambana na issue hii Sana na naimani imetulia kwa Sasa.

Kuna kipindi wakenya walitaka kuwafukuza wafanyabiashara wote waliopo Nairobi toka Tanzania nafikiri mnakumbuka.

ISISUE YA MAHINDI.

Kwanza Kenya wametufanyia mbaya Sana kutangaza Moja kwa Moja bila kutupa taarifa kama jirani mwema tuyapime Kama kweli yana Sumu. Tafsiri rahisi Ni kwamba mahindi yetu yatakuwa yamekosa soko kwenye nchi zote kwa kuwa tu Kenya imetangaza Moja kwa Moja kuwa yana Sumu.

Sijui kama Balozi wetu Kenya anafanya kazi gani Ila ningeshauri abadilishwe apelekwe mtu mwingine mwenye uwezo wa kunusa mbali na mwenye ushawishi na anayeweza kutibu mipasuko ya nchi zote mbili. Taifa hili lina vijana Smart wanaoweza kucheza hii michezo kwa umadhubuti mkubwa..... Tuna nchi ambazo tuna maslahi nazo Kama Kenya si pa kupeleka Balozi Ni Balozi economic intelligence huanzia hapa. Someni historia ya Balozi wa Kenya nchini Tanzania. Yupo very Smart Hadi Rais aliwahi kutamani kumpa uraia.

Nalaumu kuhusu Balozi lakini pia idara nyingine kwa kuwa Kenya toka mwaka Jana walishaonyesha interest ya kununua mahindi toka Mexico, Malawi na Zambia kwa kuwa aidha wanayapata kwa Bei rahisi na hakuna mlolongo wa Kodi. Fuata link ifuatayo ambayo gazeti la the East African lilishaonyesha Dalili kuwa Kenya itaagiza mahindi toka kwenye hayo mataifa.

Kenya in plan to import 2m bags of maize by May

Inawezekana Kenya imeyapata Mahindi kwenye mataifa hayo kwa Bei Rahisi zaidi kuliko hapa kwetu. Na Kenya wametunyima Soko la mahindi kipindi ambacho wanauhitaji mkubwa Sana w mahindi kutokana na Nzige na Corona.

Tulitamka hadharani kuwa wakati watu wakiwa lockdown sisi tulime mahindi tutakuja kuwauzia. Sasa kwa kauli hii ya Kenya hatutauza popote. Tuboreshe idara zetu nyeti.

Wametuotea katika hili. Je, ni kweli yana sumu au ni Siasa ya kiuchumi? Wametupiga panapouma.

Pia soma; Tanzania ni Taifa kubwa, tusiyumbishwe
 
Achana na hao jamaa wanajitekenyaga na kucheka wenyewe!

Wao huhisi ni wazungu!

Wamechukua hayo maamuzi kwa influence ya mabepari wanaoimiriki Nairobi, lakini wakazi wa kibera na maeneo mengine ya nchi ndio wataamua kama mahindi toka Tanzania yataendelea kuingia au la!

Wait and see!
 
Kuna mgombea mmoja wa Urais kwenye kampeni za 2020 alisema tatizo letu Tanzania tunajiona special sana, kana kwamba tunayofanya hapa hayawezi kufanyika Nchi nyingine haya ndio majibu yake, kumbe Kenya inaweza kununua mahindi kutoka Mexico tena kwa bei rahisi, hili liwe fundisho kwa watawala kwamba Tanzania tunaihitaji dunia kwa kuwa na ushirikiano mzuri na kila Nchi.

Hapa tuombe Mungu hii vita itatuliwe kiungwana, vinginevyo tutahamia kwenye maparachichi na bidhaa zingine, hali itakuwa mbaya sana kwetu wakulima na wafanyabiashara.
 
Mtoa hoja umeelezea vema ila future ya Africa kibiashara ni DRC,sio Kenya,Rwanda au jirani zetu wengine.ni wakati wa kuimarisha bandari yetu ya Dar kiufanisi sio majengo,tuijenge upya ikiwa na kuipanua barabara yetu ya Dar to Tunduma ikiwa na kuwaomba wazambia waongeze kasi ya ukarabati wa barabara yao hasa kutoka Mpika hadi Nakonde, haya yakikamilika our no 1 aitembelee DRC na kuwaeleza uwezo wetu wa kuhudumia bidhaa zao(we just need 40%tu ya bidhaa za DRC)kinyume cha hapo tutaendelea kuumia kibiashara, Zambia ameimarisha barabara yake inayokwenda Zimbabwe (thr Chilundu border post)na ile inayokwenda kwenye borders zake na Namibia na Botswana, tuambiane ukweli bidhaa nyingi za DRC zinaelekezwa Durban na Walvis Bay na mbaya zaidi lile daraja linalounganisha Zambia na Botswana limekamilika sasa sisi tuendelee kumtafuta mchawi wetu wakati sisi wenyewe ndio tunajiloga.
 
Utawaweza Kenya walio feli kiuchumi, huu umekuwa mtindo wao wa muda mrefu wakiwa wanatafuta njia ya kuonge na TZ. Tokea enzi za Kikwete, walikuwa wanabania vitu vyetu, tukijibu mapigo wanatuma waziri haraka kuja kusulimisha na kuongeza mengine wanayoyataka.

Lakini kwa kipindi hichi nashauri serikali iwape kibano halafu ikae kimya kidogo, soko la mahindi na bidhaa zingine za kilimo ni kubwa sana duniani. Hakuna kitakacho doda.
 
Yule mkulima mkazi wa Arusha mwenye gunia zake 100 aliyekuwa anawasubiri wakenya huku mke wake akiwa ameajiriwa kampuni ya utalii na hajalipwa mshahara mwezi wa 5 huu na watoto kwenye hoteli za nyota kadhaa sizizo na wageni ataumia sanaaa.
 
Ujinga wa hawa jirani zetu hawakumbuki kwamba sisi ndio soko lao kubwa...wameanza tukimaliza wasilalamike!
Dawa ya moto ni moto tu. Natarajia vikwazo vya haraka sana kwa bidhaa zao zinazo uzwa ndani ya nchi yetu.

Kama tulivyo wajibu kwenye ishu ya corona na ndege za abiria. Hawa manyang'au kamwe wasipewe nafasi ya kujiona wako juu yetu na wakati sisi ni kaka zao.
 
Na ni gharama sana kuagiza mahindi toka Zambia, alafu Zambia au Malawi hawana mahindi mengi kama Tanzania, pia kuagiza mahindi toka Mexico ni mbali sana gharama kubwa plus time, Kenya watapata tabu sana wakituletea ujinga na bidhaa zao tutapiga ban zote, yaani Kenya wasituchezee kabisa, jangwa kwao ni kubwa. Njaa haina ubabe na bado.
 
Manyang'au njaa itawaua na njaa haina ubabe.. Na ni gharama sana kuagiza mahindi toka Zambia, alafu Zambia au Malawi hawana mahindi mengi kama Tanzania, pia kuagiza mahindi toka Mexico ni mbali sana gharama kubwa plus time, Kenya watapata tabu sana wakituletea ujinga na bidhaa zao tutapiga ban zote, yaani Kenya wasituchezee kabisa, jangwa kwao ni kubwa. Njaa haina ubabe na bado.
Wanacheza na Akili za Wabongo hawa.
Watajirudi tu
 
Mimi pamoja na kwamba ni mtanzania kila siku huwa nashindwa kuelewa hivi hizi kelele za kusema Tanzania tuna rasilimali nyingi kuliko Kenya wakati huo huo Kenya yenye rasislimali chahche ina GDP kubwa kuliko Tanzania pamoja na kuwa population yetu pia ni kubwa tunakuwa tuna maanisha nini.

Nchi yenye rasilimali nyingi inakuwaje ni masikini kuliko hiyo Kenya. Hata mapato ya kodi ya kenya kwa mwaka ni karibu mara mbili ya mapato ya Tanzania sasa kelele ni zanini kwamba sasa Kenya inaiogopa Tanzania kwa hivi tunavozidi kuwa masikini waliacha kituogopa wakati Uchumi wetu ukikua kwa 7.2 percent waogopa sasa unapokuwa kwenye makaratasi tu.

Ni mambo ya kuchekesha sana. Hivi ni mamlaka gani hapa nchini inayoweza kusema imepima ubora wa mahindi yanayouzwa nje na utaratibu wa kupima hayo mahindi ukoje.

Ni vema tukapokea hiyo kama changamoto na kupima mahindi yetu na kuona je hayana asilimia kubwa ya sumu sasa kama tumeshalaumu hadi nchi ambazo kwa uwezo wa tekinoljia yao zingeweza kusaidia kupima na kutoa majibu kuhusu mahindi yetu. Basi tuhesabu tunajichimbia shimo wenyewe.
 
Back
Top Bottom