Magufuli: Wanaopita kwenye barabara za mwendokasi chomoeni tairi za magari yao muuze

Nilikuwa nasubiri wanafunzi wa UDOM nao wagome, wangeondoka wote- Rais Magufuli

Tumeleta mradi wa mabasi ya mwendo kasi lakini watu wanajisaidia humo. Mkuu wa Mkoa, Wilaya, Polisi wapo. Wapelekeni wakajisaidie gerezani-Rsis Magufuli

Badala fedha ziende kujenga maabara, madarasa na madawati, zinaenda kuwalipia vilaza.- Rais Magufuli

"Trafiki wakamate magari yanayopita barabara ya magari yaendayo kasi na kutoa matairi na wakihojiwa wajibu, lilikuja bila matairi."-Rais Magufuli
kazi kweli..
 
Ni janga kubwa la Taifa huyu. Hajui hata kipi anastahili kuongea na kipi hakistahili kuongelewa.

Naliona taifa likiwa limepoteza dira sijui nani atalikomboa taifa maana naodha hajui tunakoenda nae anahitaji kuongozwa
 
  • Thanks
Reactions: BAK
kauli kama hii angeitamka mtu kama jk enzi zake ingekua poa tu, kwasababu ni mtu wa masihala wakati wote. lakini kwa magufuri kwasababu sio mtu mwenye uso wa masihala, ahakilishe anatamka kwa kufuata hotuba tu, la sivyo kila siku kauli zake zitakosolewa tu. magufuri anatakiwa amuige mkapa maana mkapa ni mtu asiependa utani na siku zote anahakikisha annafuata hotuba aliyoandaliwa na wataalam wake.
 
Kwa hiyo RAIS anasapoti wizi wa matairi ya magari ya watakaokamatwa? Kweli you can take a bushman from the bush but can't take the bush out of him. Let's go.....
 
ngoja ninoe panga na sime yangu kabisa olewake mtu aguse tairi yangu, yaani michelini hata mwezi haijamaliza.
Kabla sijapiga jerk gari yako nakusweka kwanza lupango ndio naendelea na kazi yangu
 
Relax mkuu,,utajipa vidonda vya tumbo bila ulazima.Tunachosema hapa ni kwamba wale wanaopita kwenye barabara za magari yaendayo haraka wanavunja sheria, wakamatwe wafikishwe mahakamani na si vinginevyo.

Jambo Jepesi tu la kuheshimu barabara ya mwendo kasi leo hii ikajaze mahakama zetu na bado tunaona Watanzania tuko sawa..!!!!
 
Hiyo ndo kazi ya mahakama, tukisema turuhusu kila mtu awe hakimu hii itakuwa jamii ya aina gani? Mbona wezi wa kuku, wapiga debe nk tunawapeleka mahakamani? Hata kama kosa ni dogo kiasi gani ni lazima uwepo utaratibu wa kisheria wa namna ya kulishughulikia.
 
Kwa hiyo RAIS anasapoti wizi wa matairi ya magari ya watakaokamatwa? Kweli you can take a bushman from the bush but can't take the bush out of him. Let's go.....

Huo ni mtazamo wako kwa maana umeamua kuangalia kutokea upande huo..... Wapi katamka "waibe"?!!! "Vichaa" saa ingine wanatakiwa waongozwe kiukichaa ....
 
Hiyo ndo kazi ya mahakama, tukisema turuhusu kila mtu awe hakimu hii itakuwa jamii ya aina gani? Mbona wezi wa kuku, wapiga debe nk tunawapeleka mahakamani? Hata kama kosa ni dogo kiasi gani ni lazima uwepo utaratibu wa kisheria wa namna ya kulishughulikia.
Ukiangalia idadi ya boda boda, biskeli, guta, waenda kwa miguu, taxi, daladala nk nk zinavyo tumia hizo barabara sidhani mahakama inaweza kushulikia hizo case zikafika huko... Hata waki simamisha case zingine zote.Tunahitaji by laws zitakazo pambana na huu "ukichaa" Papo kwa Papo na kwa njia ambayo muhusika hata akifikiria tu kupita hapo anasikia kutoka jasho.....
 
Mkuu nakubaliana na wewe kwamba zitungwe by laws kukabiliana na ulichokiita "ukichaa" hiyo ni sahihi kabisa,lakini ile ya kuchomoa tairi na kuuza siamini kama hata wewe ungependa uwe treated hivyo siku ukikutwa na kosa la usalama barabarani.
 
Kuna siku pale uwanja wa taifa, marehemu Mziray kocha wa zamani wa Taifa Stars alimkamata jamaa mmoja aliyekuwa amekojoa kwenye sinki wakati sehemu za watu kukojolea zikiwa hazina watu!!. Marehemu Mziray akawa anawaambia mashabiki waliokuwa wameingia chooni wakati wa mapumziko, kwamba yule jamaa hapaswi kuachiwa kwa namna yoyote ile. Na kweli polisi wakaja wakambeba mpumbavu yule na kwenda nae kituoni.

Kuna kipindi sisi wabongo akili zetu zinakuwa mbovu kupita maelezo. Tunahitaji rais wa aina hii ya JPM ambaye hachekei wapumbavu, wasiokuwa na uchungu na shilingi bilioni 388. Wakati mwingine tunakuwa ni taifa la kipuuzi sana ingawa kwa bahati mbaya huwa hatuna desturi ya kupenda kukubali hoja zinazotukosoa kwa nia ya kutubadilisha tabia.
 
Daaah sijui watanzania tunatakiwa tuongozwe kivip ila kuongea wananch wa Tanzania unahitaj kuwa Na kipaji binafsi big up sana Mr President magufuli mungu akusaidie
 
Ila kwa kweli hili hata mimi namuunga mkono mh. Raisi maana hawa jamaa wanauzi sana
Bora wewe umeliona kaka mkubwa, kuna watu humu JF mtu wa kwanza akianza kwa kuiponda post basi wengine wooote ni kuponda tu, hebu fikiria ni hela zetu zimetumika kutengeneza hizo barabara ili watu waende mbio makazini na kurudi mapema afu mtu anapitisha kikopo chake humo, kweli kamata afu piga change kota pin ukirudi watu wamelamba mpaka gear box wameweka ya zamani utajuuuuuuuuuuuuuuutraaaaaaaa
 
Kuna siku pale uwanja wa taifa, marehemu Mziray kocha wa zamani wa Taifa Stars alimkamata jamaa mmoja aliyekuwa amekojoa kwenye sinki wakati sehemu za watu kukojolea zikiwa hazina watu!!. Marehemu Mziray akawa anawaambia mashabiki waliokuwa wameingia chooni wakati wa mapumziko, kwamba yule jamaa hapaswi kuachiwa kwa namna yoyote ile. Na kweli polisi wakaja wakambeba mpumbavu yule na kwenda nae kituoni.

Kuna kipindi sisi wabongo akili zetu zinakuwa mbovu kupita maelezo. Tunahitaji rais wa aina hii ya JPM ambaye hachekei wapumbavu, wasiokuwa na uchungu na shilingi bilioni 388. Wakati mwingine tunakuwa ni taifa la kipuuzi sana ingawa kwa bahati mbaya huwa hatuna desturi ya kupenda kukubali hoja zinazotukosoa kwa nia ya kutubadilisha tabia.
No comment ndugu sio mambo ya TB Joshua sijui nani hapa, watu wakaziwe mwanzo mwisho nchi itabadilika tu.
 
Hacha upuuzi wako hapo ww kupitisha kimtumba chako ni sheria gani unafuata , vunja sheria naye avunje sheria za kukuadhibu ndio akili itawaingia , kiburi chàko ni sababu sheria ni dhaifu ndio maana mnazivunja unataka uharibu mali ya milioni ulipe elfu 10, shwaini !
Kimtumba gani?
 
Kumbu kumbu zangu zikiwa sawa.

Alianza Mohammed mpinga(mkuu traffik tz)kuonya wachepukaji.

Wiki moja iloyopita mh waziri mkuu akiwa na M.mpinga kwa mara nyingine naye akaonya vikali wavamizi wa barabara hizo za mwendo kasi. Siku mbili zilizofuata baada ya tamko ajari mbili zilizotukuka zinatokea kwenye barabara hizo.

Watanzania wakati wote huwa ni wabishi.
Two wrongs do not make a right.

Kama watu wanavunja sheria, dawa yake ni kuwarudisha kwenye mstari kwa kutumia sheria. Si kuvunja sheria ili watu warudi kwenye sheria, huko kutakuwa kujichanganya.

Rais kachaguliwa kuchochea na kutetea utawala wa sheria. Hajachaguliwa kuchochea kuvunja sheria.

Rais hatakiwi kutisha watu wafuate sheria kwa njia zisizofuata sheria. Huo utakuwa ujuha.
 
Kuna siku pale uwanja wa taifa, marehemu Mziray kocha wa zamani wa Taifa Stars alimkamata jamaa mmoja aliyekuwa amekojoa kwenye sinki wakati sehemu za watu kukojolea zikiwa hazina watu!!. Marehemu Mziray akawa anawaambia mashabiki waliokuwa wameingia chooni wakati wa mapumziko, kwamba yule jamaa hapaswi kuachiwa kwa namna yoyote ile. Na kweli polisi wakaja wakambeba mpumbavu yule na kwenda nae kituoni.

Kuna kipindi sisi wabongo akili zetu zinakuwa mbovu kupita maelezo. Tunahitaji rais wa aina hii ya JPM ambaye hachekei wapumbavu, wasiokuwa na uchungu na shilingi bilioni 388. Wakati mwingine tunakuwa ni taifa la kipuuzi sana ingawa kwa bahati mbaya huwa hatuna desturi ya kupenda kukubali hoja zinazotukosoa kwa nia ya kutubadilisha tabia.
Rais hatakiwi kutoa kauli za kutaka watu wafuate sheria kwa kuruhusu polisi wavunje sheria.

Anawachanganya watu hawajui kama anataka utawala wa sheria au hautaki.
 
Back
Top Bottom