Magufuli ukishindwa yote hayo 2020 gombea kupitia UKAWA

MSEZA MKULU

JF-Expert Member
Jul 22, 2011
3,763
5,591
Simuoni Magufuli ndani ya safari ya wanaCCM, chama kikongwe kinamemrundikia kiongozi huyu Mizigo mizito ambayo kama kweli wangekuwa na nia njema na taifa hili kuna mengine wakeshayatatua.

Katikati ya maamuzi magumu anayofanya bado jana anadai kuna waziri wake mmoja alitaka kutokubaliana nae hadi akampa option ya kuresign kama anaona hawezi. Katikati ya udhaifu wake (kwa mujibu wa wakosoaji wa utawala wake)naiona nia dhabiti ya kumsaidia maskini.

Nia hii imegubikwa na ukinzani mzito sio kutoka UKAWA bali nashawishika kuamini ni kwa wale walioifikisha hapa chini ya mwamvuli wa CCM na fans wao.

Mahakama ya Mafisadi kiukweli ni kama kuzungumzia kung'oa engine ya basi unalosafiria huku ukitegemea ufike unakokwenda.

Badili Basi ndio uamuzi wa busara. Jiunge na Chama kipya 2020, Kama UKAWA wanamakandokando Jiunge hata na CHAMA KIPYA ili upate platform nzuri ya kuifikia Tanzania unayoiona katika Maono yako.

Vinginevyo nitakuwa wa mwisho kuamini uwezekanaji wa nia yako na unayoyasema.
 
Nahisi kuwa hata huko unakomshauri aende, anaweza kukutana na mambulula wengi pengine katika kiwango sawa na hawa walio ndani ya CCM. Kwenye malezi yetu kuna mahali pana tatizo la msingi, ndio maana vituko haviishi nchini, na vipo ndani ya vyama vyote. Watu ni wale wale, iwe ndani ya CCM iwe nje ya CCM.
 
Back
Top Bottom