Magufuli udumu

rutoryo

Member
Nov 11, 2016
56
31
Mimi mwananchi wa musoma napongeza sana kwa hatua Kali ulizochukua kuindeleza hospitali ya kwangwa iliopo nje kidogo ya mji wa musoma,kwani tangia awamu ya mwl nyerere watu walipiga hela hospitali ikajengwa nusu tangia hapo ilibaki gofu kila mbuge aliekuja alikuja na mbwembwe nyingi kuwa atajenga akipata uongoz akuna utekelezaji,hivo kwa hatua ulizochukua kuwaweka TBA na jkt kujenga hiyo hospitali hakika nakuambia 2020 utanyakua kula zote mjini musoma kwani kilikuwa kisiki kikubwa kwa viongozi wote waliopita,
 
Ila nashauli pajengwe chuo kikubwa ndani ya hospitali cha mambo ya afya ili kuufungua mji wa musoma katika biashara kwani mji umezorota hauendelei viwanda vyote vilikwisha kufa mfano mutex maisha magumu, Leo hii mji wa musoma unazidiwa hata na singida nafikili hata manyara ya juzi itaupita mkoa huu,hivo juhudi binafsi Zinatakiwa kuchukuliwa kuuokoa mkoa huu uliodumaa kimaendeleo,Leo Serengeti inahesabika kuwa ya Arusha mapato yote yanaenda arusha hakuna hata hoteli moja ya utalii viongozi wetu tunaowachagua hawajengi hoja za msingi kuuendeleza mkoa huu,huu mkoa ulibalikiwa kutoa viongozi wakubwa kitaifa lakini hakuna hata mmoja anaeupigania wengi wao ubinafsi umewajaa kila mtu anajali maslahi ya wilaya yake inauma sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom