Magufuli tusaidie wahitimu UDSM tupate vyeti na transcript mapema

Magufuli tusaidie wahitimu UDSM tupate vyeti na transcript mapema

Bob Malik

Senior Member
Joined
Oct 1, 2019
Posts
125
Reaction score
419
Naandikaa huu uzi nikiwa na majonzi ya kurudi mkoani (Kigoma) kijijini kwetu bila cheti wala trascript. Nilikuja Dar ili nifanye clearance kisha nichukue cheti transcript pamoja na cheti.

Cha ajabu nimekamilisha process zote kulipia transcript na kufanya clearance. Naambiwa vyeti mpaka mwakani, basi nikawaambia naombeni hata transcript, wameniambia mpaka Ijumaa ijayo. Sasa mpaka hiyo Ijumaa nitakuwa nakula kwao au kulala kwao?

Kama chuo wameshindwa kuandaa transcript toka mwezi wa 7 mpaka sasa mwezi wa kumi na mbili wanategemea nini?

Mtaani hakuna ajira kabisa, ajira zilizopo zinahitaji angalau uwe na transcript au cheti na sio matokeo nusu.

Kama serikali imeshindwa kutupa ajira basi itype vyeti vyeti ili tuombe hata scholarship nje kwenye fursa ili angalau tuepukane na kukaa bila kutumia tulichokisoma.

Naamini watu mnaomsaidia Rais mmesikia.

Asante JF kwa kunipa uwanja japo niseme hili. Jumapili naenda kukata tiketi kurudi kwetu bila cheti wala transcript.
 
kwaiyo moja kwa moja umeona anaefaa kujibu tatizo lako ni namba 01. umeruka msusuru woooote wa wahusika paka kwa namba moja.

pamoja na kubahatika kupata elimi ya chuo kikuu bado hujaelewa kua we need stronger institutions and not expect a single person to solve all the country’s problems..

na wewe umekua miongoni mwa wale vijijini, the help-less, wanaosubiri wapate maji baada ya namba 01 kupata ziara huko na kumpigia simu katibu wa wizara ya maji, huku allocated budget ya maji ikiwa disbursed at shoe-number percent.

kweli kusoma si kuelimika!
 
Muda huohuo,wale wa UDOM wameondoka jumlajumla na vyeti vyao kwasababu ya kauli ya Rais.Kweli siasa ina nguvu sana.
Angalau tungekuwa na mshahara tungeweza kuhimili gharama za kuishi kwenye hili jiji. Sasa hata mahafali yenyewe hatujashiriki kwa sababu za uhaba wa pesa, tumeungaunga ili tupate nauli na tumefikiq kwa marafiki zetu ambao na wenyewe wanategemea boom kuishi. Halafu tunaamniwa transcript eti cjui mtandao unasumbua mpaka wiki lijalo.
 
cejo, Mkuu Mimi ninamaana yangu kumuomba Magufuli kama rais sijakurupuka.

Najua yeye mara nyingi akisema anasikilizwa kwa sababu ndie aliyewateua hao watu wa chuo nao wakateu na kuajiri wafanyqkazi wazembe.
 
Mkuu Mimi ninamaana yangu kumuomba Magufuli kama rais sijakurupuka.

Najua yeye mara nyingi akisema anasikilizwa kwa sababu ndie aliyewateua hao watu wa chuo nao wakateu na kuajiri wafanyqkazi wazembe.

mkuu una a very genuine concern, hujakurupuka hata kidogo ku raise concern yako.

ila namna unavyowaza kutatua tatizo lako basi umepotoka vibaya sana.. na kama “msomi” tena wa chuo “bora” kabisa Tanzania embu jitoe kweny hii aibu.

kwaiyo watu mil 55+ kila mmoja aanze kutafuta audience ya namba 01 katika matatizo yake.. amekua Mungu yeye!

na mtaani utapaona pagumu kweli ukija na attitude hiyo, badili namna unavyofikiri.
 
Rais ni taasisi mkuu. Rais sio mtu mmja. Utakuwa umenielewa vibaya baada ya kutumia neno Magufuli badala ya rais.
 
Punguza temper kijana cheti chako kipo tu as long as umefanya mitihani yako na kufaulu vizuri. UDSM ni chuo kikubwa, mambo yote yanafanyika kwa utaratibu. Kuwa na subira usiwe na papara hata wenzenu waliomaliza mwaka jana vyeti vyao walianza kuchukua mwaka huu mwezi wa pili
 
Hapan usisema hivyo vumilia uone wiki ijayo itakuaje .
Hongera yao. Naanza kuamini nililetwa jararani kweli.

Hakuna kujali kama wahitimu wengi no wa mikoani wengine hawana ndugu wala jamaa hapa jijini.
 
Hapan usisema hivyo vumilia uone wiki ijayo itakuaje .
Itakuwa ngumu mkuu...
Bajeti yqngu iliisha Jana...hizi siku tatu mpaka jpili najikongoja tu.
Hadi sasa nikekula had I nauli ya basi ntapanda treni ili kufidia.
 
Rais ni taasisi mkuu. Rais sio mtu mmja. Utakuwa umenielewa vibaya baada ya kutumia neno Magufuli badala ya rais.

ukishapata cheti, ukaomba kazi manispaa wakachelewa kukujibu uiombe tena taasisi ya Rais, mtaani kwenu kukiwa na vibaka wengi serikali ya mtaa ikachelewa kuwajibika uiombe tena taasisi ya Rais, ikitokea uka amua kufanya kilimo kigoma mbolea zikachelewa usisite kuiomba taasisi ifanye yake..

kila la kheri mkuu!
 
Back
Top Bottom