Magufuli, tupambane tuachane na kutegemea misaada!

Magufuli, tupambane tuachane na kutegemea misaada!

nachukia wala urojo wanapotuletea frustration zao wakifikiri tupo so much interested, si huwa wanatukataa hawa, mbona leo wanatutaka. tukienda kwao wanatuita "chogo", kama sisi machogo basi wao ni mabulula na watumwa wa waarabu.
 
Hapo ndipo utakapomjua Mzungu ni Nani, Nyerere alikoma kwa hao na akasema kabisa kuwa hata korosho wakiamua wanaweza kutupangia bei ya kuuza.

Tena aendelee kujifanya anakomaa uone katika kipindi kigumu kuwahi kutokea katika historian ya Tz itakuwa ni hiki cha Magufuli.

Nyie wengine mnajua kuandika mithamiati tu humu, Watz kwa uchumi tunawazidi Iran? Hebu jaribu kuiangalia Zimbabwe Leo ikoje? Ushauri mbovu sana huu.

Bandari wanaoleta Leo kesho wakipigwa mkwala washushe Mombasa je utakula nini? Na dhadabu yako ukiambiwa haikidhi kiwango? Acheni kasumba za kibantu.

Katika watu waliofilisika kimawazo we ni nambari one yani kwa jinsi ulivyoandika ni kana kwamba Tanzania kujitegemea ni crime.Ina maana Tanzania kama haitakiwi kuwa na ambition ya kutransform yani tuendelee kuishi kwa mazoea ya shida huku tukilalamokiana?
 
Miaka 52 tulishindwa nini? Ninachokiongea ni ukweli tuu Ndio unaokuingia. Na mm sikuambii Tz tuuninakwambia Africa bado sana.
 
Kati ya vitu vinavyoniuma moyo ni serikali yetu kutegemea misaada ya wazungu. hii MCCG ambayo tumenyimwa na wamarekan limeshakuwa gumzo, wazungu wanatumia kama fimbo kutuchapia, kipindi cha kikwete walizuia misaada na kuvuruga kabisa bajeti yetu. wakati wa bajeti waliahidi kutoa misaada, tukaweka ahadi zao kwenye bajeti, wakafika katikati wakasema hatutoi misaada tuliyoahidi. huu ni unyama wa hali ya juu. ndugu yangu magufuli naomba unisikilize:

1. kama tukibana mianya yote ya ubadhilifu, tutaweza kukusanya kodi ya kutosha kuendesha nchi.

2. bandari na TRA kuwekewe task force maalumu kuchunguza uchafu wote, na kuzuia uchafu wote ili tukusanye hela.

3. watu waanze kulipa kodi, machine za EFD zianze kutumika ipasavyo.

4. makontena 5000 tu yakipita na kulipa kodi ni hela nyingi sana, angalia hayo waliyotuibia akina masamaki, hela nyingi kumbe inaweza kupatikana kama tukiwa na ulinzi mzuri kuziba mianya ya ubadhilifu.

5. bandari ya dsm, reli ya tazara na ya kati ziboreshwe.

6. USIJIKOMBE KWA WAZUNGU, usijikombe kabisa kwa wamarekani na waingereza, ninachokushauri, angalia nani yupo pamoja na wewe then ambatana na huyo (kwa caution, usiende miguu yote), kwamfano; wachina na wajapan sasaivi wanaonekana hawajatutupa mkono sana, ambatana na hao, watembelee hata nchini kwao. marekani, uingereza na hao mabepari waliokata misaada, achana nao kabisa, waweke pembeni na uonyesha kuwa umewaweka pembeni. USIJIKOMBE, usiwalambe miguu, ukiwaweka pembeni, haitapita muda watarudi wenyewe wakijibembeleza kwako. angalia mwenzio kagame alipowaweka ufaransa pembeni, walijuta wafaransa hadi rais wao akaja rwanda. usihangaike na nchi ambayo haina faida kwa watanzania.

angalia kwamfano hao wa CANADA, na wamarekani ambao wanachimba migodini kwetu ACACIA na geita etc, wanachuma sana lakini hawatoi misaada mingi kwenye nchi zetu, wewe waweke pembeni na anza kuwashughulikia.

UKITAKA NCHI YETU IHESHIMIKE, wafanya hao wazungu wajue kuwa wakija kwetu hawaji kutusaidia tu, wao pia wanapata faida nyingi toka kwetu, hivyo kama hawatakuwa na adabu watashughulikiwa vilevile.

pia, kama wamagaribi wataleta nyodo, waonyeshe kujiunga na uchina, nenda ziarani uchina, wewe kama rais ziara sio siku zote kitu kibaya, mkwere alikuwa anatoka nje ya nchi mara nyingi lakini sio kwamba kwenda nchi za nje ni kitu kibaya moja kwa moja, unatakiwa kubalance, nenda kwenye zile safari za muhimu tu. nenda china, nenda japan. andaa safari yako ya china na japan, india usienda hawana faida kwetu na hawana historia hiyo.

usifikiri kukaa bila kusafiri unapata masifa kwa watanzania waone kama unatunza pesa, kwenda nje kidogo ni kutafuta madili vilevile. sasa ona, wazungu wamezuia msaada ambao ulikuwa unategemea ungesaidia kwenye umeme, ili kuwakomesha waonyeshe kwamba sio lazima sana tuwe marafiki za wazungu, hata wachina na wajapan tunaweza kushirikiana nao. wasalaam!

Porojo tupu umeandika, yaani wewe kweli ni mwehu kichwa chako ni hard-headed - Nchi kama Marekani ni nchi ambayo imeendelea kwa viwanda zaidi duniani na uchumi wake kukua kwa kasi ya ajabu lakini kwa taarifa yako Marekani haijaacha wala haitaacha kutegemea partners kwa misaada mbali mbali kwa njia yeyote ile ili kuendelea kukuza uchumi wao, Itakuja kuwa Tanzanian nchi ambayo duniani ni nchi ya pili ama ya tatu inayoongozwa kwa umasikini duniani?

Ni vyema Ungemshauri magufuli awe na moyo wa kuendeleza kuziba hiyo mianya rushwa lakini sio kumshauri eti Tanzania isitegemee misaada kutoka kwa wazungu kama unavyokejeli.

Nyinyi ndio wale wenye mawazo mgando zaidi duniani kwamba bora tule dongo lakini nchi hatutoi. wazungu kama wanleta misaada yao au heweleta basi ni basi hamujali kabisa maisha ya watu.

Huna tofauti na kiongozi mmoja wa Tanzania siku moja aliwaambia na kujaribu kuwaaminisha watanzania kwamba watu wasidanganwe maisha ya Ulaya na hapa Tanzania hayana tofauti yeyote watu wasidanganywe.
 
@Azusa str unapoints lakini fahamu kwamba sekta ya afya 3/4 inasaidiwa na wamarekani haswa uzazi,ukimwi,malaria etc. Hii kitu Pepfar,Tanroads kwenyewe kulikuwa na projects za MCC- Marekani, Clinton foundation,MDH
 
mawazo mgando sana watu wenye ushauri namna hii wakipewa nchi wanaweza kuiangamiza mara moja. Ivi ni nchi gani ulimwenguni itaishi bila kutegemea misaada kutoka nje hasa kwa Tanzania nchi ambayo ni maskini wa kutupwa? nadhani tupo nafasi pili kwa umaskini zaidi duniani.

Marekani hadi sasa bado haijaacha kutegemea partners katika kuboresha uchumi wake na haina mpango huo kabisa ambayo tunaweza kusema ni miongoni mwa nchi zilizoendelea na uchumi wake kukua kwa kasi ya ajabu sana duniani.

Tanzania saivi wananchi wake walio wengi ni shida ata kutengeneza mlo 1 kwa siku eti tutegemee uchumi wetu wa ndani bila misaada kutoka nje kuendesha nchi,

Nadhani hawa ndio washauri wabaya zaidi ambao 6 amesema wanamshauri Rais Magufuli vibaya bila kufanya tathmini na uchunguzi. Ukiona mtu analeta porojo kama hizi ujuwe tu amepata pahali ameshika ndani ya serikali yake yanamuendea hajali mtu mwengine au atakuwa mvuta bangi na mpiga ulevi.
 
Ni mjinga tu anayedhanitunapaswa kuwanyenyekea wazungu. Miafrika mingine mijinga. Inadhani bila wazungu, hatupo. Lazima tukomae.
 
mawazo mgando sana watu wenye ushauri namna hii wakipewa nchi wanaweza kuiangamiza mara moja. Ivi ni nchi gani ulimwenguni itaishi bila kutegemea misaada kutoka nje hasa kwa Tanzania nchi ambayo ni maskini wa kutupwa? nadhani tupo nafasi pili kwa umaskini zaidi duniani.

Marekani hadi sasa bado haijaacha kutegemea partners katika kuboresha uchumi wake na haina mpango huo kabisa ambayo tunaweza kusema ni miongoni mwa nchi zilizoendelea na uchumi wake kukua kwa kasi ya ajabu sana duniani.

Tanzania saivi wananchi wake walio wengi ni shida ata kutengeneza mlo 1 kwa siku eti tutegemee uchumi wetu wa ndani bila misaada kutoka nje kuendesha nchi,

Nadhani hawa ndio washauri wabaya zaidi ambao 6 amesema wanamshauri Rais Magufuli vibaya bila kufanya tathmini na uchunguzi. Ukiona mtu analeta porojo kama hizi ujuwe tu amepata pahali ameshika ndani ya serikali yake yanamuendea hajali mtu mwengine au atakuwa mvuta bangi na mpiga ulevi.
yaani akili kama hizi ndio tunatakiwa kupambana tuwapeleke shule. hata kama amemaliza degree anatakiwa asaidiwe arudi shule kwasababu ni bomb kubwa kwa taifa. yaani unaamini marekani wanahitaji msaada wa kifedha toka nchi nyingine?..nchi gani inawapa marekani msaada, ..ni msaada wenye conditons kama huo unaopewa wewe na wacheza bao wenzio?...ungelisema marekani inahitaji ushirikiano wa kibiashara na nchi nyingine ushirikiano ambao una usawa na kuheshimiana hapo sawa, ila hakuna nchi inatoa pesa ili marekani waongezee kwenye kibaba cha bajeti yao kama nchi yetu ilivyo. sasa unatakiwa kuelewa kwamba, kama tungekuwa na bajeti inayojitosheleza asilimia mia moja bila kupewa msaada kujazia toka kwa hao mabwana zako, tungekuwa na uhuru sana. tunapata shida kwasababu tunategemea misaada, wanaileta kwa masharti kiasi kwamba hata kuwafukuza huko mwadui, kahama na geita tunashindwa kwasababu wametushika masikio na madini yetu wanatuibia na hatuna usemi kwasababu wanajazia kibaba bajeti zetu. tukikusanya kodi vizuri, tutafika tu na kuna siku utakuja kuelewa hiki nilichokisema. pole sana ndugu.
 
Porojo tupu umeandika, yaani wewe kweli ni mwehu kichwa chako ni hard-headed - Nchi kama Marekani ni nchi ambayo imeendelea kwa viwanda zaidi duniani na uchumi wake kukua kwa kasi ya ajabu lakini kwa taarifa yako Marekani haijaacha wala haitaacha kutegemea partners kwa misaada mbali mbali kwa njia yeyote ile ili kuendelea kukuza uchumi wao, Itakuja kuwa Tanzanian nchi ambayo duniani ni nchi ya pili ama ya tatu inayoongozwa kwa umasikini duniani?

Ni vyema Ungemshauri magufuli awe na moyo wa kuendeleza kuziba hiyo mianya rushwa lakini sio kumshauri eti Tanzania isitegemee misaada kutoka kwa wazungu kama unavyokejeli.

Nyinyi ndio wale wenye mawazo mgando zaidi duniani kwamba bora tule dongo lakini nchi hatutoi. wazungu kama wanleta misaada yao au heweleta basi ni basi hamujali kabisa maisha ya watu.

Huna tofauti na kiongozi mmoja wa Tanzania siku moja aliwaambia na kujaribu kuwaaminisha watanzania kwamba watu wasidanganwe maisha ya Ulaya na hapa Tanzania hayana tofauti yeyote watu wasidanganywe.
lini obama alishatembeza bakuli kama tunavyofanya hapa, au haujaelewa nini unaongea? kuwa serious tafadhali.
 
@Azusa str unapoints lakini fahamu kwamba sekta ya afya 3/4 inasaidiwa na wamarekani haswa uzazi,ukimwi,malaria etc. Hii kitu Pepfar,Tanroads kwenyewe kulikuwa na projects za MCC- Marekani, Clinton foundation,MDH
usipoonyesha msimamo katika maisha, utakuwa mtumwa milele. tunahitaji kuwafahamisha kwamba, wakija kuleta misaada hapa na wao kuna kitu wanakipata toka kwetu. kama wakiamua kukata misaada basi waache wakate, ndio tutatafuta solution baada ya hapo, ila kuishi kwa kufungwa utumwani ati kwasababu wanatupatia misaada ndio watufanye watakavyo, sikubaliani nalo. angalia mwaka jana, wameahidi hela kibao kwenye bajeti yetu, tukaweka malengo, wamefika katikati wamesema hawatatoa hela na sisi tulishazipangilia, mtu kama huyo si anakufanya we mjinga?...ni utumwa ambao kama hatutajikomboa, tutaish hvihivi tu. tukusanye kodi, kila mtu alipe kodi, tufanye kazi kwa bidii, tuimarishe ulinzi na mshikamano ili tupate wawekezaji (kama wamagaribi wakikataa tuitwe wa china na wengine waje)....tutafika tu.
 
lini obama alishatembeza bakuli kama tunavyofanya hapa, au haujaelewa nini unaongea? kuwa serious tafadhali.

Ivi ni lini uchumi wa Tanzania umeboreka angalau kuikaribia Kenya sikwambii Merakani ili Tanzania ikome kutembeza bakuli la kuomba omba???

Wewe hujamsikia magufuli ndio kwanza ana mpango sasa wa kufufua viwanda Tanzania wakati wenzenu wanavyo viwanda kwa karne na hawajaacha kuomba? Alafu eti usitembeze bakuli la omba omba?? huo ubavu unao?? ivyo vijisent vyenu mulivyokusanya apo TRA ata walimu mumeshindwa kuwalipa mishahara, dawa hospital bado ni ndoto sikwambii ata barabara kilo mita 1 hamjajenga nk. unapata wapi kiburi cha kuwa usitembeze bakuli la omba omba. nyi si ndo munasema ccm daima vipi mtachoka kuomba omba?

Tafuta nchi yako ukae peke yako alafu usitembeze ilo bakuli uendeshe maisha yako na jamaa zako, huwezi kuongea pumba kwa kuwalenga watanzania wote.
 
yaani akili kama hizi ndio tunatakiwa kupambana tuwapeleke shule. hata kama amemaliza degree anatakiwa asaidiwe arudi shule kwasababu ni bomb kubwa kwa taifa. yaani unaamini marekani wanahitaji msaada wa kifedha toka nchi nyingine?..nchi gani inawapa marekani msaada, ..ni msaada wenye conditons kama huo unaopewa wewe na wacheza bao wenzio?...ungelisema marekani inahitaji ushirikiano wa kibiashara na nchi nyingine ushirikiano ambao una usawa na kuheshimiana hapo sawa, ila hakuna nchi inatoa pesa ili marekani waongezee kwenye kibaba cha bajeti yao kama nchi yetu ilivyo. sasa unatakiwa kuelewa kwamba, kama tungekuwa na bajeti inayojitosheleza asilimia mia moja bila kupewa msaada kujazia toka kwa hao mabwana zako, tungekuwa na uhuru sana. tunapata shida kwasababu tunategemea misaada, wanaileta kwa masharti kiasi kwamba hata kuwafukuza huko mwadui, kahama na geita tunashindwa kwasababu wametushika masikio na madini yetu wanatuibia na hatuna usemi kwasababu wanajazia kibaba bajeti zetu. tukikusanya kodi vizuri, tutafika tu na kuna siku utakuja kuelewa hiki nilichokisema. pole sana ndugu.

Hiyo bajeti inayojitosheleza utaitolea wapi nchi kama Tanzania? kule bungeni wakipitisha zile bajeti ndugu yangu yale ni makaratasi tu yanachapwa kwa computer lakini mfukoni hamna kitu.

Tanzania haijawai kufanya bajeti hata ndogo isikwame kutekelezeka kwa sababu hela hawana, kuna bajeti toke JK anaapishwa kuwa rais zimepangwa bungeni hadi leo hamuna kitu miaka 10 iliisha maisha bado watanzania wamezidi umasikini.

Unapoongelea omba omba usichukue mfano kwa nchi kama marekani kwa sababu Tanzania sio level yake level ya Tanzania ni kama Uganda na Zimbabwe., hata kama marekani haombi fedha taslim lakini ikibidi kutafuta patners kwa njia za kibiashara pia tunasema inategemea mashirikiano na nchi nyengine ni aina ya misaada pia ata hili bado unaendelea kubishana.

Nataka ni kwambie saivi Shilingi yenu imeporomoka kwenye masoko ya kifedha haijawai tokea tokea dunia iumbwe vipi utakosa kutembeza bakuli, wenzenu wanategeneza note Tz bado imerudi kwenye shilingi alafu kweli bado utakuwa na ujasiri wa kukwepa kuomba omba?? wewe hufahamu lakini Rais wako Magufuli anayajuwa haya.
 
Hakuna aja ya kushindana na wazungu hatuwezi kuwashinda cha muhimu ni kukaza tutengeneze pesa yetu wenyewe nyingi tu. Rais atatue kero za wananchi. Magufuli afocus kwenye kujenga nchi zaidi sio migogoro isiyo na tija. Akusanye mapato mengi ili bajeti zisikwame sababu misaada imesimama au imechelewa na zikija za misaada ndio wananchi tunachotaka sio ubabe. Maige yupo pale hakuna litaloharibika.
 
Back
Top Bottom