Magufuli, tupambane tuachane na kutegemea misaada!

Magufuli, tupambane tuachane na kutegemea misaada!

Hatuwezi kuishi kwa mihemko, eti tukiambiwa ukweli ndio tujitutumue. Ni kweli tunapaswa kujitegemea, lakini sababu za kunyimwa misaada nazo zina mashiko.

Kama watu wamewekwa tu ndani kwa kosa la kujumlisha matokeo, mlitaka hao wazungu wakae kimya? Juzi Japan imeipa msaada India, ina maana tumewaacha nyuma India au?

Wakati mnajinasibu hapa na makusanyo ya bandari, mkumbuke kuwa huyo mnayemwambia akaze kamba akiumwa utamwona MBIO, yuko huko kutibiwa, hatotibiwa na Kigwangala.

Tujitegemee, lakini tuache na unafiki. Zanzibar ni AGENDA isiyopaswa kufumbiwa macho. Hizi shamra shamra za kutumbua majipu hazitoshi kuifikisha nchi tunapotaka, unless kama nia yetu ni kucheka cheka wkt wa taarifa ya habari kwa waziri kufanya kazi ya kufunga mageti.

Hahahahah!!!!! Wabongo kweli minyoo. Umewambia ukweli mchungu.
 
Misaada wanayotupatia ukiifuatilia 50% inarudi kwao inakua na masharti kibao. Zamani nilikua najua kua wakitupa msaada wa billion 300 katika afya nilidhani labda tunaletewa fedha inakuwepo pale hazina LA hasha, kumbe wanaleta mradi wa ukimwi ambapo ndani ya fedha hiyo kuna gharama za kununua nagari, administration cost ambapo utakuta shirika linaloendesha huo mradi lina ofisi mpaka marekani na staff wa kule wanalipwa hela hiyo hiyo, pia kuna staff wakimarekani wataajiriwa Tanzania senior position watalipwa USD 20,000 kwa mwezi kutoka katika hela hiyo hiyo. Bado procurement mtafuata Sera zao ambapo kuna vifaa mtaambiwa lazima vinunuliwe marekani na gharama kibao tu zinarudi kwao. Tukusanye mapato tubane matumizi tutasurvive tu na Mungu yupo pamoja nasi
 
Msaada wanaturingia nao nisawa na kila Mtanzania akitoka 19000 tu, sisi wenyewe tu nauwezo wakuchangia maendeleo kama tukiweka utaratibu mzuri, hakuna sababu kuomba omba tunachangia harusi kwanini tusifunge mkanda ifunguliwe akaunti ya maendeleo watanzania wengi watachangia naiwe chini ya ofisi ya rais uwezo tunao, kupanga ni kuchangua
 
Azusha
Mbona unajijibu mwenyewe, hayo uliyoandika ndiyo wazungu wanataka ufanye usifuje Mali. Kama Kikwete du Magufuli angefanya uliyotajs hapo juu Tanzania ingeua ndege wawili kwa jiwe Moja. Yaani ungezipata za hapa na za wazungu.

Wazungu nao wanatunza kwanza ndiyo wanatupa sisi kidogo nao wanao watu maskini kwa nini wakupe wewe ufuje?
 
Kati ya vitu vinavyoniuma moyo ni serikali yetu kutegemea misaada ya wazungu. hii MCCG ambayo tumenyimwa na wamarekan limeshakuwa gumzo, wazungu wanatumia kama fimbo kutuchapia, kipindi cha kikwete walizuia misaada na kuvuruga kabisa bajeti yetu. wakati wa bajeti waliahidi kutoa misaada, tukaweka ahadi zao kwenye bajeti, wakafika katikati wakasema hatutoi misaada tuliyoahidi. huu ni unyama wa hali ya juu. ndugu yangu magufuli naomba unisikilize:

1. kama tukibana mianya yote ya ubadhilifu, tutaweza kukusanya kodi ya kutosha kuendesha nchi.

2. bandari na TRA kuwekewe task force maalumu kuchunguza uchafu wote, na kuzuia uchafu wote ili tukusanye hela.

3. watu waanze kulipa kodi, machine za EFD zianze kutumika ipasavyo.

4. makontena 5000 tu yakipita na kulipa kodi ni hela nyingi sana, angalia hayo waliyotuibia akina masamaki, hela nyingi kumbe inaweza kupatikana kama tukiwa na ulinzi mzuri kuziba mianya ya ubadhilifu.

5. bandari ya dsm, reli ya tazara na ya kati ziboreshwe.

6. USIJIKOMBE KWA WAZUNGU, usijikombe kabisa kwa wamarekani na waingereza, ninachokushauri, angalia nani yupo pamoja na wewe then ambatana na huyo (kwa caution, usiende miguu yote), kwamfano; wachina na wajapan sasaivi wanaonekana hawajatutupa mkono sana, ambatana na hao, watembelee hata nchini kwao. marekani, uingereza na hao mabepari waliokata misaada, achana nao kabisa, waweke pembeni na uonyesha kuwa umewaweka pembeni. USIJIKOMBE, usiwalambe miguu, ukiwaweka pembeni, haitapita muda watarudi wenyewe wakijibembeleza kwako. angalia mwenzio kagame alipowaweka ufaransa pembeni, walijuta wafaransa hadi rais wao akaja rwanda. usihangaike na nchi ambayo haina faida kwa watanzania.

angalia kwamfano hao wa CANADA, na wamarekani ambao wanachimba migodini kwetu ACACIA na geita etc, wanachuma sana lakini hawatoi misaada mingi kwenye nchi zetu, wewe waweke pembeni na anza kuwashughulikia.

UKITAKA NCHI YETU IHESHIMIKE, wafanya hao wazungu wajue kuwa wakija kwetu hawaji kutusaidia tu, wao pia wanapata faida nyingi toka kwetu, hivyo kama hawatakuwa na adabu watashughulikiwa vilevile.

pia, kama wamagaribi wataleta nyodo, waonyeshe kujiunga na uchina, nenda ziarani uchina, wewe kama rais ziara sio siku zote kitu kibaya, mkwere alikuwa anatoka nje ya nchi mara nyingi lakini sio kwamba kwenda nchi za nje ni kitu kibaya moja kwa moja, unatakiwa kubalance, nenda kwenye zile safari za muhimu tu. nenda china, nenda japan. andaa safari yako ya china na japan, india usienda hawana faida kwetu na hawana historia hiyo.

usifikiri kukaa bila kusafiri unapata masifa kwa watanzania waone kama unatunza pesa, kwenda nje kidogo ni kutafuta madili vilevile. sasa ona, wazungu wamezuia msaada ambao ulikuwa unategemea ungesaidia kwenye umeme, ili kuwakomesha waonyeshe kwamba sio lazima sana tuwe marafiki za wazungu, hata wachina na wajapan tunaweza kushirikiana nao. wasalaam!

Katika harakati za kuongeza mapato serikali iunde chombo cha kuweka malengo ya ukusanyaji mapato kwa taasisi zote zinazokusanya mapato (tax and non tax revenue). Utaratibu huu utaachana na taasisi kujiwekea malengo, kujipima na kuvuka malengo yao. Chombo hiki kiwe chini ya ofisi ya Rais. Kazi hii ingefanywa na BRN Bureau lakini sina imani nayo. Malengo yake huwa ya kisiasa zaidi. Walengwa wakuu wawe pamoja na TRA, TPA, TANAPA, NCCA, TFS, Migodi ya madini nk. Chombo hiki pia kiwe na majukumu ya ufutiliaji na tathimini ya malengo. Tanzania inauwezo wa kuandaa bajeti ambayo 100% ya mapato yatokanayo na vyanzo vyake vya ndani. Tupunguze au tuachane na uandaaji wa bajeti tegemezi kutoka kwa Uncle Sam na wadogo zake. Tuangaze zaidi mashariki. Miaka ya mwanzo itakuwa migumu lakini tutavuka na kujenga utu wetu
 
Kifuu kabisa
Uko tayari demokrasia yetu ikanyagwe huku ukipewa pipi ule kama mtoto mdogo alie pata kichapo kwa mzazi wake.
Tukatae misaada yako kwa hoja nyengine lakini sio hii ya kukanyaga demokrasia ya wananchi.
 
umesema ukweli kabisa. msaada wanaotupatia wazungu, ni sawa na hela ambayo tunaweza kukusanya kwa mwezi mmoja tu hapa Tanzania. na kama tukibana mianya ya rushwa na ubadhilifu, tukawanyonga mafisadi, tunaweza kukusanya hata mara mbili yake na misaada yao tukaikataa. heshima yetu itabaki.

We kichwa chako kimejaa utomvu kabisa mkuu.

Hio hela unayo ona wewe sio hela kwa nchi kama Tanzania yenye population 45 milioni.

Pili umesahahu deni la taifa.
 
Hivi kwani hatuwezi kupanga bajeti kwa mapato yetu tu? tusitegemee misaad mhe Rais
Endelea kukata matumizi yasiyoyalazima mfano kata hizo posho za wabunge na mikopo ya magari usiwape tusonge mbele
 
Hivi kwani hatuwezi kupanga bajeti kwa mapato yetu tu? tusitegemee misaad mhe Rais
Endelea kukata matumizi yasiyoyalazima mfano kata hizo posho za wabunge na mikopo ya magari usiwape tusonge mbele

we hushangai kwa nini tunajenga barabara za 2 lanes karne hii ....
we think small and we will remain small 4 life

watu hawana confidence kabisa na mipango ya nchi
 
Mahesabu kidogo Tu 1.3T makusanyo ya mwezi * 12 miezi ya mwaka = 15.6T. Bajeti ya mwisho ilikuwa 22T Bila elimu bule. Na hizo ni midafu hatuwezi agizia mafuta, dawa. Pia msahada wenyewe mashariti yake ndo hayo nchi yako iwe ya kidemokrasia. Pia jua atuna export yoyote ya kutuingizia $ nyingi ili tuimport mahitaji yetu. Hata kama tukikusanya 50T kwa mwezi madafu yetu, atuwezi nunulia dawa hata hapo kenya.
 
We kichwa chako kimejaa utomvu kabisa mkuu.

Hio hela unayo ona wewe sio hela kwa nchi kama Tanzania yenye population 45 milioni.

Pili umesahahu deni la taifa.
acha kujadili mambo ya nchi ya watu wewe, ninajua ninyi hamfurahii mafanikio tunayoyapata katika nchi yetu, wakati nchi yenu imejaa magaidi, mashoga na wauza unga. uchaguzi wenu hautuhusu, shughulikieni uchaguzi wenu, msituonee wivu. sisi hapa kazi tu, na mtaisoma namba. si mlitaka kusepa ninyi, ati mjiunge na watu wengine, achaneni na sisi, endeleeni kushangaa wazungu wanaokuja kuwashikisha ukuta huko, sisi wenzenu huku bongo hapa kazi tuuuuu.
 
Kifuu kabisa
Uko tayari demokrasia yetu ikanyagwe huku ukipewa pipi ule kama mtoto mdogo alie pata kichapo kwa mzazi wake.
Tukatae misaada yako kwa hoja nyengine lakini sio hii ya kukanyaga demokrasia ya wananchi.
sisi wenzenu tulishayamaliza hayo kitambo sana, ninyi ndio mnahangaika sasa. wakati sisi wenzenu tunatafuta maendeleo, ninyi bado mko kwenye siasa maji taka. usijefikiri sisi wengine huku tuko so much concerned about you.....tulishawafuta kichwani kitambo sana.
 
Katika harakati za kuongeza mapato serikali iunde chombo cha kuweka malengo ya ukusanyaji mapato kwa taasisi zote zinazokusanya mapato (tax and non tax revenue). Utaratibu huu utaachana na taasisi kujiwekea malengo, kujipima na kuvuka malengo yao. Chombo hiki kiwe chini ya ofisi ya Rais. Kazi hii ingefanywa na BRN Bureau lakini sina imani nayo. Malengo yake huwa ya kisiasa zaidi. Walengwa wakuu wawe pamoja na TRA, TPA, TANAPA, NCCA, TFS, Migodi ya madini nk. Chombo hiki pia kiwe na majukumu ya ufutiliaji na tathimini ya malengo. Tanzania inauwezo wa kuandaa bajeti ambayo 100% ya mapato yatokanayo na vyanzo vyake vya ndani. Tupunguze au tuachane na uandaaji wa bajeti tegemezi kutoka kwa Uncle Sam na wadogo zake. Tuangaze zaidi mashariki. Miaka ya mwanzo itakuwa migumu lakini tutavuka na kujenga utu wetu
umeongea jambo la maana sana. kweli kuna watu wana uchungu na nchi yetu. i hope magufuli atapitia huu ushauri wako.
 
Mahesabu kidogo Tu 1.3T makusanyo ya mwezi * 12 miezi ya mwaka = 15.6T. Bajeti ya mwisho ilikuwa 22T Bila elimu bule. Na hizo ni midafu hatuwezi agizia mafuta, dawa. Pia msahada wenyewe mashariti yake ndo hayo nchi yako iwe ya kidemokrasia. Pia jua atuna export yoyote ya kutuingizia $ nyingi ili tuimport mahitaji yetu. Hata kama tukikusanya 50T kwa mwezi madafu yetu, atuwezi nunulia dawa hata hapo kenya.
mkuu, najua wewe hauna akili na inawezekana bado upo kwenye mihemuko ya uchaguzi na siasa za maji taka. kwa taarifa yako, hizo 1.3 trillion ambazo wanakusanya kwa mwezi, ni makusanyo yaliyopatikana bila mianya ya rushwa kubanwa, na bila matumizi sahihi ya EFD machines, na asilimia 50% ya wafanyabiashara Tanzania, hawalipi kodi ipasavyo. kama tukibana mianya vizuri, kodi ikalipwa na kila mtu, asiye lipa kodi akapelekwa mahakamani kwa tax aversion, nakuhakikishia makusanyo kwa mwaka yanaweza kufika hata 40 trillion.

watu wenye akili kama za kwako ni matomaso, hawawezi kuamini vitu hadi waone vimetokea. akitokea mtu anayethubuti akafanya vitu vya maana, ndio tunaona matunda. unajua kuwa makusanyo yamekuwa yakienda kwa balance hiyo hiyo bila kupishana sana kwa miaka kama miwili iliyopita, na hapohapo kuna makontena kama alfu tatu yamepita bila kulipiewa ndani ya miezi michache tu, na billion zaidi ya 500b kupotea. hizo ni container na kodi zilizogunduliwa. maduka mengi hayalipi kodi, viwanda havilipi kodi ipasavyo, watu wanalipa kodi ya nadharia tu....akiwa anatakiwa kulipa milioni 500ml kama kodi, anaongea na TRA analipa miliion 100 au 50, zingine anawatip tu hao jamaa. maduka yanakwepa sana kodi, importers na exporters wanakwepa sana kodi, uchimbaji madini huko ndio usiseme. sasa kwa akili ya mtu kama wewe, ukipewa urais si ndio tutarudi umasikini kabisa. jipime.
 
Hapo ndipo utakapomjua Mzungu ni Nani, Nyerere alikoma kwa hao na akasema kabisa kuwa hata korosho wakiamua wanaweza kutupangia bei ya kuuza.

Tena aendelee kujifanya anakomaa uone katika kipindi kigumu kuwahi kutokea katika historian ya Tz itakuwa ni hiki cha Magufuli.

Nyie wengine mnajua kuandika mithamiati tu humu, Watz kwa uchumi tunawazidi Iran? Hebu jaribu kuiangalia Zimbabwe Leo ikoje? Ushauri mbovu sana huu.

Bandari wanaoleta Leo kesho wakipigwa mkwala washushe Mombasa je utakula nini? Na dhadabu yako ukiambiwa haikidhi kiwango? Acheni kasumba za kibantu.

Well said! Kuna watu wanafikiri ukiwa na bandari na madini eti unaweza komaa ukajitegemea. Hao wazungu tunawategemea kwa kila kitu sio utakwepea wapi. Kama ni utalii wao ndiyo wanachangia kuliko sisi. Tukisema tulime mazao ya biashara tutamuuzia nani kama si wao? Na wenyewe ndiyo wanapanga wanunue au wasinunue. Sababu kubwa ya Viwanda vingi kufa ni kutokana na bidhaa zetu kuonekana ni duni au hazifai huko soko la dunia.
 
Zanzibar walijengewa line mpya ya Cable ya umeme kwa fedha hizi.bila ya msaada huu leo wangekua giza. Sio muungano wala ccm wangeweza kuwasaidia.
Tanzania bara awamu ya kwanza ya umeme vijijini imeanza kwa msaada wa MCC.

MCC ni fedha za walipa kodi wa Marekani na masharti yake ni mazuri na yanalinda maslahi ya watu wa nchi inazo kusudiwa...

Masharti hayo ni pamoja na

Utawala bora

Democrasia

Haki za binadamu

Kupiga vita ufisadi na rushwa.

Haya masharti ni mazuri na kwa maslahi ya raia ....haya ni machungu kwa watawala wetu...

Suala la cybercrime ni muhimu na kwa faida ya watanzania...sheria hio hata marekani ipo lakini wao wan itumia kwa ajili ya mijizi ya mitandao na usalama . Hawaitumii kwa ajili ya kukomoana kisiasa baina ya vyama vyao. Hapa kwetu inatumika zaidi kisiasa kunyamazishana na ilipitishwa kipindi cha uchagui Ni sheria nzuri lakini yenye malengo ya kisiasa zaidi. Hivyo sharti hili la MCC ni kwa ajili ya faida yetu kama raia ni sharti zuri watawala walitimize.

Sharti la pili la Zanzibar....hili ni sharti muhimu na kwa faida ya Watanzania kuona democrasia haichezewi. Watu wanzanzibar wameamua kuiweka Ccm benchi na tupo katika mfumo wa vyama vingi ikubali masharti ya kikatiba .

Uchaguzi umefanyika na Ccm imeshindwa na haitaki kuachia , hivyo sharti hili la MCC ni kwa manufaa ya Nchi yetu kwa ujumla na njia ya kutusaidia kuona ccm wanakubali mfumo wa vyama vingi kama njia bora ya utwala ili kuleta maendeleo ...shinikizo hili ni kwa ajili ya watanzania ..ni shinikizo chungu kwa ccm...wao hawapendi kuyatekeleza masharti hayo si kwa maslahi mapana ya nchi bali wanayakataa kwa maslahi ya kichama..wanaweka maslahi ya chama mbele kuliko ya nchi .

MCC wako sahihi na kwa ajili ya Watanzania ....na masharti yao ni kwa manufaa ya watanzania...wanao kataa kuyatekeleza wameweka maslahi ya chama mbele.

Ama kuhusu kujitegemea hilo suala zuri. Hioi linapaswa kutekelezwa kwa kuamini kuwa multiparty politics ni policy nzuri kuifikisha nchi mbele kimaendeleo na kujitegema. Hesabu za makontena zinakuja ikiwa hizo kontena zenyewe zinafika hapo bandarini kama haziji hesabu zako ni zero. MUgabe alijaribu kutaka kujitegemea lakini kwa kuviminya vyama vya wapinzania na kuiba uchaguzi hatimae ameimaliza Zimbabwe mpaka kununua mkate pesa ubebe na kontena!!!

Masharti haya ya MCC ni ya msingi kabisa na wala haya husiani na ukoloni mambo leo au utegemezi . Ni masharti yanayo linda haki za msingi wa raia wa nchi hizi za kiafrika ambazo zina matatizo sana ya utawala bora. Sote tunaona Burundi, COngo ,Rwanda viongozi vinganganizi wanavosababisha mauaji kwa raia wao...Wazungu wana matatizo yao lakini huwezi kusikia serikali zao kuua raia zao hovyo...raia zao ni dhahabu wanapenda na sisi tuwe mfano wa kwao...ndio haya masharti
 
Mh.magufuli nikuombe ukomae nao hili la wapiga dili na wahujumu uchumi waisome namba kwanza ni kundi dogo ambao wanaishi matawi tuliyo wengi ni maharage na mchicha kwa mbele kata mifereji yote na ndiyo mana wanazoza sana humu ndani jf
 
Well said! Kuna watu wanafikiri ukiwa na bandari na madini eti unaweza komaa ukajitegemea. Hao wazungu tunawategemea kwa kila kitu sio utakwepea wapi. Kama ni utalii wao ndiyo wanachangia kuliko sisi. Tukisema tulime mazao ya biashara tutamuuzia nani kama si wao? Na wenyewe ndiyo wanapanga wanunue au wasinunue. Sababu kubwa ya Viwanda vingi kufa ni kutokana na bidhaa zetu kuonekana ni duni au hazifai huko soko la dunia.
yaani tukiwa na watu wenye akili kama zakwako hapa tz, tunaweza kurudi enzi za ujima. kwa akili yako unaamini kuwa hatuwezi kuwakwepa wazungu? hiyo dhahabu ya kahama wakileta za kuleta tukachimba sisi wenyewe au tukaingia ubia na kampuni za china au india hata russia, unafikiri tutakosa sehemu ya kuuza dhahabu? unaijua dhahabu wewe, ukiwa nayo hautakosa soko la kuuza. kuhusu kilimo, tutauza hapahapa africa, au tutaenda asia. una elimu gani mkuu?
 
Bado mkuu vunja muungano,

Back
Top Bottom