Amesema ametenga kila kijiji Tanzania kupata milioni 50. Sasa utendaji ndo umeanza watch out
a dharurahizo milioni 50 kila kijiji ni kwaajili ya nini? au atawagawia wananchi kila mmoja elfu kumi kumi kama kijiji kina watu 5000? , mbona mipango ya hawa CCM haieleweki?
Turudi kwenye mipango ya CCM kama chama, Kilimo kwanza kipo wapi? Mabilioni ya JK yako wapi? maabara ziko wapi? MATOKEO MAKUBWA SASA! MKUKUTA!! MKURABITA!!! yaani maneno lukuki
matokeo yako wapi? shilingi inashuka, umeme shida, shule watoto hawana vyoo hawana madawati, hospitali shida.. matatizo kila kona..
CCM imefilisika kifikra.
Duh!!!!!
Nani alimwambia kumwaga hela kunaleta maendeleo?
Kiuchumi, ukiongeza hela kwenye mzunguko kuna madhara hasi kuliko magufuli anavyo dhani,kwani bei zitapanda na thamani ya fedha inapungua.
Afterall,mil 50 kwa kijiji mbona ni fedha kidogo sana??????
Huo ni mwendelezo wa ukurupukaji wa viongozi wa ccm baada ya kuanza kuonja machungu ya ukawa
Hii ni rushwa kwa wapiga kura. Hizo hela zilikuwa wapi miaka yote na zitatumika kwa kazi gani? He atatoa taslimu au kwa installment na kwa muda gani. Kama kuna hela nyingi hivyo mbona waalimu bado wanadai hela zao, mbona watu wengi waliobomolewa kupisha miundombinu mbalimbali hawajalipwa, mbona wanatuongezea Tshs 100 kwa kila lita ya petrol kugharamia REA. Kama hizo hela zipo zingeelekezwa kwenye miradi yenye tija kuliko kuwahadaa watanzania kupata kura. Watanzania tusikubali kuuziwa mbuzi kwenye gunia kama kweli kuna hela na zitolewe kabla ya uchaguzi na zitolewe cash na siyo ahadi wala kusainishwa makaratasi.[/QUOT
inaanzishwa saccos ya kijiji so wananchi
wanakopa kwa mashariti nafuu na kwa wepesi
ivo kuongeza mzunguko wapesa vijijin as result
boost economy
Dah..ulivyoshupalia mods abadilishe 10m kuwa 50m..hivi hujielewi kuwa unajiaibisha?..kijiji kimoja kina wakaazi wangapi na hizo pesa zitagawanywa au itakuwaje? Walikuwa wapi miaka yote..ni hongo au...kama sera zake ndo hizo amejua ashashindwa mapema sana..wananchi wa sasa sio wale wa miaka ya nyuma!
Kuna walimu hata simu hawawezi kutumia huko vijiji hizo laptop itakuwaje??? Ok mwalimu anaye fundisha darasa la kwanza laptop kwake ya nn??
Na laptop kila mwalimu nchi nzima! Yaani nimecheka kidogo nife. Kujenga maabara walikuwa wanafukuzana na mbuzi na kuku wa masikini wawang'anye na kuuza ili wapate michango huko vijijini leo wana hela za kugawa vijijini hivyohivyo?
Waalimu hata fedha za likizo wanashindwa kuwalipa miaka yote leo wawanunulie Laptop wote?
Ama kweli sasa uchizi umeingia chama tawala na wanaropoka wakidhani watu ni mazoba.
mkuu km umefatilia documentary ya magufuli ameshikanafasi chache za chama about 15 years amekua mtendaji na kaxi zake zinajieleza actions speak louder than words.
Wakiwa na nia wanaweza kwani zipo za kila bei, hata laki 2,3,4
Amesema ametenga kila kijiji Tanzania kupata milioni 50. Sasa utendaji ndo umeanza watch out