Dr.Magufuli ni mdogo mno, CCM ni mbuyu mkubwa huku Magufuli akiwa ni mchicha tu chini ya mbuyu huo.
Dr.Magufuli atuhakikishie namna atakavyomtaifisha nyumba zake Nkapa, Nsekwa, Marechela, siksi, mangura na wenginewe. Nyumba ambazo mafisadi waliuziana kwa bei ya tofari mia tano.
Aidha,asema kabisa kungali kweupe atakavyo tulejeshea aridhi ya Loliondo. Watangulizi wake hatujawahi wasikia wakiongelea hilo.si yule wa tatu wala wa tano.
Atuambie namna atakavyoiwajibisha Stanbic Bank kulipa fidia ya kukiuka sheria za fedha kwa kutoa mamilion ya dola zetu kwa singha singha. Zile dola tunazokatwa kila tununuapo umeme.
WASI WASI WETU: Dr.hawezi kuibadilisha CCM.