Magufuli Si lolote si chochote kwa Mfumo wa CCM

1954tanu

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
1,038
487
Tumechoshwa na mtindo wa kubadilishiwa majina mazuri na sura za ki-handsame,watanzania tunahitaji badiliko la kimfumo,historia ya mgombea yawezakuwa ya kuvutia na kupendeza lakini tatizo ni historia mbaya ya mfumo uliopo.

'CCM ni gari bovu,ambalo linahitaji kuondolewa barabarani si kulibadilishia dereva mpya, litaendea kuuwa watu kwa ubovu wake.'

Tatizo ni system,Magufuli hawezi kufuta historia mbaya ya taasisi ya chama cha mapinduzi,wezi wote wa mali za umma ndio wale wanaompigia debe achaguliwe kuwa Rais, nini kipo nyuma ya pazia???.Hata wenzake waliingia wakiwa wasafi na bila scandal lakini sasa ni dhahiri tumejua kuwa kwamba tatizo ni mfumo.

Mnaweza msinielewe.mfano wanampigia chapuo magufuli ndio hao ambao wanakashfa za Richmond,EPA,KAGODA,MELEMETA NA ESCROW ya hivi majuzi,usafi wa Huyu bwana huko wapi,ni kwa bahati tu hakupata fursa ya kushirikishwa kwenye ma-deals.

Ufisadi huu ulifanyika kwenye mfumo wa chama chake na yeye alikuwa Mbunge tangu mwaka 1995 na kuwa waziri kamili mpaka sasa,hakuwai kusikika akikemea ufisadi au kuwakemea wezi wa ndani ya mfumo wake.usafi wake uko wapi?.magufuli kama ni msafi atangaze wazi kuwafunga wale waliotajwa kwenye (11LIST OF SHAME).hawezi na hapo ndipo utajua tunaliwa kekundu.tatizo ni mfumo.

Urais ni taasisi si MTU.tunahitaji badiliko la mfumo si majina mazuri wala sura nzuri,WATANZANIA TUNATAKA MABADILIKO NJE YA MFUMO MBOVU WA CHAMA CHA MAPINDUZI.

Watanzania wasitegemee wala wasitarajie mazuri yoyote toka kwa Magufuli.Mfumo ulioundwa na kujengwa na CCM hauwezi kupinduliwa wala kubadilishwa na Magufuli. Mh. Pinda aliwahi bainisha kwamba ni vigumu kuwashughulikia mafisadi, eti nchi itayumba.

Magufuli naye anatoka kwenye kundi ilo hilo, hawezi fanya lolote. CCM ni mfumo wa kimaslahi, kadharika Magufuli ana maslahi yake ndani ya mfumo huo.

Watu wamwekeao matarajio Magufuli wamesahau kwamba walifanya vivo hivyo kwa J.Kikwete, lakini leo yako wapi! Kikwete alipoapishwa tu alianza kwa kishindo, mara kazuka ghafla Muhimbili, mara ghafla bin vuu kaibukia bandari.

Mizuko na ziara za ukaguzi wa kushitukiza zilileta matumaini, watanzania wakasema sasa tumempata rais. Kumbe upande wa pili, mfumo ndani ya CCM unamcheki na kumpima. Punde watanzania wakaona mambo yanatulia. Mbwembwe za JK zikafa.

Kuna fununu kwamba mfumo wa mafisadi ndani ya CCM ulianza kujengwa tangu enzi za Mwalimu. Marehemu Sokoine alipojaribu kuufuta mfumo huo akafutwa yeye kwanza. Familia ya Sokoine wamekuwa siku zote wakisihi mabaki ya baba yao yachunguzwe ili kubaini kifo cha baba yao. Hili limeshindikana. Wanauomba mfumo kuchunguza kilichofanywa na mfumo huo. Abadani haiwezekani.

Aidha, kwa fununu izo hizo, inasemekana mfumo uliharakisha kifo cha Mwalimu. Fununu hizi zilikazwa zaidi wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo huko Arumeru. Mh. V. Nyerere aliweka bayana mazingira ya kifo cha baba yao kuwa yana dalili ya mkono wa mtu.

Kauli za Mh. V. Nyerere hazikukanushwa na yeyote iwe ndani ya serikali ama familia ya mwalimu. Hata kifo cha Kolimba inasemekana kilipangwa na mfumo huo.

Kwa ufupi, watazania wasisahau jinsi walivyoanza na JK enzi zile za miaka ya 2005; ndivyo itakavyo kuwa hata kwa Magufuli iwapo atachaguliwa kuwa rais wa TZ. Kwa jumla, Mh. Magufuli ni mwepesi mno kuliko mfumo uliomweka hapo alipo.

Hakika hakutakuwa na mapya, mfumo umemweka hapo ili kulinda nyumba za umma walizouziana na kulinda mikataba mbali mbali waliosainiana na wawekezaji mbalimbali wa madini, gesi na mafuta.

WATANZANIA MMEUMIA!

1. Mfumo unaotakiwa kwa Tanzania mpya (kuanzia 2015) ni wa serikali kuwajibika kwa wananchi (kupunguza madaraka mengi ya rais na viongozi wengine wa serikali na wabunge kama ilivyo kwenye rasimu ya pili ya katiba) - Rasimu ya Warioba.

2. Mfumo wa sasa ni wa 'wananchi kuwajibika kwa serikali' (madaraka makubwa ya rais na wabunge na viongozi wengine wakishachaguliwa kutoka madarakani ni kwa kupenda kwao na si kwa matakwa ya wananchi). Rasimu ya pili iliweka wazi kwamba mbunge asiyetimiza wajibu wake aweze kuwajibishwa na wananchi. Kulitakiwa tu kuweka utaratibu mzuri wa kumwajibisha mbunge na ubunge hata kama hawawakilishi tena wananchi wake kama inavyotakiwa.

3. Rasimu ya pili ilipochakachuliwa, katiba pendekezwa (ambayo ndiyo ingeleta mfumo mpya wa utawala wa nchi) tumebakiwa na katiba karibu sawa na katiba ya sasa ya 1977.
4. Hivyo, kwa mfumo wa sasa hata Magufuli (Hapa ni Kazi Tu) hawezi kuleta mabadiliko yanayotakiwa maana mfumo wa serikali ya sasa na ambao ndio uliomlea na kumteua hawezi kwenda kinyume nao kwa maana 'he who goes against the system crushes himself'.

5. Kama Magufuli atashinda ‘it'll be just like pouring new wine into old wineskins'. Good intention only is not enough one has to be backed by the operating system in order to bring about desired changes.

6. Magufuli akishinda kuwa Rais atafanyaje?
 
Tumelogwa na aliyetuloga kafa! Watu hatujiulizi no link Pombe alijitenga na mafisadi? Fikiri!!
 
Watanzania ni kama Chapati kwa CCM wakiungua upande huu wanapinduliwa upande wa pili, tunahitaji kujitambua kulalamikia mfumo bila kuchukua hatua za kuubadilisha ni ukichaa.
mtapigwa kipigo cha mbwa mwizi. subirini tr 25.10.2015
 
Ndugu yangu, ni mfumo huu huu ambao ulifanya vizuri kwa Nyerere, Mwinyi na Mkapa!
Ni mfumo huu ambao utafanya kazi vizuri chini ya Magufuli!
Sasa hebu uelezee huo mfumo mpya wa ukawa ukoje???
Structure yake ikoje! Mfumo huo una watendaji gani?? Au ni hao akina Mbowe????
Msijaribu kulishwa maneno bila kufanya kautafiti kidogo!
 
ni magufuli tuuuu...hakuna mwingine...ukawa waroho wa madaraka
 
1954tanu

Nikweli mkuu,nakumbuka Philpo Mangula wakati anarudishwa kwenye chama baada ya kusota karibu miaka saba alisema nita safisha chama baada tu ya miezi sita.Ona sasa chama kimekuwa na majizi kuliko mwanzo
 
Last edited by a moderator:
Nikweli mkuu,nakumbuka Philpo Mangula wakati anarudishwa kwenye chama baada ya kusota karibu miaka saba alisema nita safisha chama baada tu ya miezi sita.Ona sasa chama kimekuwa na majizi kuliko mwanzo
Ndani ya uongozi wake, ametoa mgombea safi au mbaya? Tehe tehe, Maghufuli jembe.
 
Dawa yakuondoa mfumo wa wizi nikuondoa mfumo uliopo na kuweka mfumo mpya, Watanzania tusitegemee jipya sana kutoka kwa Magufuli, ingawa tunatambua utendaji wake ila hawezi kwenda nje ya mfumo uliomweka, swali rahisi lakujiuliza ni je Magufuli akigundua wizi wa waliomtangulia hasa maraisi ataweza kuwawajibisha? Muda unatoa jibu la mambo mengi.
 
Ndugu zangu,
Ujio wa Magufuli umenikumbusha ule ubeti wa Afande Sele kwenye ule wimbo wake wa "Darubini Kali", ambapo alitukumbusha kwamba tusitarajie "kuvuna miwa kwenye shamba la mihogo."

Tatizo linaloikabili inchi yetu sasa hivi ni kuwa na chama tawala kilichopoteza muelekeo na kuacha misingi ya kizalendo kwa maslahi ya nchi yetu. Katika hali kama hii usitarajie chama cha aina hii kuja na mtu wa mabadiliko au kwa maneno mengine, mtu "safi." Ule utabiri wa Mzee Nyerere kwamba "wananchi wasipoyaona mabadiliko ndani ya CCM, watayatafuta nje ya CCM" umefika.

CCM wamekuwa wakiwarubuni wananchi kila mwaka wa uchaguzi( haswa baada ya miaka 10) kwamba safari hii imeleta mtu wa kupambana na rushwa na majanga mengine yanayoikabili nchi. Lakini, ukweli ni kwamba majanga haya hayatomalizwa na Rais kutoka CCM, kwani tatizo sio rais, tatizo ni chama kibovu kilichotupa raisi huyo. Amkeni watanzania, nchi hii ina angamia!! Msitarajie kuvuna miwa kwenye shamba la mihogo!
 
ni kweli watanzania tuwe makinu tusichekelee ka zuzu kaokota kipande cha cha chupa akidhani dhahabu
 
Why are we as Tanzanians getting excited about the choice of Magufuli? This is a person who has served the rotten system led by CCM so faithfully and diligently over the plundering of the nation's wealth without a whimper. He is the
most appropriate choice of the invisible cabal of looters who expect their secrets to be preserved. He is just a lightweight
putting up a front to con poor Tanzanians once again. Sorry, I don't have your faith!!!
 
Back
Top Bottom