Magufuli sasa kufuta ibara ya 46 (3) ya katiba

Magufuli sasa kufuta ibara ya 46 (3) ya katiba

Sasa kufuta kifungu kuna maana gani wakati rasimu ya katiba ya Warioba imebeba mambo yote ,anachopaswa kufanya ni kurudisha rasimu ya katiba ya Warioba ,hapo ndio nitamwelewa ,vinginevyo mambo mengine ni sifa sasa
 
Nani alikuambia rais mstaafu hawezi kushitakiw?? Acheni Mbwembwe na Maigizo
Hata kesho wabunge wakitaka wanapiga kura a nashitakiwa
Sema aabunge magamba ndio wanatuangusha
 
Acha porojo.
Siunge mkono upuuzi kama huu kwani itakuja kusababisha Rais wa nchi kung'ang'ania madaraka kwa hofu ya kushtakiwa na kusababisha kutokea mapinduzi kama nchi za wenzetu

Mkuu pia kipengele hicho kikiondolewa Raisi kazi yake itakuwa kushinda mahakamani badala ya kufanya kazi za kiraisi,Wahuni utasikia leo wamemfungulia kesi mahakama ya kisutu,kesho anatakiwa mahakama kuu kanda ya mwanza keshokutwa anatakiwa mahakani songea nk.Kufuta hiyo sheria ni ujinga mtupu.Kuiweka ni kumwezesha afanye shughuli zake asikae anakesha mahakamani.Ukiruhusu kwa viinchi vyetu hivi kila siku watu watakuwa wanamburuza raisi hata kwa vitu vya kijinga tu
 
Kizingiti cha kwanza kitakuwa ni Bunge kwa mshangao wa wengi.

This is how system works.

Tusubiri.
nakubaliana nawe. Mafisiemu watajipanga. kuhakikisha wabunge wanaukataaa mswaada huo. Pia kama itakataliwa jpm ajue atakuwa ktk hali ngumu. Itamlazimu aongezewe ulinzi zaidi vinginevyo itakuwa sawa kumjeruhi nyati porini.
 
Kizingiti cha kwanza kitakuwa ni Bunge kwa mshangao wa wengi.

This is how system works.

Tusubiri.
Majuzi kuna uzi wachangiaji wamesema system ndiyo imemuweka JPM sasa leo system hiyo hiyo iko against JPM, system, system, system...
 
It a dream and a wishful thinking...hakuna mtu anayeota/kutaka kujikaanga kwa mafuta yake mwenyewe
 
Chanzo cha ndani Ikulu kimetoa habari kwamba mpaka sasa kazi zinazofanywa na Magufuli si mageni hata kidogo.

Kws mujibu wa chanzo hiki ni kwamba mafile yaliyoko mezani yalipelekwa siku nyingi sana na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Dr. Hoseah ila Serikali iliyokuwa ilipuuzia na kuyaweka kando.

Hivyo kwa mujibu wa chanzo hiki Dr. Hoseah anasemekana kufanya kazi zake nyingi kwa ustadi mkubwa ila amekuwa akipuuzwa.

Kwa mujibu wa chanzo hiki Dr. John Joseph Magufuli ameamua sasa muda si mrefu kukutana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano hasa akitaka Bunge lake lijalo lishughulike mapema sana kurekebisha Ibara ya 46(3) ambayo imeweka kinga dhidi ya kutoshtakiwa Rais aliyemaliza muda wake kwa kosa lolote.

Chanzo hicho kinasema Magufuli anataka Ibara hiyo ifutwe na kimsingi yeye anataka mtu aliwahi kuwa Rais na kulisababishia Taifa hasara aburuzwe Mahakamani......
 
Hiyo sheria ingewekwa kabla Mkwere hajamaliza muda wake ingesaidia sana.
naziona chuki zako za wazi kwa Kikwete, Akina mkapa waliojiuziwa kiwira, waliouza NBC, TANESCO, rada, ndege za jeshi,, magari ya jeshi, epa, meremeta, tangold na mengineyo huoni kabisa. naziona chuki zako za wazi kwa Kikwete. keep on mngese wewe.
 
Wanawachezea akili tu hamna kitu.
Ataishia kwenye visasi na vidagaa tu.
CCM wanataka tusahau kuwa walichakachua kura.
 
Back
Top Bottom