Magufuli Pumzika, yatosha sasa!

My Son drink water

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
4,932
13,283
Urais wako unakoma Oktoba 2020, hebu hata wewe jitathimini Kama kweli unafaa kuendelea kuongoza watanzania.

Hapa ulikolifikisha Taifa yatosha kabisa ,heshima yako itabaki pale pale Kama Rais mstaafu na hakuna utakachopungukiwa.

Maisha ya watu ni magumu kupindukia ktk awamu yako kuliko awamu zote zilizopita.

Eti kila anayelalamika maisha ni magumu eti alikuwa mpiga dili, hata watoto wadogo wanaolala na njaa nao walikuwa wapiga dili ndo maana wanalala njaa.

Mfumuko wa Bei ni mkubwa kupindukia, Pesa haipatikani mitaani kwa sababu umeanzisha miradi mingi kuliko uwezo wa nchi kiuchumi na kwa hiyo pesa zote zinaenda nje ya nchi na zile za Halmashauri umezihamishia serikali kuu eti zilikuwa zinaibiwa ila wezi hawakamatiki.

Tangu uingie madarakani hujaajiri wala kuongeza mishahara zaidi ya kufukuza watu kazi eti walikuwa na vyeti feki na Wafanyakazi hewa, mbona hao waliokuwa wakila pesa za Wafanyakazi hewa hatujaona hata mmoja akifikishwa mahakamani kwa uhujumu uchumi?
Wanaofikishwa mahakamani kwa uhujumu uchumi ni watu wanaokosoa utawala wako,kama Kabendera na Magoti.

Muda wako mwingi madarakani umeutumia kuua upinzani kwa kuwanunua Wapinzani na kuwahonga vyeo.

Uchumi unaouendesha ni wa aina yako mwenyewe, unaiga mataifa yaliyofeli huku ukitaka kufanikiwa.

Serikali huwa haifanyi Biashara, ATCL ungei privatize na siyo kutumia mabilioni ya Pesa kununua ndege badala ya kuboresha Elimu na Kilimo.

Mataifa yote yaliyofanikiwa Duniani yana mfumo mmoja, nao ni Demokrasia na Uchumi kuwa mikononi mwa watu na siyo serikali.

Hiyo China mnayojifanya wana CCM kuiiga, ina mfumo imara wa haki kwa watu wote chini ya Chama kimoja siyo nyie mnaolindana kwa kuitafuna nchi .

Na serikali ya China haifanyi tena Biashara, ime privatize njia zote za uchumi, ujamaa waliukimbia siku nyingi.

Mikononi mwako hakuna nuru ya mafanikio, umaskini ndo umekuwa role model ya watanzania, na kila anayekukosoa hadharani anakipata cha moto, bahati yake binafsi Ngurumo naye yangemkuta ya Ben Saanane na Azory Gwanda.
Tanzania nzima inalia maisha magumu, mradi wa umeme wa Hydro Power ulioanzisha kwa pesa nyingi hauna impact yoyote kwenye uchumi kwa sababu ni wa kizamani mno .

Nchi ikiingia kwenye ukame umeme unakuwa wa mgao tena, hakuna ulichofanya, ndo maana Wajerumani walikushauri wajenge mitambo ya umeme wa Gesi kwa umeme wa uhakika kwa sababu Gesi tunayo nyingi.

Tutaikumbuka mno hiyo hifadhi ya Selous ambayo miti zaidi ya milioni moja imekatwa ili kupisha ujenzi wa Bwawa la umeme.

Miti huwa inavuta mvua pia, sasa itakuwaje hali ya Geography ya mvua hilo eneo na wakati Bwawa linahitaji maji ili umeme upatikane?
Yetu macho.

Wakati wa Kampeni utatueleza nini watanzania?
Na unataka uendelee kutuongoza ili iweje?




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kura haina nguvu Afrika!
Kuna sababu kura haina nguvu.

Kampeni ya kumuondoa kwa kura si kupiga kura tu, ni pamoja na kuipa nguvu kura.

Kwa mfano, kama Tume ya Uchaguzi inatumika kubadili kura, mabadiliko ya tume ya uchaguzi nayo yanatakiwa kuwa katika kampeni.

Bottom line, kumwambia Magufuli apumzike kwa hiyari yake, ukitegemea akusikilize na kukubali, ni biashara kichaa.
 
Kuna sababu kura haina nguvu.

Kampeni ya kumuondoa kwa kura si kupiga kura tu, ni pamoja na kuipa nguvu kura.

Kwa mfano, kama Tume ya Uchaguzi inatumika kubadili kura, mabadiliko ya tume ya uchaguzi nayo yanatakiwa kuwa katika kampeni.

Bottom line, kumwambia Magufuli apumzike kwa hiyari yake, ukitegemea akusikilize na kukubali, ni biashara kichaa.
Serekali za Afrika zilizopo madarakani kuzigusia kuwa inatakiwa tume huru ni sawa na kujaribu kumwaminisha papa kuwa hakuna Mungu bali ni story tu za kutunga!
 
Ni ajabu unalinganisha Tanzania na nchi zilizoendelea hapo hapo unasema Serikali haijaajiri, ni Serikali gani Dunia hii hutoa ajira kwa Wananchi? Tangia lini Serikali ikawa mwajiri mkuu? Isitoshe unaelewa kwa nini huitwa Shirika la ndege huitwa ,,national airline“ ?
 
Ni ajabu unalinganisha Tanzania na nchi zilizoendelea hapo hapo unasema Serikali haijaajiri, ni Serikali gani Dunia hii hutoa ajira kwa Wananchi? Tangia lini Serikali ikawa mwajiri mkuu? Isitoshe unaelewa kwa nini huitwa Shirika la ndege huitwa ,,national airline“ ?
Bwana mdogo, uelewa wako ni mdogo mno kwenye mada Kama hii,
Walimu huajiriwa na Kampuni gani Kama siyo serikali?
Elewa maudhui ya mada ,National Airline ni serikali kufanya Biashara jambo ambalo ni la hovyo kabisa.
Kazi ya serikali ni kukusanya kodi na kusimamia uchumi kupitia Central Bank na Treasury.
Pesa za serikali ni kwa ajili ya Elimu, Afya na infrastructures.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom