Magufuli ondoa bugudha ya kuchelewesha ajira za walimu

Magufuli ondoa bugudha ya kuchelewesha ajira za walimu

Vumilieni Bandugu Mwaka jana 2014 Tumekula kitaa balaa..Nilihitimu Pale udsm July 04 2014..mahafali nikafanya November 15 Ajira nikapata May mwaka huu 2015 Mshahara wa Kwanza nikaanza kupata September 2015 !!

Naidai serikali Mishahara ya miezi mi 4 madeni ambayo yamesababishwa na Uzembe wa aliekua anakaimu Nafasi ya Afisa utumishi wilaya Ikungi singida nilipopangwa (bila ya kupachagua) baada ya kuchelewa kutuma taarifa zangu pahala husika ili niingizwe kwenye payroll,,!!Sjui nalipwa lini labda Mr Pombe anavyobana matumizi huenda Hazina wakanikumbuka
..

Kazi Mazingira ni magumu,,Mshahara wenyewe ndo kama huo.,,Huduma duni za afya,,Upatikanaji duni wa maji(ya chumvi visimani...yanapaushaje??),,ukosefu wa umeme,,so waalimu wapya mue tayari kupokea changamoto hizi..vinginevyo mtaanza kulialia tu Halmashauri...

Navutia miaka mi3 nitimize masharti Ajirani nirudi tena Mlimani kupigana na Masters katika kada tofauti na Elimu...Bado sijaridhika...hii ni kama njia tu ya kutokeaa..Waalimu msibweteke!!
 
kwanini hutaki kuambiwa ukweli serikali haina haja na walimu wa arts ni sayansi wataajiriwa nao wachache sanaa watakuwa wanaajiriwa kulinganan na uhitaji sio kama ilivyokuwa kipindi cha kikwete saizi tupo kwenye austerity measure hatujazi watu ofisini kwenda kupiga stori kuna shule somo moja walimu 3. ushauri wangu mjipange kwa sera za kubana matumizi hamuwezi salimika sasa serikali inaangalia uboreshaji wa maslahi ya mwalimu pamoja na mazingira ya kujifunzia ikiwemo madawati.

acha upotoshaji wako wewe. Walimu tarajali wameshaanza kupangiwa vituo toka mwezi wa11. Na zile changamoto za ucheleweshaji wa ajira kwa mwaka huu ilikuwa ni kukosa kanzidata hasa maeneo ya vijijini ambapo tayari kanzidata ya walimu wanaohtajka tayari ipo tamisemi na ajira mpya 2016/17 zitatoka mapema sana baada ya kupeleka kibali cha ajira.
 
ata kama ajira zikisitishwa, vyuo havitaacha kudahili wanafunzi katika fani ya ualimu kwa sababu ni fani kama fani nyingine tukumbuke pia kuwa wanafunz hawasomi bure na pia wanafunzi ndio wanaomba kupangwa vyuo flani.
 
kwa kifupi ni kwamba ajira za walimu zipo lakini mfumo wa kuajir lazima ubadilike kwa serikali ya awamu ya tano...jitahidini sana kujifunza namna ya kuandika APPLICATION LETTER pamoja na CV na jiandaeni kwa INTERVIEW watakaofanya vizur ndio watakao ajiriwa.
 
Hyo ni kweli
 
ajira ni muhimu hata kama ni october mwakani wataajiri tu na haijarishi ni art au sayansi wote wataajiriwa kama wa art wangekuwa hawaitajiki basi vyuo visingekuwa vinawachukua lakn mpaka leo vyuo vipo na vinawadahiri , kama huna cha kusema bora usiwachokonoe wenzio usikie watasema nini muda mwingine unaweza tukanwa ukaaibika bure.

Kwani kozi nyingine ambazo hazina ajira wanafunzi wameachwa kudailiwa?
 
acha upotoshaji wako wewe. Walimu tarajali wameshaanza kupangiwa vituo toka mwezi wa11. Na zile changamoto za ucheleweshaji wa ajira kwa mwaka huu ilikuwa ni kukosa kanzidata hasa maeneo ya vijijini ambapo tayari kanzidata ya walimu wanaohtajka tayari ipo tamisemi na ajira mpya 2016/17 zitatoka mapema sana baada ya kupeleka kibali cha ajira.

Hyo kanzi data haina umuhimu wowote maana walimu wakishaletwa halmashauri wanaonga maafisa elimu wanapangwa mijin tu, huku vijijin wanaenda wachache sana. Kwa mfano mwaka huu shule moja tumepangwa walimu 50 na za vijijin wameambulia walimu 3 kila shule
 
tuombe mungu mkuu tutakutana hapa mwez feb kutoa shilingi.
 
Mbona hamjiamini walimu si waziri amesema mwezi mei kwani mwezi mei umeisha? Acheni kutishana
 
reasoning yako iko chini sana kijana nani kakuambia watu wana ajiriwa sababu vyuo bado vina dahiri. na kwanini ufikirie kutukana unpoambiwa ukweli ambao huutaki ajira za walimu wa sanaa hakuna i save hii comment uje tena hapa mwakani kunikumbusha.
Mkuu mwakani umeshafika mtag basi huyo jamaa
 
Muwe na subura ajira zenu zinashugulikiwa by wa pili mtakuwa mmepangiwa vituo vya kazi.
Kwa Ubashite huu!? Labda walimu wa Kenya nao wagome kwa miezi minne ili mpate nafasi ya kuomba nafasi za kazi huko kwa ilivyo sasa kwa Madaktari.
 
Ukinishauri ndiyo umeharibu kabisaa
Mimi sijaribiwi aliyasema jana
 
Back
Top Bottom