Magufuli ni mbumbumbu wa Diplomasia?

Magufuli ni mbumbumbu wa Diplomasia?

Toka Magufuli aingie madarakani kama Rais wa Tanzania, mwenendo mzima wa Diplomasia ya Tanzania umekuwa tata kabisa. Tanzania kwa sasa ameanza kupoteza taswira nzima ya Diplomasia ya mambo ya nchi za nje na pia katika utatuzi wa migogoro, iwe ya kisiasa au kisheria.
Hapa chini ni mifano michache ya matukio ya kustaajabisha yaliyofanywa na Serikali ya Magufuli katika Nyanza ya Diplomasia ambayo yamezaa maswali makubwa sana.

1/Magufuli amegoma kusafiri nje ya nchi ili kwenda kuhudhuria mikutano ya Wakuu wa nchi na badala yake amekuwa akituma wawakilishi.

2/Magufuli ameandaa Hafla ya mabalozi Ikulu lakini akakimbia kuhudhuria hafla hiyo.

3/Magufuli ametoa jibu la utatuzi wa mgogoro mkubwa wa kisiasa Zanzibar pasipo kufanya majadiliano ya usuluhishi na pande zinazovutana.

4/Serikali ya Magufuli(Kupitia kwa wasemaji wake) imesema haiwajibiki kuingilia kutatua mgogoro wa kisiasa Zanzibar lakini itawajibika wakati wote kupeleka askari polisi na askari jeshi ili kuzima ghasia zozote zinazotokana na mgogoro wa Zanzibar.

5/Magufuli amesema tayari anajua hukumu za Mahakamani kuhusu kesi zinazoendelea zinazohusu wadaiwa wa Serikali kabla ya hizo kesi kusikilizwa au kwisha!!
 
Magufuli ameomba aachwe kwa muda kama wa miezi 6 ili asuke nchi. Kwa hali ilivyokuwa Waziri wa mambo ya nje alikuwa hana kazi maana aliyekuwepo Ikulu alikuwa anaifanya hiyo kazi, na ilifika mahali mabalozi wa nje wakaona kama Ikulu ndiyo wizara inayowahusu, Wizara ya mambo ya kigeni wao walikuwa kama tarishi tu! Ikulu ilikuwa na wageni wa kila aina mpaka wacheza mpira wa vikapu!

Kwa mtazamo wa jicho la tatu, Magufuli anataka apitie kila kitu na ajiweke sawa 'kimfumo' na atakapoanza kukutana na watu wa nje (mabalozi wakiwemo) ajue anataka nini (ambacho amekosa nchini). Ombaomba inafedhesha, inavunja heshma ya nchi na watu wake. Tanzania tunaomba misaada mingine ya aibu kabisa - msaada ya kuweka vidumu ya maji ya kunawa mikono watoto shuleni wanapotoka maliwatoni!

Lakini pia naamini Magufuli anashindwa kuongea mambo mengine hadharani lakini upo uwekezakano amekuta mafaili yamejaa kila kona ya 'jumba jeupe' huku yakiwa hayajafanyiwa kazi! Mwenyeji wa zamani alikuwa na muda mchache sana nchini na hivyo hakuweza kufanya mambo mengi!!! Mambo mengine ni yanasikitisha kidogo lakini ndio hivyo.

NB: Rais wa Botswana vipi, na unaonaje mambo ya Botswana!

kaka hii ni siasa ...kwa wema kabisa nchi hii yetu sote ....hakuna namna ya kumtetea magufuli katika hili .....kuna majukumu ya kirais ambayo hayana mbadala ...ni lazima awe yeye.........sidhani kama toka mwaka 1961 hadi leo 2016 marais wote hawakuwa na kazi ...hadi iwe yeye....,kavunja utamaduni wa jumuia ya madola na jumuia ya kimataifa ....
Hata marais walio na kazi nyingi na za hatari kama BASHER AL ASSAD , Hizi kazi wanafanya wenyewe ...
Hata mataifa makubwa kama Uk,usa,japan,india,russia ,china ...hapo lazima atoke rais hadharani ...............pengine kama tunataka kuiga siasa za nje za NORTH KOREA . ..ndie wana rais ambaye hasafiri nje ,wala hakutani na wageni
 
Kwenye Diplomasia Magu ni disaster tukubali
kwenye tathmini ya wagombea wa ccm ..hili suala la kutokuwa na uzoefu na siasa za nje .....,na historia ya shaka ya afya yake huko nyuma ya mwili na akili ....ni kati ya mambo yaliyotiwa shaka , na pengine JK Kwa kujua taarifa hizi za tathmini na kutokuwa na uzoeufu ndani ya chama alijuwa wajumbe wangemuangusha ...lakiNI Mungu sio athumani ......watu wote wa LOWASSA wakaungana kumpa magufuli kura za ushindi .......
Nina imani kwa kuwa Magufuli ni super intelligent beside all those odds atajifunza kea bidii kufunika madhaifu yake hasa ukizingatia ana waziri wa nje mzuri sana .....muhimu amsikilize!!
 
Saddam hussein rais wa libya ooops rais wa kuwait hahahahaha toka dunia iumbwe libya na kuwai hakujawahi kuwa na vyeo vya urais
 
Mj
kaka hii ni siasa ...kwa wema kabisa nchi hii yetu sote ....hakuna namna ya kumtetea magufuli katika hili .....kuna majukumu ya kirais ambayo hayana mbadala ...ni lazima awe yeye.........sidhani kama toka mwaka 1961 hadi leo 2016 marais wote hawakuwa na kazi ...hadi iwe yeye....,kavunja utamaduni wa jumuia ya madola na jumuia ya kimataifa ....
Hata marais walio na kazi nyingi na za hatari kama BASHER AL ASSAD , Hizi kazi wanafanya wenyewe ...
Hata mataifa makubwa kama Uk,usa,japan,india,russia ,china ...hapo lazima atoke rais hadharani ...............pengine kama tunataka kuiga siasa za nje za NORTH KOREA . ..ndie wana rais ambaye hasafiri nje ,wala hakutani na wageni

Mkuu jose eduardo dos santos pia huwa hasafiri nje
 
Nadhani ipo haja ya kufahamu maana ya diplomasia ili uweze kumfanyia tathmini Magufuli katika uwanja wa diplomasia
Kwa faida ya watu ambao somo la diplomasia sio eneo jipya kwao nianzie tasfiri nyepesi na kutumia mifano‎ ya kawaida kabisa.....
Diplomasia inahusu mahusiano (relations) ya nchi moja na nchi nyingine, na pia inahusu ushirikiano‎ (cooperations) baina ya nchi moja na nchi nyinginezo zenye mtazamo,malengo,agenda inayofanana
Njia kuu ya kujenga mahusiano ni kupitia mawasiliano‎.....ambayo yanaweza kufanyika kwa njia ya:
1) Kiongozi wa nchi kukutana ana kwa ana na kiongozi wa nchi nyingine‎
2) Kiongozi wa nchi kuwa na mawasiliano ya barua, simu,nukushi na viongozi wengine‎
3) Kiongozi wa nchi kutuma mwakilishi wake Katika nchi yenye uhusiano na nchi yake (Mabalozi)
4) Kiongozi wa nchi kutuma Mjumbe wake maalum kwa kiongozi wa nchi nyingine‎ (special envoy)
hizi njia zote hutumika kwenye diplomasia- kwa maana ya kujenga na kukuza uhusiano na ushirikiano.
Ukifanya tathmini ya siku alizokaa madarakani, Rais Magufuli amefanya kazi kubwa ya diplomasia kwa kutumia njia zote nilizozitaja hapo juu. Pengine nifanye uchambuzi wa njia moja baada ya nyingine kuonyesha ushahidi wa ninachosema
1) Kiongozi wa nchi kukutana ana kwa ana na kiongozi wa nchi nyingine
Rais Magufuli mara baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano alikutana na kufanya mazungumzo na Wakuu wa nchi mbalimbali waliohudhuria sherehe zake za kuapishwa....walikuwepo marais kadhaa kutoka Kenya,Uganda,Rwanda,Mozambique, Zambia,Zimbabwe n.k Wote hawa alipata fursa ya kuonana nao na pia aliwaandalia chakula cha mchana na kujumuika nao. Katika mazungumzo na kila mmoja wao,alizungumzia kuendeleza mahusiano ya Tanzania na nchi zao
2) Kiongozi wa Nchi kuwa na mawasiliano ya simu,barua,nukushi
Rais Magufuli toka aingie madarakani amepokea barua nyingi kutoka kwa Wakuu wa nchi mbalimbali duniani kumpongeza kuingia madarakani na yeye amewajibu barua hizo na kuwahakikishia kuendeleza ushirikiano na nchi zao. Vilevile Rais Magufuli amekuwa na mawasiliano ya simu na viongozi mbalimbali wa nje kuzungumzia masuala ya mashirikiano ya kikanda,kimataifa......
‎
3) Kiongozi wa nchi kutuma mwakilishi wake Katika nchi yenye uhusiano na nchi yake (Mabalozi)‎
‎
‎Rais Magufuli anao mabalozi wanaomwakilisha katika nchi zipatazo 30 na ushee.....na pale palipokuwa na haja,amewapa maelekezo ya kumwakilisha na kumfikishia ujumbe sehemu mbalimbali. Mabalozi wa Tanzania huko Afrika ya Kusini, Uingereza, Italy, Uswisi, Ufaransa wamehudhuria vikao mbalimbali kwa niaba ya Tanzania na ushiriki wa Tanzania ulikuwa timilifu.
‎ Vilevile, Rais Magufuli amekutana na wawakilishi (mabalozi) wa viongozi wengine hapa nchini mara kadhaa...mfano amekutana na Balozi wa Sudan,Zambia,Malawi, Norway,China, Korea ya kusini,Israel, Angola, Palestina,Finland, Switzerland, Rwanda n.k Wote hao wamemfikishia ujumbe kutoka kwa viongozi wao na yeye aliwapa ujumbe wa kupeleka kwenye nchi zao. Pia Rais Magufuli amekutana na wawakilishi wa Taasisi za Kimataifa kama vile World Bank, African Development Bank n.k kwenye mikutano yao ameongelea jinsi taasisi hizo zitakavyoshirikiana na Tanzania kutekeleza miradi mikubwa ya miundombinu ya umeme, maji,barabara n.k
‎4) Kiongozi wa nchi kutuma Mjumbe wake maalum kwa kiongozi wa nchi nyingine‎ (special envoy)‎
Toka aingie madarakani Rais Magufuli mara kadhaa amepokea Wajumbe Maalum wa Viongozi wa Nje kuja kumfikishia ujumbe kutoka kwa viongozi hao....mfano Rais Paul Kagame alimtuwa Waziri wake wa mambo ya nje kuja kuonana na Rais magufuli kuzungumzia masuala ya ushirikiano.....kupitia mjumbe huyo maalum Rais kagame alielezea kufurahishwa kwake na hatua alizochukua Rais Magufuli kuboresha utendaji bandari ya Dar es salaam inayotumiwa na nchi yake kupitishia mizigo..... Rais Magufuli pia alimpokea mjumbe maalum wa Rais Albashir wa Sudan ambaye alimtuma Waziri wake wa Mambo ya Nje, vilevile Rais Magufuli alimpokea mjumbe maalum wa Waziri Mkuu wa Japan ambaye alipata fursa ya kuelezea namna nchi hiyo itakavyoendelea kushirikiana na Tanzania kwenye ujenzi wa miundombinu ya barabara na umeme.Kwenye ujio huo mgeni huyo alishuhudia utiwaji saini mkopo wa zaidi ya bilioni 900 kwa ajili ya ujenzi wa njia ya umeme. Rais Magufuli pia alimpokea Mjumbe maalum wa Rais wa China ambaye alimtuma Makamu Mwenyekiti wa Bunge la China...naye alimhakikishia Rais ushirikiano wa China na Tanzania katika nyanja mbalimbali.
Mbali na kupokea wajumbe wa viongozi wakuu wa nchi mbalimbali Rais Magufuli naye mara kadhaa ametuma wajumbe wake maalum kukutana na viongozi mbalimbali......mfano amemtuma Makamu wa Rais kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa Nchi wa China na Afrika, pia alimtuma Makamu wa Rais kwenye mkutano wa Umoja wa Afrika. Katika mikutano yote hiyo Makamu wa Rais alikutana na kufanya mazungumzo na wakuu wa nchi za Kenya, Botswana, Zambia,n.k kufikisha ujumbe wa Rais Magufuli kuhusu masuala mbalimbali. Aidha,Rais Magufuli alimtuma Waziri mkuu kumwakilisha kwenye mkutano wa SADC, na pia alimtuma Waziri wa mambo ya Nje kufikisha ujumbe maalum kwa Rais Nkurunzinza na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Afrika
Kwa ujumla diplomasia ya Tanzania imeendelea kung'ara katika kipindi cha siki 100 za Serikali ya awamu ya tano na mwelekeo unaonyesha itazidi kung'ara.
Kuhusu Waziri wa Mambo ya Nje kufanya sherehe na mabalozi
Rais magufuli sio mtu wa kufanya kazi kwa mazoea.....kila anachofanya hukipima faida zake kwa wakati husika....endapo atajikuta ana majukumu yanayogongana,mara zote huchagua kufanya jukumu lenye umuhimu wa haraka na tija kwa wananchi‎...hivyo anavyosema aliwakilishwa kwakuwa hakuwepo Dar,maana yake alipokuwa kulikuwa na majukumu mengine mazito ya kitaifa ambayo hana ulazima wa kuyaeleza kwakuwa si kila kazi afanyayo rais inaelezwa.
Lakini sio ajabu kwa foreign Minister kuhost new Year's party...nchi nyingine wanafanya hivyo.....kule China, tarehe 6 january..Foreign minister wao alihost party hiyo kwa mabalozi angalia link hiyo ‎Foreign Ministry Holds 2016 New Year Reception
Na kuhusu kusafiri kwenda nje.......Rais wetu amechaguliwa kuongoza nchi kwa siku 1825 (miaka mitano) na Mungu akipenda siku nyingine 1825 awamu ya pili‎.....hana haraka ya kusafiri ndani ya siku 100..... wakati ukifika, haja ikiwepo atasafiri bila shaka yoyote. Rais wa Botswana hasafiri sana, hakuna walilopungukiwa kama nchi.....na diplomasia yao inashamiri.
hivyo nikijibu swali la mtoa mada kwamba magufuli ni mbumbumbu wa Diplomasia? Jibu ni Hapana. Ushahidi niliouweka hapo unaonyesha ANAFANYA mambo ipasayo.‎
‎
‎
‎
hii post yako wanaipita kama hawaioni..!!! ila wenye akili tumeshajua nini kinachotafutwa katika huu uzi!!

ufafanuzi mzuri kabisa mkuu, kama bado mtu atashindwa kukuelewa basi uyo ana ajenda yake binafsi!!!

ni kweli Raisi sio malaika kama hana makosa... ila kulazimishia makosa yasiyo ya lazima na kutuhumu bila ya kua na hoja yenye mantiki ni Ujuha!!
Siasa zinatufanya tunakua WAJINGA...
 
hapo namba 2. mabalozi wanawasiliana kwa kutumia lugha gani?
 
Nasikia lugha za kigeni hazipandi kwa Mkuu wewe ndo maana, anasepa, si mlimuona mama suluhu kule nje alikuwa amevalishwa king'amuzi masikioni, hata kwetu Mkuu wa kaya angewavalisha wageni king'amuzi ili aongee kwa lugha anayoimudu?
 
Mj

Mkuu jose eduardo dos santos pia huwa hasafiri nje

jose eduardo dos santos ... wamekaa sana haga wakati wanapigania uhuru ....na kina augustino neto ,baadaye nchi ikaingia vita ya wenyewe kwa wenyewe akipigana na JONAS SAVIMBI ....wakati huo alikuwa anasafiri sana ,siku hizi amepunguza au hasafiri kwa kuwa umri wake umesogea sana ..na offcourse baada ya amani uchumi umekuwa mzuri sana ...sana .

Rais wa zamani wa Kenya , Jomo Kenyatta alikuwa akisema wazi kuwa hapendi kusafiri kwakuwa ukiacha umri kusogea alikuwa anakiri kuogopa ndege ....na ziara zake nyingi za nje alikuwa akifanya makamu wake wakati huo ...DANIEL TOROITICH ARAP MOI
 
Toka Magufuli aingie madarakani kama Rais wa Tanzania, mwenendo mzima wa Diplomasia ya Tanzania umekuwa tata kabisa. Tanzania kwa sasa ameanza kupoteza taswira nzima ya Diplomasia ya mambo ya nchi za nje na pia katika utatuzi wa migogoro, iwe ya kisiasa au kisheria.
Hapa chini ni mifano michache ya matukio ya kustaajabisha yaliyofanywa na Serikali ya Magufuli katika Nyanza ya Diplomasia ambayo yamezaa maswali makubwa sana.

1/Magufuli amegoma kusafiri nje ya nchi ili kwenda kuhudhuria mikutano ya Wakuu wa nchi na badala yake amekuwa akituma wawakilishi.

2/Magufuli ameandaa Hafla ya mabalozi Ikulu lakini akakimbia kuhudhuria hafla hiyo.

3/Magufuli ametoa jibu la utatuzi wa mgogoro mkubwa wa kisiasa Zanzibar pasipo kufanya majadiliano ya usuluhishi na pande zinazovutana.

4/Serikali ya Magufuli(Kupitia kwa wasemaji wake) imesema haiwajibiki kuingilia kutatua mgogoro wa kisiasa Zanzibar lakini itawajibika wakati wote kupeleka askari polisi na askari jeshi ili kuzima ghasia zozote zinazotokana na mgogoro wa Zanzibar.

5/Magufuli amesema tayari anajua hukumu za Mahakamani kuhusu kesi zinazoendelea zinazohusu wadaiwa wa Serikali kabla ya hizo kesi kusikilizwa au kwisha!!
Hapa kazi tu
 
Mabalozi wana jukumu kubwa katika swala la Diplomasia kutokana na ukweli kuwa ni swala wanaloshughulika nalo moja kwa moja,hivyo tuwaachie hilo jukumu. Sisi Tunahitaji Rais atutumikie sisi na sio kushinda angani au kuacha majukumu ya maana yenye tija kwa ajili ya kutoa speech ya dakika tano kwenye sherry party.
 
Toka Magufuli aingie madarakani kama Rais wa Tanzania, mwenendo mzima wa Diplomasia ya Tanzania umekuwa tata kabisa. Tanzania kwa sasa ameanza kupoteza taswira nzima ya Diplomasia ya mambo ya nchi za nje na pia katika utatuzi wa migogoro, iwe ya kisiasa au kisheria.
Hapa chini ni mifano michache ya matukio ya kustaajabisha yaliyofanywa na Serikali ya Magufuli katika Nyanza ya Diplomasia ambayo yamezaa maswali makubwa sana.

1/Magufuli amegoma kusafiri nje ya nchi ili kwenda kuhudhuria mikutano ya Wakuu wa nchi na badala yake amekuwa akituma wawakilishi.

2/Magufuli ameandaa Hafla ya mabalozi Ikulu lakini akakimbia kuhudhuria hafla hiyo.

3/Magufuli ametoa jibu la utatuzi wa mgogoro mkubwa wa kisiasa Zanzibar pasipo kufanya majadiliano ya usuluhishi na pande zinazovutana.

4/Serikali ya Magufuli(Kupitia kwa wasemaji wake) imesema haiwajibiki kuingilia kutatua mgogoro wa kisiasa Zanzibar lakini itawajibika wakati wote kupeleka askari polisi na askari jeshi ili kuzima ghasia zozote zinazotokana na mgogoro wa Zanzibar.

5/Magufuli amesema tayari anajua hukumu za Mahakamani kuhusu kesi zinazoendelea zinazohusu wadaiwa wa Serikali kabla ya hizo kesi kusikilizwa au kwisha!!
serikali hii ni ya kukurupuka
 
Nadhani ipo haja ya kufahamu maana ya diplomasia ili uweze kumfanyia tathmini Magufuli katika uwanja wa diplomasia
Kwa faida ya watu ambao somo la diplomasia sio eneo jipya kwao nianzie tasfiri nyepesi na kutumia mifano‎ ya kawaida kabisa.....
Diplomasia inahusu mahusiano (relations) ya nchi moja na nchi nyingine, na pia inahusu ushirikiano‎ (cooperations) baina ya nchi moja na nchi nyinginezo zenye mtazamo,malengo,agenda inayofanana
Njia kuu ya kujenga mahusiano ni kupitia mawasiliano‎.....ambayo yanaweza kufanyika kwa njia ya:
1) Kiongozi wa nchi kukutana ana kwa ana na kiongozi wa nchi nyingine‎
2) Kiongozi wa nchi kuwa na mawasiliano ya barua, simu,nukushi na viongozi wengine‎
3) Kiongozi wa nchi kutuma mwakilishi wake Katika nchi yenye uhusiano na nchi yake (Mabalozi)
4) Kiongozi wa nchi kutuma Mjumbe wake maalum kwa kiongozi wa nchi nyingine‎ (special envoy)
hizi njia zote hutumika kwenye diplomasia- kwa maana ya kujenga na kukuza uhusiano na ushirikiano.
Ukifanya tathmini ya siku alizokaa madarakani, Rais Magufuli amefanya kazi kubwa ya diplomasia kwa kutumia njia zote nilizozitaja hapo juu. Pengine nifanye uchambuzi wa njia moja baada ya nyingine kuonyesha ushahidi wa ninachosema
1) Kiongozi wa nchi kukutana ana kwa ana na kiongozi wa nchi nyingine
Rais Magufuli mara baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano alikutana na kufanya mazungumzo na Wakuu wa nchi mbalimbali waliohudhuria sherehe zake za kuapishwa....walikuwepo marais kadhaa kutoka Kenya,Uganda,Rwanda,Mozambique, Zambia,Zimbabwe n.k Wote hawa alipata fursa ya kuonana nao na pia aliwaandalia chakula cha mchana na kujumuika nao. Katika mazungumzo na kila mmoja wao,alizungumzia kuendeleza mahusiano ya Tanzania na nchi zao
2) Kiongozi wa Nchi kuwa na mawasiliano ya simu,barua,nukushi
Rais Magufuli toka aingie madarakani amepokea barua nyingi kutoka kwa Wakuu wa nchi mbalimbali duniani kumpongeza kuingia madarakani na yeye amewajibu barua hizo na kuwahakikishia kuendeleza ushirikiano na nchi zao. Vilevile Rais Magufuli amekuwa na mawasiliano ya simu na viongozi mbalimbali wa nje kuzungumzia masuala ya mashirikiano ya kikanda,kimataifa......
‎
3) Kiongozi wa nchi kutuma mwakilishi wake Katika nchi yenye uhusiano na nchi yake (Mabalozi)‎
‎
‎Rais Magufuli anao mabalozi wanaomwakilisha katika nchi zipatazo 30 na ushee.....na pale palipokuwa na haja,amewapa maelekezo ya kumwakilisha na kumfikishia ujumbe sehemu mbalimbali. Mabalozi wa Tanzania huko Afrika ya Kusini, Uingereza, Italy, Uswisi, Ufaransa wamehudhuria vikao mbalimbali kwa niaba ya Tanzania na ushiriki wa Tanzania ulikuwa timilifu.
‎ Vilevile, Rais Magufuli amekutana na wawakilishi (mabalozi) wa viongozi wengine hapa nchini mara kadhaa...mfano amekutana na Balozi wa Sudan,Zambia,Malawi, Norway,China, Korea ya kusini,Israel, Angola, Palestina,Finland, Switzerland, Rwanda n.k Wote hao wamemfikishia ujumbe kutoka kwa viongozi wao na yeye aliwapa ujumbe wa kupeleka kwenye nchi zao. Pia Rais Magufuli amekutana na wawakilishi wa Taasisi za Kimataifa kama vile World Bank, African Development Bank n.k kwenye mikutano yao ameongelea jinsi taasisi hizo zitakavyoshirikiana na Tanzania kutekeleza miradi mikubwa ya miundombinu ya umeme, maji,barabara n.k
‎4) Kiongozi wa nchi kutuma Mjumbe wake maalum kwa kiongozi wa nchi nyingine‎ (special envoy)‎
Toka aingie madarakani Rais Magufuli mara kadhaa amepokea Wajumbe Maalum wa Viongozi wa Nje kuja kumfikishia ujumbe kutoka kwa viongozi hao....mfano Rais Paul Kagame alimtuwa Waziri wake wa mambo ya nje kuja kuonana na Rais magufuli kuzungumzia masuala ya ushirikiano.....kupitia mjumbe huyo maalum Rais kagame alielezea kufurahishwa kwake na hatua alizochukua Rais Magufuli kuboresha utendaji bandari ya Dar es salaam inayotumiwa na nchi yake kupitishia mizigo..... Rais Magufuli pia alimpokea mjumbe maalum wa Rais Albashir wa Sudan ambaye alimtuma Waziri wake wa Mambo ya Nje, vilevile Rais Magufuli alimpokea mjumbe maalum wa Waziri Mkuu wa Japan ambaye alipata fursa ya kuelezea namna nchi hiyo itakavyoendelea kushirikiana na Tanzania kwenye ujenzi wa miundombinu ya barabara na umeme.Kwenye ujio huo mgeni huyo alishuhudia utiwaji saini mkopo wa zaidi ya bilioni 900 kwa ajili ya ujenzi wa njia ya umeme. Rais Magufuli pia alimpokea Mjumbe maalum wa Rais wa China ambaye alimtuma Makamu Mwenyekiti wa Bunge la China...naye alimhakikishia Rais ushirikiano wa China na Tanzania katika nyanja mbalimbali.
Mbali na kupokea wajumbe wa viongozi wakuu wa nchi mbalimbali Rais Magufuli naye mara kadhaa ametuma wajumbe wake maalum kukutana na viongozi mbalimbali......mfano amemtuma Makamu wa Rais kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa Nchi wa China na Afrika, pia alimtuma Makamu wa Rais kwenye mkutano wa Umoja wa Afrika. Katika mikutano yote hiyo Makamu wa Rais alikutana na kufanya mazungumzo na wakuu wa nchi za Kenya, Botswana, Zambia,n.k kufikisha ujumbe wa Rais Magufuli kuhusu masuala mbalimbali. Aidha,Rais Magufuli alimtuma Waziri mkuu kumwakilisha kwenye mkutano wa SADC, na pia alimtuma Waziri wa mambo ya Nje kufikisha ujumbe maalum kwa Rais Nkurunzinza na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Afrika
Kwa ujumla diplomasia ya Tanzania imeendelea kung'ara katika kipindi cha siki 100 za Serikali ya awamu ya tano na mwelekeo unaonyesha itazidi kung'ara.
Kuhusu Waziri wa Mambo ya Nje kufanya sherehe na mabalozi
Rais magufuli sio mtu wa kufanya kazi kwa mazoea.....kila anachofanya hukipima faida zake kwa wakati husika....endapo atajikuta ana majukumu yanayogongana,mara zote huchagua kufanya jukumu lenye umuhimu wa haraka na tija kwa wananchi‎...hivyo anavyosema aliwakilishwa kwakuwa hakuwepo Dar,maana yake alipokuwa kulikuwa na majukumu mengine mazito ya kitaifa ambayo hana ulazima wa kuyaeleza kwakuwa si kila kazi afanyayo rais inaelezwa.
Lakini sio ajabu kwa foreign Minister kuhost new Year's party...nchi nyingine wanafanya hivyo.....kule China, tarehe 6 january..Foreign minister wao alihost party hiyo kwa mabalozi angalia link hiyo ‎Foreign Ministry Holds 2016 New Year Reception
Na kuhusu kusafiri kwenda nje.......Rais wetu amechaguliwa kuongoza nchi kwa siku 1825 (miaka mitano) na Mungu akipenda siku nyingine 1825 awamu ya pili‎.....hana haraka ya kusafiri ndani ya siku 100..... wakati ukifika, haja ikiwepo atasafiri bila shaka yoyote. Rais wa Botswana hasafiri sana, hakuna walilopungukiwa kama nchi.....na diplomasia yao inashamiri.
hivyo nikijibu swali la mtoa mada kwamba magufuli ni mbumbumbu wa Diplomasia? Jibu ni Hapana. Ushahidi niliouweka hapo unaonyesha ANAFANYA mambo ipasayo.‎
‎
‎
‎
Tatizo la UKAWA Genieous wao ni MBOWE NA SUGU.Think Tank ni KUBENEA.Mtu wa Elimu ya HAPA NA PALE.Unategemea nini cha maana.
 
jose eduardo dos santos ... wamekaa sana haga wakati wanapigania uhuru ....na kina augustino neto ,baadaye nchi ikaingia vita ya wenyewe kwa wenyewe akipigana na JONAS SAVIMBI ....wakati huo alikuwa anasafiri sana ,siku hizi amepunguza au hasafiri kwa kuwa umri wake umesogea sana ..na offcourse baada ya amani uchumi umekuwa mzuri sana ...sana .

Rais wa zamani wa Kenya , Jomo Kenyatta alikuwa akisema wazi kuwa hapendi kusafiri kwakuwa ukiacha umri kusogea alikuwa anakiri kuogopa ndege ....na ziara zake nyingi za nje alikuwa akifanya makamu wake wakati huo ...DANIEL TOROITICH ARAP MOI
Mkuuu Philomon nikuhakikishie kuwa do santos hawahi kukaa Tanzania kabisa pia simsikiagi akisafirisafiri hata UN new huwa haendi
 
ImageUploadedByJamiiForums1455183757.247687.jpg
ImageUploadedByJamiiForums1455183775.281012.jpg
 
Back
Top Bottom