Determinantor
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 61,438
- 100,721
Nina uhakika Magufuli anaogopa yasijekumkuta ya Tshingarai alipokuana na Markel, jamaa anaelekezwa huku yeye anafanya hivi, jitahidi uione video just incase hukuiona.
Jibu hoja wewe mfagia choo cha Lumumba. Lowasa au ufisadi umeingiaje? Hivi mnatumia mi.ku and.u kufikiri? Kuwa mstaarabu hasa wewe yehodaya.Kama Magufuli hajui diplomasia basi Diplomasia unaijua wewe na wana UKAWA wenzio mliosimama na kuitangazia dunia kuwa Lowasa FISADI papa halafu baadaye mkasema tena Lowasa SI FISADI afaa kugombea uraisi.Nyie ndio wana diplomasia
Watu wengine bwana!
Sasa wewe mwerevu wa Diplomasia uko wapi?
Ikulu ni Taasisi!
Toka Magufuli aingie madarakani kama Rais wa Tanzania, mwenendo mzima wa Diplomasia ya Tanzania umekuwa tata kabisa. Tanzania kwa sasa ameanza kupoteza taswira nzima ya Diplomasia ya mambo ya nchi za nje na pia katika utatuzi wa migogoro, iwe ya kisiasa au kisheria.
Hapa chini ni mifano michache ya matukio ya kustaajabisha yaliyofanywa na Serikali ya Magufuli katika Nyanza ya Diplomasia ambayo yamezaa maswali makubwa sana.
1/Magufuli amegoma kusafiri nje ya nchi ili kwenda kuhudhuria mikutano ya Wakuu wa nchi na badala yake amekuwa akituma wawakilishi.
2/Magufuli ameandaa Hafla ya mabalozi Ikulu lakini akakimbia kuhudhuria hafla hiyo.
3/Magufuli ametoa jibu la utatuzi wa mgogoro mkubwa wa kisiasa Zanzibar pasipo kufanya majadiliano ya usuluhishi na pande zinazovutana.
4/Serikali ya Magufuli(Kupitia kwa wasemaji wake) imesema haiwajibiki kuingilia kutatua mgogoro wa kisiasa Zanzibar lakini itawajibika wakati wote kupeleka askari polisi na askari jeshi ili kuzima ghasia zozote zinazotokana na mgogoro wa Zanzibar.
5/Magufuli amesema tayari anajua hukumu za Mahakamani kuhusu kesi zinazoendelea zinazohusu wadaiwa wa Serikali kabla ya hizo kesi kusikilizwa au kwisha!!
4/Serikali ya Magufuli(Kupitia kwa wasemaji wake) imesema haiwajibiki kuingilia kutatua mgogoro wa kisiasa Zanzibar lakini itawajibika wakati wote kupeleka askari polisi na askari jeshi ili kuzima ghasia zozote zinazotokana na mgogoro wa Zanzibar.
namba 3 na 4 ni vigumu kuelewa unakusudia nini lakini kuna kaui ilitolewa na mwanasheria mkuu wa serikali kuhusu raisi Magufuli kujiingiza kwenye uchaguzi huo.
Magufuli ameomba aachwe kwa muda kama wa miezi 6 ili asuke nchi. Kwa hali ilivyokuwa Waziri wa mambo ya nje alikuwa hana kazi maana aliyekuwepo Ikulu alikuwa anaifanya hiyo kazi, na ilifika mahali mabalozi wa nje wakaona kama Ikulu ndiyo wizara inayowahusu, Wizara ya mambo ya kigeni wao walikuwa kama tarishi tu! Ikulu ilikuwa na wageni wa kila aina mpaka wacheza mpira wa vikapu!
Kwa mtazamo wa jicho la tatu, Magufuli anataka apitie kila kitu na ajiweke sawa 'kimfumo' na atakapoanza kukutana na watu wa nje (mabalozi wakiwemo) ajue anataka nini (ambacho amekosa nchini). Ombaomba inafedhesha, inavunja heshma ya nchi na watu wake. Tanzania tunaomba misaada mingine ya aibu kabisa - msaada ya kuweka vidumu ya maji ya kunawa mikono watoto shuleni wanapotoka maliwatoni!
Lakini pia naamini Magufuli anashindwa kuongea mambo mengine hadharani lakini upo uwekezakano amekuta mafaili yamejaa kila kona ya 'jumba jeupe' huku yakiwa hayajafanyiwa kazi! Mwenyeji wa zamani alikuwa na muda mchache sana nchini na hivyo hakuweza kufanya mambo mengi!!! Mambo mengine ni yanasikitisha kidogo lakini ndio hivyo.
NB: Rais wa Botswana vipi, na unaonaje mambo ya Botswana!
Hushangai hawa walisema kashfa ya Richmond ni ajali ya kisiasa na wakampigia debe 2010 ubunge na leo kahamia Chadema mnamsema vingine?Kama Magufuli hajui diplomasia basi Diplomasia unaijua wewe na wana UKAWA wenzio mliosimama na kuitangazia dunia kuwa Lowasa FISADI papa halafu baadaye mkasema tena Lowasa SI FISADI afaa kugombea uraisi.Nyie ndio wana diplomasia
Watu walishazoea kumwona mzee wa kiguu na njia sasa wamebaki wanashangaa.
Miaka kumi ya uongozi wa mzee Mwai Kibaki alisafiri nje ya Kenya mara 13 tu. Ndiyo aliyejenga uchumi imara ambao Uhuru Kenyatta bingwa wa kusafiri anauharibu kwa speed kubwa kabisa. Rushwa imekuwepo siku zote Kenya lakini hii ya sasa ni balaa kwa vigezo vyovyote vile. Fuatilia makala za David Ndii kwenye gazeti la Nation.
Kwa kutumia mtazamo wa Lumumba huwezi kuelewa kitu! Kwa hiyo usijaze server bure!
Eti mwanasheria Mkuu wa serikali kwani umesika kunatengenezwa Katiba mpya?
Hushangai hawa walisema kashfa ya Richmond ni ajali ya kisiasa na wakampigia debe 2010 ubunge na leo kahamia Chadema mnamsema vingine?
View attachment 322565
Mkuu wa nchi atasafiri pale itakapobidi! Kwa sasa hana incentive ya kwenda nje, wakati watu wingi wapo wanaweza kumweakilisha.
Halafu hili si swala la kujadili kitaifa kama vile lina tija yoyote. Watu wanapenda kuongea kirahisi rahisi tu! Alishasema, nchi ipo katika majanga mengi; uchumi mbovu na matatizo mengi ya wananchi ambayo yanatakiwa kutatuliwa ili tufike mahala tufanye miradi ya maendeleo na si kutatua kero zisizoisha daima.
Mlizoea kiongozi wa nchi anakimbia kimbia matatizo myumbani kwake, anatatua ya wengine, ukweli ni kwamba rais huyu atakubukwa kwa kuleta mabadiliko ya ukweli, ambayo kila mmoja atayaona,.
Kwanini wananchi wasitulie na kufanya kazi ili waone uzuri wa Tanzania? Hatutaenda kuomba tena! watakuja wao hapa, tumuunge mkono mwokozi huyu wa wananchi.
Mkuu kweli kabisa ndio maana nikasema kuna watu bado wana fikra za kitumwaWatu walishazoea kumwona mzee wa kiguu na njia sasa wamebaki wanashangaa.
Miaka kumi ya uongozi wa mzee Mwai Kibaki alisafiri nje ya Kenya mara 13 tu. Ndiyo aliyejenga uchumi imara ambao Uhuru Kenyatta bingwa wa kusafiri anauharibu kwa speed kubwa kabisa. Rushwa imekuwepo siku zote Kenya lakini hii ya sasa ni balaa kwa vigezo vyovyote vile. Fuatilia makala za David Ndii kwenye gazeti la Nation.
Mkuu, mimi nimewahi kusema kwenye mijadala mingine kwamba watanzania tuna budi kusimama na kujisifu kwa Amani na utulivu wetu tulio nao maana naamini kabisa ingekuwa nchi zingine kuna watu leo hii wangakuwa kizuizini na wasisikike tena.
Adui wa maendeleo ni baadhi ya watanzania wenzetu, sasa ni wakati wa kuwatafuta popote walipo na kuwashughulikia.
Tuchape kazi tuirudishe nchi kwenye mstari.