Magufuli ndie Rais bora Afrika na Duniani

Magufuli ndie Rais bora Afrika na Duniani

britanicca

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2015
Posts
17,211
Reaction score
41,788
RAIS BORA AFRICA
Leo tukipewa nafasi ya kuchagua kiongozi bora Africa na duniani. Nitakuchagua Rais wangu Mhe. Dr. John Joseph Pombe Magufuli. Sababu za kukuchagua;
1. Mpaka hivi sasa umerejesha thamani ya utumishi wa umma.
2. Umepambana na mafisadi na wabadhirufu kwa vitendo
3. Umetekeleza sera ya viwanda kwa vitendo.
4. Umeboresha miundo mbinu (fly overs zinajengwa, Standard gauge kwa Upande wa Reli, maboresho ya viwanja vya ndege na shirika la ATCL)
5. Umetekeleza ahadi ya Elimu bure kwa vitendo.

Hizi sababu 5 kila moja inazaa faida zaidi ya 20. Hivyo tunayo sababu kubwa ya kukuamini na kukupenda.

Watanzania pamoja na maboresho hayo bado nchi yetu ina changamoto nyingi ambazo ili tukabiliane nazo tunahitaji ushiriki wetu kwa kuiunga mkono serikali yetu. Hata nchi Zenye uchumi mkubwa kama Marekani hazikosi Changamoto na ndo maana zina vyama vya upinzani. Changamoto hizo haziwafanyi waandamane au kuitukana serikali Yao. Changamoto zao ndo zinawaunganisha na kuwafanya kuwa taifa lenye nguvu duniani. Hivyo lazima kama taifa tuisaidie serikali yetu katika utatuzi wa Changamoto zinazotukabili

FB_IMG_1521350077304.jpg
 
Njaa zako ndo zinakusumbua ili ujikombe
1. Thamani ipi unaizungumzia nilipo mimi maji, barabara, elimu bado ni kero au utumishi wa umma upi??
2. Ufisadi upi natunawaona mafisadi yana peta
3.Viwanda au vi-wonder
4.hizo flyovers, standard gauge bado hazijakamilika so piga kimya
5.Hii elimu bure ndo kafeli michango daily lasivyo tukubali watoto wetu wapate zero
 
Akili yako imejaa ujuha na unafki. Lengo lako ni kujikweza na kulamba miguu ya watu wala huu sio uchambuzi.
-Vipi kuporomoka kwa uchumi?
-Vipi mauaji utesaji na utekaji wa watu?
-Vipi Uhuru wa habari?
-Hivyo ulivyovitaja kuna hata moja matunda yake yanaonekana?
-Wewe unapigana na benki ya dunia?
-Wewe unapingana na wachumi wa dunia?

Nimalizie tu kwa kusema kwamba ujinga wako utakuumbua siku moja, sijui utakimbilia wapi.Njaa yako ndio shida yako.
 
Wewe ndo mjinga coz hujui thamani ya ulichonacho. Wasomi ndo wanajua thamani ya magufuli, kama umewahi kutoka nje ya nchi basi utagundua huyu ndo rais anayetufaa, ila kama hujavuka boda my friend mtamlaumu sana anko magu. Hii ndo life style ya nchi zote zilizoendelea.
Tulia wewe mammalia tokea lini dikteta likawa na thamani?
 
Ni maoni yako mkuu, upo huru kumsifia katika kila kitu na ni muhimu pia umjuze wapo watakaomkosoa katika kila kitu. Tubishane kwa hoja, nchi hii ni yetu sote.
 
RAIS BORA AFRICA
Leo tukipewa nafasi ya kuchagua kiongozi bora Africa na duniani. Nitakuchagua Rais wangu Mhe. Dr. John Joseph Pombe Magufuli.
Naunga mkono hoja na hata Katto hili analijua.

Ni ukweli usiofichika kuwa rais Magufuli is the best that we have, kwa kanuni ya penda chako.

The best mother duniani ni mama yako,
The best father ni baba yako.
The best wife ni mkeo/memo
The best country ni Tanzania,
The best president ni Magufuli.
P.

Rais Magufuli ni Simple, Genuine & Down To Earth-He is Simply A Man of The People!

Magufuli Kama Nyerere: Ni Mtu wa Watu, Hapapasi, Hamung'unyi, Ni Kazi Tuu, Ila Pia sio Kama Nyerere!
 
Anajitahidi. Hebu tuorodheshe viwanda vilivyoanza kipindi chake. Viwanda in pamoja na miundombinu na mikakati kadhaa ya kufanikisha hvyo viwanda - umeme, wataalamu , masoko na nk. Lasivyo tunaweza kuwa tuna zalisha bidhaa zisizotakiwa popote au zenye ubora duni kulinganisha na zizalishwazo penginepo duniani naviwanda vyetu kufa. Au gharama zetu za kuzalisha zikawa Juu kulinganisha na bidhaa kutoka nje. Tutakuwa tumefanya nini?

Viwanda sio bora viwanda. Ifikie na sisi bidhaa zetu za viwandani zijae kwenye mitaa ya kenya, Malawi, Zambia, Kongo na kwingineko kama vile bidhaa za Kenya na afrika kusini zinavyojaa kwenye mitaa ya Tanzania. Hapa sijasema bidhaa za uchina. Na inabidi tulenge mbali. Kwa mtazamo wangu kuna Nazi Kubwa na umakini mkubwa unatakiwa kufika huko

Akifanikiwa kuhakikisha madini tunafaidika NAyo nitamuona wa maana. Maana madini yalipaswa yawe mtaji wetu wa kufikia huo uchumi wa viwanda. Mabwge yalivyokuwa hayajui mahesabu hayo ukichanganya na uzuzu, ulafi, tamaa, kibri, hila na fitina Kwa miaka kadhaa yaakaachia madini yetu Yachukuliwe na wazungu bure kabisa tens Kwa miaka mingi.

kwa madini yaliyochukuliwa tungelipwa Hela Nzuri na hao wazungu hiyo Hela mida hii ndio ingetumika kuwa na umeme mzuri wa uhakika, Maji , miundombinu mingine, nguvu kazi yenye ujuzi na maarifa na nk.

First things first. Mi siamini kama hii kauli mbiu ya uchumi wa viwanda ni sahihi kihivyo. Uchumi wa viwanda sio wa vuuup huo umefika katika miaka mitano. Ni wa maandalizi. labda Yeye ndo anaweka / aweke msingi wa kuelekea huko.

unataka kutengeneza Nguo lakin Kwa miaka sasa viwanda vya urafiki na mwatex etc vilishakufa. Hamna mashine, wataalamu na umeme unalalamikiwa kuwa ni ghali na nk. Viwanda vilivyopo ni vidogo kiuwezo . sasa utahakikishaje urafiki na mwatex vinaanza kazi kiushindani dhidi ya nguo kutoka nje katika kipindi cha miaka 5? Hivyo vilivyopo vya binafsi utafanyaje viongeze uwezo wake katika miaka 5?

Viwanda ni maandalizi. waulize wachina walifikaje pale fasta vile
 
Hivi huyu britanicca si amewahi kutapeli watu humu? Naomba mwenye uzi ule ausasicrybu hapa..
 
RAIS BORA AFRICA
Leo tukipewa nafasi ya kuchagua kiongozi bora Africa na duniani. Nitakuchagua Rais wangu Mhe. Dr. John Joseph Pombe Magufuli. Sababu za kukuchagua;
1. Mpaka hivi sasa umerejesha thamani ya utumishi wa umma.
2. Umepambana na mafisadi na wabadhirufu kwa vitendo
3. Umetekeleza sera ya viwanda kwa vitendo.
4. Umeboresha miundo mbinu (fly overs zinajengwa, Standard gauge kwa Upande wa Reli, maboresho ya viwanja vya ndege na shirika la ATCL)
5. Umetekeleza ahadi ya Elimu bure kwa vitendo.

Hizi sababu 5 kila moja inazaa faida zaidi ya 20. Hivyo tunayo sababu kubwa ya kukuamini na kukupenda.

Watanzania pamoja na maboresho hayo bado nchi yetu ina changamoto nyingi ambazo ili tukabiliane nazo tunahitaji ushiriki wetu kwa kuiunga mkono serikali yetu. Hata nchi Zenye uchumi mkubwa kama Marekani hazikosi Changamoto na ndo maana zina vyama vya upinzani. Changamoto hizo haziwafanyi waandamane au kuitukana serikali Yao. Changamoto zao ndo zinawaunganisha na kuwafanya kuwa taifa lenye nguvu duniani. Hivyo lazima kama taifa tuisaidie serikali yetu katika utatuzi wa Changamoto zinazotukabili

View attachment 718140
😀 Watanzania wana safari refu lakini watafika,Mkuu umeshawahi kutembea nchi nyengine za Afrika ukaona nini kinaendelea??Magufuli ni raisi wa mwisho katika Afrika hamfikii hata Uhuru Kenyatta,Huwezi kumsifu raisi, anaewanyanyasa raia wake,anaewabagua raia wake,Flying Over kitu gani kama raia hawana furaha..
 
Mayalla kuna kanafasi unakanyemelea?
Mkuu Tea Bag, hakuna kanafasi chochote ninacho kanyemelea, bali siku zote mimi ni mkweli daima.

Ni ukweli usiofichika kuwa rais Magufuli is the best that we have, kwa kanuni ya penda chako.

The best mother duniani ni mama yako,
The best father ni baba yako.
The best wife ni mkeo/memo
The best country ni Tanzania,
The best president ni Magufuli.
P.
 
Naunga mkono hoja na hata Katto hili analijua.

Ni ukweli usiofichika kuwa rais Magufuli is the best that we have, kwa kanuni ya penda chako.

The best mother duniani ni mama yako,
The best father ni baba yako.
The best wife ni mkeo/memo
The best country ni Tanzania,
The best president ni Magufuli.
P.

Rais Magufuli ni Simple, Genuine & Down To Earth-He is Simply A Man of The People!

Magufuli Kama Nyerere: Ni Mtu wa Watu, Hapapasi, Hamung'unyi, Ni Kazi Tuu, Ila Pia sio Kama Nyerere!
nakushauri uirudie ile ID yako ya pasco
that way utakuwa huru zaidi
 
Wewe ndo mjinga coz hujui thamani ya ulichonacho. Wasomi ndo wanajua thamani ya magufuli, kama umewahi kutoka nje ya nchi basi utagundua huyu ndo rais anayetufaa, ila kama hujavuka boda my friend mtamlaumu sana anko magu. Hii ndo life style ya nchi zote zilizoendelea.
Kuvuka nje ya nchi kwenda wapi?

Tena kwa aliyesafiri kidogo tu kufika hapo Kenya hawezi kusema haya uyasemayo.

Raisi mwenye wakuu wa mikoa wanaotukana watumishi wa umma.

Nchi yenye watawala badala ya watumishi wa umma.

Nchi inayokandamiza demokrasia?

Nchi iliyojitoa kwenye makubaliano ya kuongoza serikali kwa uwazi (transparency)?

Ni wapi huko unataka twende ili tuone mema ya Magufuli.

Kawasema waliosaini mikataba ya madini ofisini yeye karudia kulekule..hakuna mwananchi (au tuseme tu hata mbunge) anayejua makubaliano mapya yapoje. Kweli kuna maendeleo unayoyategemea?

Hebu nishawishi kabla hujatutukana eti hatujasafiri ndiyo maana.

Ni kweli kusafiri na kusoma vitabu ni njia bora sana za kupanua wigo wa kufikiri lakini raisi wako tu hayo ameyakosa. Sidhani hata kama huwa anasoma Biblia ukiachia vitabu vingine.

Am sorry mkuu nisije mtukana raisi...ameshindwa kuongoza.
 
Back
Top Bottom