SANCTUS ANACLETUS
JF-Expert Member
- Mar 5, 2016
- 3,337
- 4,664
Tunaposema na kuvaa ujivuni juu ya kuzawadiwa imani Katoliki tunafanya hivyo baada ya tafakari ya kina sana.Baadhi yetu tunatembea kifua mbele na ujivuni wenye upole na unyenyekevu kwa kutambua kuwa ukweli,amani,utulivu,mshikamano,maendeleo na mapinduzi yoyote ya kitekenolojia ambayo dunia inayapitia sehemu kubwa chimbuko lake ni Kanisa Katoliki.
Leo nimebahatika kupata Kitabu ambacho kinachimbua historia ya Mtakatifu Petro,Mkuu wa Kwanza wa Kanisa lake Kristu,Kanisa Katoliki.Kitabu kimeandikwa na Mwanafasihi Padri Stefano Kaombe,wa Jimbo Kuu la Dar es salaamu.Sitaki kujadili kwa undani jinsi alivyomchambua Mt.Petro( Baba Mtakatifu wa Kwanza) kadri anavyoelezwa na Wainjili wanne kutoka Maandiko Matakatifu, bali nataka kumshukuru Mungu kwa jinsi anavyoweza kutung'amurisha mambo mbalimbali maishani mwetu kwa namna ya ajabu sana.
Ni hivi: dibaji ya Kitabu hicho " Mfahamu Mtakatifu Petro anavyosimuliwa na Wainjili" imeandikwa na John Pombe Joseph Magufuli.Ni muumini wa Kanisa Katoliki.Ni huyu huyu Raisi wa Tanzania.
Baada ya kusoma kitabu hicho juu ya tabia za Mtakatifu Petro na kuoanisha na tabia za Magufuli,ndipo nikang'amua jinsi Roho Mtakatifu anavyotimiza ahadi yake ya kulisaidia na kulitegemeza Kanisa kila wakati kwa namna ya ajabu sana.Sijui Mwandishi (Pd.Kaombe) akiulizwa ni kitu gani kilimfanya amchague Magufuli ndiye awe mwandishi wa Dibaji ya Kitabu chake atasemaje. Lakini mimi nimeng'amua kuwa pamoja na sababu zozote zinazoweza kutolewa na Mwandishi,ni Roho Mtakatifu kupitia Mwandishi amependa kumuimarisha na kumkamilisha Magufuli katika kazi ya uongozi wa nchi yetu kwa yeye kumsoma Mt.Petro na kisha kuandika kwa usuli juu ya kiongozi kama yeye,Petro,Kefa.
Ukisoma dibaji ya Magufuli katika Kitabu hicho utagundua ni Mtu mwerevu sana.Ni mtu ambaye anacho kipaji cha kuweza kuchambua mambo na akayapa tafsiri chanya kabisa! Uwezo na karama hii wamepewa wachache lakini kwa faida ya wengi.
Mtakatifu Petro,kwa muhutasari alikuwa na sifa zote chanya na hasi.Aliishi kama mtu jasiri.Alikuwa mwepesi wa kukubali majukumu yoyote aliyopewa na aliyoona ni stahili yake kuyahudumu.Mtakatifu Petro,aliifanya vizuri sana kazi ya utume na ya uongozi wa Kanisa.Ni yeye aliweka misingi ya Kanisa tunalojivunia Leo.Petro alichukua uongozi wa Kanisa katika kipindi kigumu sana wakati huo.Petro aliachiwa uongozi wa Kanisa kipindi ambacho "mafisadi" wa imani ya Ukiristo mayahudi na dola ya Kirumi(kisiasa) walikuwa hawana mchezo na yeyote anayejaribu kuhatarisha maslahi yao.Lakini kwa nguvu ya Roho Mtakatifu kazi ya Petro matunda yake ndio tunajivuni nayo Leo.
Magufuli,alikubali kuandika dibaji ya kitabu kinachomwongelea kiongozi mwenzake (lakini Kiroho) pengine bila kujua kuwa anaweka summary juu ya mtu anayefanana naye kitabia.Na pengine hajalitambua hilo hadi wakati huu kitabu kinapokuwa sokoni.Pd.Kaombe pengine aliliona hilo kwa msaada wa Roho Mtakatifu na ndio kisa akamtwisha kazi hiyo.
Magufuli ni Kimbelembele sana kama alivyokuwa Petro.Magufuli ni mkurupukaji na mropokaji kama alivyokuwa Petro.Magufuli ni jasiri sana na yuko tayari kuchukua maamuzi yoyote madhali anaona mbele ya maamuzi hayo iko nuru.Petro alitawaliwa na tabia kama hii.Petro alikubali hata kutolewa uhai wake kwa ajili ya imani Katoliki isitawi.Magufuli alikubali kuachana na kujitenga na "falsafa" ya chama chake ya kuwajali matajiri na wenye fedha na kuwageukia maskini na wasio na tumaini.Yeye Magufuli anachukua toka mikono ya matajiri na kuweka katika mikono ya maskini.Anavua "samaki" kwa ajili ya wasio na kitoweo.Petro naye alikubali kuboresha kazi yake ya uvuvi toka ya kuvua samaki kwenda kuwa ya kuvua watu.Kazi ya kuhudumia watu kiroho na kimwili.Kazi ya kuchambua,kufafanua,kufundisha maadili na tunu za kimwili,kiakili na kiroho.Magufuli anaweka misingi ya utajirisho wa Tanzania.Anabadili Mikataba yenye masharti hasi.Anawaweka pembeni viongozi wenye mwelekeo hasi kihuduma za kijamii,kiuchumi na kisiasa.
Magufuli amefanana na Mt.Petro kwa majukumu yao.Wote walichukua majukumu ya kuongoza jamii zao katika vipindi vigumu sana.Kwa Magufuli,nchi yetu ilikuwa ni nchi iliyokosa mwelekeo baada ya kuondoka Mwalimu Nyerere.Nchi ilifikia kuwa mithili ya Lori linaloendeshwa na walevi.
Baada ya kusoma,kitabu hiki cha Pd.Kaombe nimepata mang'amuzi makubwa sana juu ya Magufuli na jinsi ambavyo Pd.Kaombe amekusudia kumuimarisha Magufili katika uongozi kwa kumukumbusha historia ya Kiongozi wa jamii kama yeye,Mt.Petro.
Nitaandika siku zijazo Kitabu juu ya Magufuli kuchambua ufanisi wake na kushindwa kwake kama ishara ya kumuunga mkono Pd.Kaombe.Historia za viongozi waliowahi kuishi huko nyuma zina mchango mkubwa sana katika kutuimarisha na kutuongoza nasi katika kazi zetu na wajibu wetu wa Leo.Na hiki ndicho alichokifanya Fr.Kaombe.
Basi nawaalikeni kwa mjadala.