Magufuli na Mt.Petro: "majabali" Wawili katika enzi tofaiti.

Nimekosea kabisa kuingia hapa japo ni mkatoliki tena katekista na nina kigango changu nakisimamia

Tatizo la wakatoliki ni unafki na kujipendekeza

Yale maharage ya Gwajima aliyokula Pengo unataka kutulisha na sisi
 
Tuuchukue huo "unafiki" wa Wakatoliki kama kioo cha kutusaidia kubaini pa kurekebisha kwenye nyuso zetu.Ni hilo tu mkuu.Hongera kwa "kumiliki" kigango! Kigango kama hicho kiko chini ya Kanisa Katoliki chini ya Mt.Petro wa ukweli au wa ""pentekoste na uhamusho"?
 
Tanzania ya Mtakatifu Pombe Yatoa msaada Marekani na Ulaya.

No matter how evil money is,but being broke is not holly.
 
Tanzania ya Mtakatifu Pombe Yatoa msaada Marekani na Ulaya.

No matter how evil money is,but being broke is not holly.

Ukiacha na mwanadamu ambaye amepewa nyenzo ya utashi wa kujua mema na mabaya hakuna kiumbe kingine katika ulimwengu wetu kinaweza kuwa najisi au evil! Sio pesa,chakula,mavazi,wala malazi.Sio Mbuzi,Paka,Kenge au mjusi.Isipokuwa sisi binadamu ndio tunaweza kuukwaa unajisi au udhambi kupitia viumbe wengine.Ukitumia panga kuua pangi haliwi najisi na wala haliwezi kuwa na dhambi ya kufanya mauaji.
 
Namna gani naweza kupata hicho kitabu Mkatoliki mwenzangu

Sent from my TECNO L8 Lite using JamiiForums mobile app
 
Hakuna mtakatifu hapa duniani ila Mungu Baba wa Mbinguni tu..
Warumi 3:10-12
 
Namna gani naweza kupata hicho kitabu Mkatoliki mwenzangu

Sent from my TECNO L8 Lite using JamiiForums mobile app

Mkuu kinapatikana pale Cathedral Bookshop,opposite na St.Joseph.Lakini pia unaweza kukipata Bookshop ya Msimbazi Centre.Unaweza kuja inbox nikupatie picha ya jinsi kinavyofafana.Hongera kwa kutaka kujisomea.Padri Matumaini leo katika Homilia yake pale Kanisa Kuu, amesisitiza juu ya watu kupenda kujisomea.Kaenda mbali kwa kubainisha kuwa akili ya binadamu asiyependa kujisomea iko kama maji yaliyotulia.Maji yasiyotembea muda mrefu uishia kunuka.Hutunga hatimaye utando ("usaha") na magugu kuota juu yake na hivi kupoteza rangi yake ya asili.Na Kilele cha maji kama hayo ni kugeuka kuwa mazalia ya Mbu na Vimelea mbalimbali vituleatavyo magonjwa anuai.

Basi nakupongeza sana kwa kutamani kufanya "Maji" ya akili yako yakae yakititiririka.
 
Hakuna mtakatifu hapa duniani ila Mungu Baba wa Mbinguni tu..
Warumi 3:10-12

Mimi sijasema Mt.Petro yuko duniani.Huyo yuko Mbinguni.Utakatifu ni taji tunayovikwa huko Mbinguni baada ya kazi zetu hapa duniani.Ni cheti tunachotuzwa baada ya kufaulu mtihani wa wito wetu wa maisha hapa duniani.Kama ujuavyo wahitimu hawako vyuoni tena bali mitaani na makazini.Kwa hiyo mada yangu haijamchora Magufuli kama Mtakatifu bali mtu anayelingana kwa tabia na mwenendo sawa na Mt.Petro.
 
Back
Top Bottom