Magufuli na Kamanda Sirro wanaamini wataweza kuwafunga gerezani wote wanaowakosoa??

Ki Mun

JF-Expert Member
Oct 6, 2014
3,443
4,386
1. Zitto Kabwe
2. Fatma Karume
3. Freeman Mbowe
4. Tundu Lissu
5. Jenerali Ulimwengu
6. Askofu Gwajima
7. Godbless Lema
8. Dk. Helen Kijo-Bisimba
9. Waandishi mbalimbali wa habari​

Kila kukicha sauti za wakosoaji dhidi ya utawala wa Rais Magufuli zinaongezeka, na badala ya Mh Rais kujiuliza kwanini wakosoaji wanaongezeka, yeye na polisi wake wanaona njia rahisi ni kuwaandama wakosoaji kwa kuwafungulia mashtaka na kuwafunga gerezani(labda)....hivi wanaamini kabisa kwamba wataweza kuzima sauti zote za wakosoaji dhidi ya utawala huu?
 
1. Zitto Kabwe
2. Fatma Karume
3. Freeman Mbowe
4. Tundu Lissu
5. Jenerali Ulimwengu
6. Askofu Gwajima
7. Godbless Lema
8. Dk. Helen Kijo-Bisimba
9. Waandishi mbalimbali wa habari​

Kila kukicha sauti za wakosoaji dhidi ya utawala wa Rais Magufuli zinaongezeka, na badala ya Mh Rais kujiuliza kwanini wakosoaji wanaongezeka, yeye anaona njia rahisi ni kuwaandama wakosoaji kwa kuwafungulia mashtaka na kuwafunga gerezani,labda....hivi wanaamini kabisa kwamba wataweza kuzima sauti zote za wakosoaji dhidi ya utawala huu?
Kukosoa hakujazuiwa ila wakosea kwa mantiki na sio kwa kufanya uchochezi kwa kisingizio cha kukosoa. Uhuru usio na mipaka ni sawa na uendawazimu
 
Uchochezi is subjective. Kwako Uchochezi maana yake ipi?

Kwa Kamanda Siro na Magufuli anayetoa hoja zinazoelekea kuwaaminisha raia kuwa maamuzi mengine ya serikali na raisi sio sahihi ana fit the profile ya kuwa mchochezi.

Kwako mchochezi ina tafsiri gani?Mchochezi anamchochea nani kwa nani?Anayechochewa ana akili timamu au hana akili timamu kupambanua kama huo ni uchochezi?...@Kalulukalunde
 
Katika karne ya 21 (tofauti na karne ya 20 na kurejea nyuma enzi za ujima), kitendo cha kuzuia fikira mbadala ni sawa na kujaribu kuzuia mkondo wa maji yanayotiririka kutoka vilimani na kuelekea sehemu tambarare.

Kama JPM na watu wanaomzunguka wangelitambua hili, kitu ambacho wangeamua kufanya si kuzuia flow ya fikira mbadala bali ni kuweka 'miundombinu' ya kuziongoza ama kuzielekeza hizo fikira mbadala zitiririke katika utaratibu wenye tija.

Mbinu mojawapo ya kuwezesha fikira mbadala kutiririka katika utaratibu wenye tija ni kuachia Bunge likawa huru. Wakati Ukuta.
 
mti ukimwagiliwa maji lazima ukue. kwa hivi tatizo si mti kukua bali wanaoumwagilia!
 
1. Zitto Kabwe
2. Fatma Karume
3. Freeman Mbowe
4. Tundu Lissu
5. Jenerali Ulimwengu
6. Askofu Gwajima
7. Godbless Lema
8. Dk. Helen Kijo-Bisimba
9. Waandishi mbalimbali wa habari​

Kila kukicha sauti za wakosoaji dhidi ya utawala wa Rais Magufuli zinaongezeka, na badala ya Mh Rais kujiuliza kwanini wakosoaji wanaongezeka, yeye na polisi wake wanaona njia rahisi ni kuwaandama wakosoaji kwa kuwafungulia mashtaka na kuwafunga gerezani(labda)....hivi wanaamini kabisa kwamba wataweza kuzima sauti zote za wakosoaji dhidi ya utawala huu?
Ukiwazuia hawa mawe yataongea.
 
Kukosoa hakujazuiwa ila wakosea kwa mantiki na sio kwa kufanya uchochezi kwa kisingizio cha kukosoa. Uhuru usio na mipaka ni sawa na uendawazimu
Uchochezi ni upi ktk kuchambua bajeti au kueleza wanavyominywa bungeni?
 
Yangu macho tu, sielewi Tanzania yetu inakoelekea. Naona mambo yanabadilika kila uchao
 
Tatizo ukosoaji wa uchochez hautakiwi

Uchochezi una maana gani kwako?Kwangu kwa mfano ulichokiandika hapo juu ndio uchochezi wenyewe wa kuchochea kuaminisha watu kuwa mawazo mbadala ni uchochezi...Kwako uchochezi ni nini ndugu?
 
Inanikumbusha enzi za utawala wa makaburu kule South Africa (kipindi cha ubaguzi wa rangi). Wazalendo kibao wakiwemo wanasiasa kama Nelson Mandela, Oliver Tambo, Solomon Mahlangu, wanamuziki kama Lucky Dube na wengineo wengi walirundikwa magerezani lakini mwisho wa siku utawala wa Makaburu uliondolewa. Baba Je.sca atawafunga jela watanzania wengi sana lakini 2020 hawezi kurejea madarakani. Tumechoshwa na utawala wa kiimla.
 
1. Zitto Kabwe
2. Fatma Karume
3. Freeman Mbowe
4. Tundu Lissu
5. Jenerali Ulimwengu
6. Askofu Gwajima
7. Godbless Lema
8. Dk. Helen Kijo-Bisimba
9. Waandishi mbalimbali wa habari​

Kila kukicha sauti za wakosoaji dhidi ya utawala wa Rais Magufuli zinaongezeka, na badala ya Mh Rais kujiuliza kwanini wakosoaji wanaongezeka, yeye na polisi wake wanaona njia rahisi ni kuwaandama wakosoaji kwa kuwafungulia mashtaka na kuwafunga gerezani(labda)....hivi wanaamini kabisa kwamba wataweza kuzima sauti zote za wakosoaji dhidi ya utawala huu?
Nakumbuka Amini aliweza kufanya hilo through mass killings! Waganda wakanyamaza mpaka leo!
 
Katika karne ya 21 (tofauti na karne ya 20 na kurejea nyuma enzi za ujima), kitendo cha kuzuia fikira mbadala ni sawa na kujaribu kuzuia mkondo wa maji yanayotiririka kutoka vilimani na kuelekea sehemu tambarare.

Kama JPM na watu wanaomzunguka wangelitambua hili, kitu ambacho wangeamua kufanya si kuzuia flow ya fikira mbadala bali ni kuweka 'miundombinu' ya kuziongoza ama kuzielekeza hizo fikira mbadala zitiririke katika utaratibu wenye tija.

Mbinu mojawapo ya kuwezesha fikira mbadala kutiririka katika utaratibu wenye tija ni kuachia Bunge likawa huru. Wakati Ukuta.

Nadhani Jamii yetu inamapungufu ya kusoma nyakati na psychology ya binadamu. Binadamu ni kiumbe wa ajabu sana. Unapo mlazimisha aendane na mawazo yako wakati akili yake haiko tayari kupokea hayo ni lazima atatafuna namna ya kuhakikisha kuwa hawezi kutawaliwa na mawazo yako. Hiyo ni historia ya nature. Unapomnyima uhuru wa kutoa mawazo yake hadharani lazima atatafuta platform nyingine ili kuwasilisha mawazo yake kwa wahusika. Nadhani Siro na bwana mkubwa wanamapungufu kwenye kuelewa dunia ya leo inaendaje?
 
Back
Top Bottom