Magufuli mwaka 2016, tutauza Ulaya mitumba, mwaka 2020 mnipe awamu nyingine tutauza mitumba Ulaya

The Assassin

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
4,416
17,501
Hua nawauliza watu ni vitu gani tangible Magufuli amefanya cha maana kwa miaka 5 iliyopita chenye kuboresha au kuongeza pato la mwananchi mmoja mmoja, utajibiwa tu flyover, ndege, Stiglers, SGR na kuhamia Dodoma. Unashindwa kuelewa hivi vitu vimewasaidiaje wananchi wa kawaida?

Kule kanda ya Ziwa toka wamevuna pamba hakuna mnunuzi, ziko store tu na watu wengine hawajalipwa toka mwaka jana serikali ilichukua pamba zao na kuwazulumu pamba zao kama ilivyokua kwenye korosho.

Kwenye korosho miaka 2 sasa watu wanadai zaidi ya Billion 20 hawajalipwa toka 2018 baada ya serikali kukopa korosho zao.

Mwaka 2016 tuliambiwa tutaanza kuuza mitumba ulaya na kua donor country, mwaka 2019 tukaambiwa Tanzania imejenga viwanda 4000, hivyo viwanda havijulikani vilipo ila kwenye takwimu za serikali vipo na vimeajiri watu milioni 6 ila takwimu za utumishi recruitment portal zinasema kwa miaka 5, wametangaza kazi chini ya elfu 10 na wameomba kazi watu zaidi ya laki 8, yaani kwa wastani kazi zote zilizotangazwa na watu walioajiriwa ni 1%.

Kama viwanda vya kuchakata pamba havipo hiyo mitumba tutakayouza ulaya ni ipi?
 
Back
Top Bottom