Magufuli Mitano Tena

Testar

JF-Expert Member
May 30, 2015
7,461
12,218
Ndio ukweli huo, mtu apende ama asipende Ila ndo hivyo. Tofauti na wagombea wengine, JPM ataendelea kuwa Rais hadi 2025.

Sababu za kumpa ushindi ni nyingi wala hazihesabiki, akianguka sana ni amepata robo tatu(75%) ya kura zote. Kwa hiyo ni uamuzi wa wapiga kura kuweka kura zao kwenye kapu la ushindi ama kuzitoa kafara.

Kuhusu wapinzani, kwanza watambue hamasa yao mitandaoni hailandani na uhalisia wa mitaani. Pili wasikate tamaa maana uchaguzi ni haki yao. Tatu, wawe tayari kukubali na kusaini karatasi za matokeo.

Kwa wale wanaopingana na huu uzi niwasihi wazitunze comments zao hadi mwezi November.

_109217029_magufuli.jpg
 
Bora nikampigie kura Hashimu Rungwe Spunda ambaye anatambua ni nini hasa mwanadamu anacho kihitaji zaidi katika maisha yake! CHAKULA! Ila siyo huyo anayewaza kununua tu ndege na kujenga flyovers akiamini ndiyo maendeleo ya kweli.

Tumchague ili iweje? Tuendelee kuishi kama mashetani halafu yeye mwenyewe, familia yake, watu wake wa karibu, marafiki zake na vibaraka wake ukiwemo wewe mtoa mada, ili tu muendelee peke yenu kufaidi mema ya nchi hii kwa kupitia njia ya kizamani na ya kinafiki ya kumlamba miguu yake!!

Big NO
 
Bora nikampigie kura Hashimu Rungwe Spunda ambaye anatambua ni hasa mwanadamu anacho kihitaji. Ila siyo huyo dikteta wenu uchwara...
Ni haki yako kumpigia kura umtakaye, kwani 2015 ulimpigia nani kura?

Mimi sinufaiki chochote kibinafsi kutoka kwake, nimeamua kusema ukweli usiokuwa na illusion.
 
Miaka mitano mingine kusagia meno.... Bora kura yangu niitupe chooni kuliko kumpa Jiwe.
 
]
Kwa aliye timamu kumkichwa haiingii akilini kuamini eti Magufuli atakuwa one term President Tena katika nyakati ambapo wapinzani wanawayawaya kisiasa.

Hata wapinzani wanalitambua hilo sema hawataki kuacha gap 2020.
 
Kwa aliye timamu kumkichwa haiingii akilini kuamini eti Magufuli atakuwa one term President Tena katika nyakati ambapo wapinzani wanatembea kwa kuchechemea...

Najua Wewe ni mwana CCM Mwenzangu ila neno lako la 'Dhihaka' la Wapinzani 'Wanachechemea' ukimlenga Tundu Lissu sijalipenda. Tubu sasa!!!
 
Najua Wewe ni mwana CCM Mwenzangu ila neno lako la 'Dhihaka' la Wapinzani 'Wanachechemea' ukimlenga Tundu Lissu sijalipenda. Tubu kwa Mola!
Mkuu kumradhi kama ndivyo nilivyoeleweka.
Niwe mkweli sina hulka ya kufurahia matatizo kwa binadamu yeyote! hata Kama ni adui yangu, nimewahi kupitia magumu mbalimbali hivyo natambua umuhimu wa kumuhurumia kila anayeteseka.

La muhimu Nampeda sana Tundu Lisu.Nimewahi kukutana naye live kama mara mbili na naweza kumwelezea kama mtu mzuri. Hata sasa hivi huwa nafuatilia na kuangalia video zake japo kumsikia tu. Anajua kujenga hoja, na ana rekodi nzuri ya kutetea wanyonge, hata ikitokea asiwe kiongozi wa kitaifa, Tundu Lisu ameshaweka alama nzuri kwenye historia ya nchi yetu.

Kuchechemea kwa wapinzani ni kisiasa wala siyo kiafya.
 
Ndio ukweli huo, mtu apende ama asipende Ila ndo hivyo. Tofauti na wagombea wengine, JPM ataendelea kuwa Rais hadi 2025.

Sababu za kumpa ushindi ni nyingi wala hazihesabiki, akianguka sana ni amepata robo tatu(75%) ya kura zote. Kwa hiyo ni uamuzi wa wapiga kura kuweka kura zao kwenye kapu la ushindi ama kuzitoa kafara.

Kuhusu wapinzani, kwanza watambue hamasa yao mitandaoni hailandani na uhalisia wa mitaani. Pili wasikate tamaa maana uchaguzi ni haki yao. Tatu, wawe tayari kukubali na kusaini karatasi za matokeo.

Kwa wale wanaopingana na huu uzi niwasihi wazitunze comments zao hadi mwezi November.

View attachment 1538043
Haaaahaaaaa
 
Ndio ukweli huo, mtu apende ama asipende Ila ndo hivyo. Tofauti na wagombea wengine, JPM ataendelea kuwa Rais hadi 2025.
Yamekuwa hayo tena...mtu apende asipende! Kumbe hakuna tena cha uchaguzi wala nini. Sawa. Laiti mngekuwa mnasoma historia msingetoa kauli hizi za hatari. Kumbe heri hata Polepole aliyekiri kwamba uchaguzi ukiwa huru na wa haki, CCM isahau ushindi.

Napata shida kidogo hapa CHARMILTON, naomba unisaidie. Ina maana hata akijitoa mtamlazimisha? Aliwahi kulalamika kuwa mwaka 2015 mlimsukumizia, je safari hii mtatumia mbinu gani? Hivi mnayo habari kwamba Mungu naye yupo na kuna mapenzi yake?

Mathalani kwa kuwa ni tupende tusipende, je tusiopenda mtatufanyaje? Je tuhame nchi au tayari dawa yetu iko jikoni ikichemka? Naomba sana utudokezee ndugu yetu kama sisi wengine tuanze kufungasha virago! Tupende tusipende, kumbe ndio maana! Ole wetu!
 
Ndo hivyo Mkuu, maana halisi ya uchaguzi ni kupenda na kutokupenda kwa watu. Mwaka 2015 zaidi ya watu milioni sita hawakupenda Dr Magufuli awe Rais, lakini haikumzuia Magufuli kuwa Rais. Haikuwa chuki bali mapenzi ya watu kwenye uwanja wa demokrasia.

Uwezekano wa JPM kujitoa kwenye huu uchaguzi ni mdogo Sana, sawa na hakuna. Hata Kama atapenda kujitoa bado Hana huo uwezo. Ukipitia maandiko matakatifu utaona Nabii Musa alivyokuwa mbishi mbele za Mungu, alitoa sababu mbalimbali kwanini hafai kuwa kiongozi wa Wana wa Israeli lakini Mungu akamsukumiza kuwa kiongozi wa kuwavusha waisaeli kwenye nyakati zilizokuwa ngumu. Hata hivyo Musa hakupendwa na waisraeli wote wakiwemo ndugu zake wa karibu kabisa.

Mungu mwenyewe aliyeumba kila kitu, kila mtu hapendwi na watu wote, sembuse Rais Mwanadamu? Kumpenda ama kutokumpenda mtu ni haki ya kila mwenye moyo, kila mtu atapita lakini nchi itabaki...kwahiyo kuwa huru kuifurahia nchi kwa kadiri ya Yale uyapendayo.
 
Back
Top Bottom