Magufuli kwa miaka 3 katunga sheria nyingi kumnyima raia uhuru kuliko marais wote toka Nyerere hadi Kikwete

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Muingereza kabla hata hajatupa Uhuru alitutungia sheria ya makosa ya adhabu(penal code) ambayo baadae ikaja weka vipengere vya makosa ya uchochezi na udhalilishaji.

Tulipopata tu uhuru,tukatungiwa sheria ya usalama wa taifa iliyoweka mipaka ya taarifa ipi ni ya umma na ipi ni ya siri?

Tukaja tukatungiwa sheria ya magazeti ambayo ikawa inayafungia magazeti ambayo hayajawapendezesha wakubwa.

Baadae tukatunga sheria nyingine ambayo ikawapa nguvu mamlaka kuvifungia vyombo vya habari vya kielektroniki.

Baadae tukatunga sheria ya kuzuia kutoa takwimu ambazo hazijathibitishwa na serikali

Baadae tukatungiwa sheria inayoweka utaratibu wa kupata taarifa.

Baadae tukatungiwa sheria inayompa mkuu wa mkoa ama wilaya kukufukuza kwenye eneo lake.

Sasa tunasheria inayotukataza kuchambua takwimu Rasmi za serikali kwa lengo la kuonesha kuwa hazipo sawa.

Sasa tunasheria inayokataza kufanya utafiti bila ruhusa ya serikali.

Haya mambo hayaaaaaaa.
 
Bandiko hili ni copy & paste toka kwa Dotto Bulendu wa Star TV Facebook wall page yake toka juzi, ulipaswa uandike source ya habari yako kama wewe siyo Dotto mwenyewe, ila kama wewe ni dotto mwenyewe haina shida.

Nikija kwenye hoja ya Uzi huu ni kweli kabisa kwenye utawala wa Rais Magufuli Sheria nyingi sana kandamizi dhidi ya Uhuru wa raia zimetungwa ili kunyamazisha wakosoaji wa rais na utawala wake kwa ujumla, kwa mantiki hiyo huyu ni rais muoga na dhaifu sana kuliko wote waliomtangulia
 
Kwakweli hatutaisahau awamu hii na wastahafu wote wa awamu hii kuanzia wakuu wa wilaya wataangaliwa vibaya sana kila atakaeseema Mimi nilikuwa DC au rc kipindi cha jpm tutamuuliza nyie ndio mliotesa na kuteka RAIA?

Nyie ndio mliolisulubisha taifa?

Nyie ndio mlioonea wafanyakazi ?

Nyie ndio mlifunga taifa midomo kwa manufaa yenu?

Nyie ndio mliofukuza watu kazi waliobakisha mwaka mmoja wa kustahafu bila kuwalipa mafao yao ?

Hakika tutawakumbuka kwa mengi mno bila kumsahau Ben SAA nane na azory waliotoweka kama nabii eliya
 
Wanatunga sheria kama hizo ili wakisema uongo usikanushe au kufuatilia ukweli, sijui wao ni Mungu kwamba hawakosei
 
Bandiko hili ni copy & paste toka kwa Dotto Bulendu wa Star TV Facebook wall page yake toka juzi, ulipaswa uandike source ya habari yako kama wewe siyo Dotto mwenyewe, ila kama wewe ni dotto mwenyewe haina shida.

Nikija kwenye hoja ya Uzi huu ni kweli kabisa kwenye utawala wa Rais Magufuli Sheria nyingi sana kandamizi dhidi ya Uhuru wa raia zimetungwa ili kunyamazisha wakosoaji wa rais na utawala wake kwa ujumla, kwa mantiki hiyo huyu ni rais muoga na dhaifu sana kuliko wote waliomtangulia
We jamaa ni mtata
 
Muingereza kabla hata hajatupa Uhuru alitutungia sheria ya makosa ya adhabu(penal code) ambayo baadae ikaja weka vipengere vya makosa ya uchochezi na udhalilishaji.

Tulipopata tu uhuru,tukatungiwa sheria ya usalama wa taifa iliyoweka mipaka ya taarifa ipi ni ya umma na ipi ni ya siri?

Tukaja tukatungiwa sheria ya magazeti ambayo ikawa inayafungia magazeti ambayo hayajawapendezesha wakubwa.

Baadae tukatunga sheria nyingine ambayo ikawapa nguvu mamlaka kuvifungia vyombo vya habari vya kielektroniki.

Baadae tukatunga sheria ya kuzuia kutoa takwimu ambazo hazijathibitishwa na serikali

Baadae tukatungiwa sheria inayoweka utaratibu wa kupata taarifa.

Baadae tukatungiwa sheria inayompa mkuu wa mkoa ama wilaya kukufukuza kwenye eneo lake.

Sasa tunasheria inayotukataza kuchambua takwimu Rasmi za serikali kwa lengo la kuonesha kuwa hazipo sawa.

Sasa tunasheria inayokataza kufanya utafiti bila ruhusa ya serikali.

Haya mambo hayaaaaaaa.
Kwa hiyo Magufuli hafai Kabisa wewe ndiyo unafaa.
 
Madikteta kama jiwe siku zote hawajiaamini ndo maana umeona huyu kichaa ametunga sheria nyingi za kutubana mpaka uhuru wa kutoa maoni yetu wale wachumia tumbo wakazipitisha bungeni madhara yake ni makubwa sana
 
Inakuja sheria ya kulazimisha kila mwananchi kuzisoma taarifa na takwimu za serikali

Back
Top Bottom