Magufuli kagua Pamba road Mwanza

Magufuli kagua Pamba road Mwanza

Marire

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2012
Posts
12,333
Reaction score
5,312
salaam wakuu.
kama mh magufuli anapita humu jf naomba aje atukagulia hii barabara ya pamba road maana hawa jamaa sijui kama ujenzi wao upo sahihi,kwa macho yangu ya nyama naona ni mchezo japo si mtaalam wa haya mambo.
wamepiga viraka kila mwaka zaidi ya mara tatu inabomoka sasa hivi pale mbele ya kituo cha polisi kijipande kidogo tu wamepaki hapo magari na ujenzi umesisi week sasa na magari ni taabu tupu njia ya bugando ndio inatumika na wagonjwa wanapitishwa huko huko.
_chini ya mh magufuli uzembe huu haukubaliki na hauvumiliki.
kampuni ni JESCO...
_NB:Nakupongeza kwa daraja la mabatini na taa za buzuruga japo foleni ndio imezidi pale...
POMBE MAGUFULI HOYEEEE
 
Kwa hapa mwanza barabara nyingi ni uozo mfano pale kemondo,hapo pamba road, na barabra ya lumumbu kuanzia hapo nono supermarket mpaka kule kinyatta road, yani nashangaa hili jiji sijui jiji gani?!!!
 
nitafanyeje mh waziri ajue hii kero?
 
Kwa hapa mwanza barabara nyingi ni uozo mfano pale kemondo,hapo pamba road, na barabra ya lumumbu kuanzia hapo nono supermarket mpaka kule kinyatta road, yani nashangaa hili jiji sijui jiji gani?!!!

Yaani ni shidaaa, imagine huko ni katikati ya Jiji, sisi wa mihama, lumala, Kiseke hata hatuongei tunasubiri kudra za uchaguzi mkuu ujao, hiyo barabara ya pamba imeshakuwa kero tunaongea hakuna anaetusikiliza acha waendelee kula
 
Hii barabara ya Pamba juzi tu ilimalizika ujenzi baada ya jesco kukaa hapo miezi Sita na zaidi wakakabidhi eti juzi imeharibika wamerudi hao jesco na hakuna wanachofanya ni kuweka vibao vya diversion eti kuna ujenzi unaenda lea,
 
Back
Top Bottom