idoyo
JF-Expert Member
- Jan 13, 2013
- 3,051
- 1,423
Hapo kabla alisema anazijua shida za wananchi na yupo tayari kuzitatua. Jana kasema atatumia usafiri wa gari ili ajue kero za wananchi. Teh!
Na pale jangwani alisema anashangaa miaka yote hamna kiwanda cha kusindika samaki, wakati yeye alishawahi kuwa waziri wa maendeleo ya mifugo na uvuvi. Siasa bwana!
Na pale jangwani alisema anashangaa miaka yote hamna kiwanda cha kusindika samaki, wakati yeye alishawahi kuwa waziri wa maendeleo ya mifugo na uvuvi. Siasa bwana!
MGOMBEA nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, amesema anazijua shida zote za Watanzania hivyo, atasimama imara katika kuzitatua na kuweka wazi kwamba, kwa muda wa miaka 20 aliyokaa Serikalini hakuwahi kushindwa.
Shida ya kwanza ni Laptop kwa Walimu ambayo atahakikisha kila mwalimu awe primary au secondary lazima awe na Laptop.
Shida zingine zilishatatuliwa na Raisi kikwete na Maraisi wengine waliopita, yeye atakachokifanya ni kuendeleza tuu., yaani " Sitawaangusha hawa maraisi waliopita" Alisema Dr. J.P. Magufuri.
Dk. Magufuli aliyasema hayo jana, wakati akizungumza na wazee na wanachama wa CCM wa Mkoa wa Dar es Salaam, baada ya mapokezi yaliyofanyika kwa kurudisha fomu ya urais, huku akibainisha kuwa, atashirikiana na mgombea mwenza wake kuhakikisha wanatatua shida za Watanzania.