Magufuli ima madaraka yamemzidi ukubwa au amelewa madaraka

JERUSALEMU

JF-Expert Member
Sep 19, 2012
3,112
3,536
Salamu wanajamvi!
Nimemfuatilia Magufuli toka anaapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Tanzania hadi juzi. Amebadilika sana kisiasa na kimwili. Siyo yule wa November, 2015.kimwili amezeeka haraka sana hata kimuonekano anamzidi Jakaya Mrisho Kikwete. Kwanini? Hili nitaliongelea muda ukifika.

Kisiasa unaweza kusema ameota mapembe, hamsikilizi yeyote awae! Ni kama amejiweka madarakani.Moyoni hana hofu yoyote, hamuogopi hata Mungu an ndio maana hana huruma kwa mtu yeyote awe mwanafunzi, mtumishi wa umma, wana siasa wenzeke, raia yeyote , yeye anajali urais wake na namna ya kudumu katika u Rais huo. Hachagui maneno! Liwe jema au baya hilo halimpi shida.

Watu wanao muudhi sana ni wale wanao mkumbusha uwepo wa KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO.Ni kama anatamani kuifuta.kwake yeye KATIBA inamchelewesha kufika anako taka japo siyo kwa masilahi ya Nchi. Anatamani matumizi ya fedha apange yeye wapi zikatumike.Mambo ya Bunge anaona yanamchelewesha tu bila sababu.ndio maana ana weza kwenda mahali katika ziara zake akaahidi kuwa pelekea hata shs bilioni 5 ambazo Bunge halija pitisha.

Kitendo cha kumlinda Makonda kwa sababu yoyote ili ni dalili za kulewa madaraka. Lakini 2020 atarudi tena kutuomba kura. Hapo ndio atajua yeye hana u Mungu wowote, ni bora angekuwa mnyenyekevu kwa watu. radio , magazeti na Tv zote hazitakuwa upande wake.
 
Na hivi sasa yeye anajiona ndiyo EACH and EVERYTHING.......

Kwa mazingira haya sioni hata sababu ya Lema kusota rumande kwa miezi 4 ambapo alichokisema ni UKWELI MTUPU.......
 
Mwaka 2020 atapita kwa kishindo kwa sababu
  1. Elimu ya uraia vijijini haipo. Wengi wanajua upinzani ni vita, CCM ni amani.
  2. Kuna mtaji wa umasikini miongoni mwa watanzania. Itakuwa rahisi kuendelea kurubuniwa.
  3. Mikutano ya kisiasa ya vyama vya upinzani imepigwa pini hadi 2020
  4. Dola, mahakama na vyombo vya ulinzi viko chini ya atakayekuwa anapigania kiti chake.
  5. Tume ya uchaguzi itakuwa hii hii. Itafanya yale yale ya lubuva.
 
Tatizo watanzania tuliowengi tu wanafiki sana na huwa tunalalama sana mitandaoni tu....Kwa jinsi nchi inavyooenda tungekuwa kama hata majirani zetu ungekuta watu washajaa barabara zote za kila mkoa....Na cha ajabu 2020 utashangaa atashinda kwa 80%.....hii ndo Danganyika....
 
Kuna makabila Mwl Nyerere alisema ni hatari kupewa madaraka . Naona usemi wake kama kuna ka ukweli fulani hivi.
 
Sijui hata atafikaje huko 2020....
Com wamuondoe haraka kabla hajaharibu zaidi nchi yetu nzuri
 
Tatizo watanzania tuliowengi tu wanafiki sana na huwa tunalalama sana mitandaoni tu....Kwa jinsi nchi inavyooenda tungekuwa kama hata majirani zetu ungekuta watu washajaa barabara zote za kila mkoa....Na cha ajabu 2020 utashangaa atashinda kwa 80%.....hii ndo Danganyika....
Tumejengewa uwoga ndomana hatuwezi kufanya hivyo. Huwezi kumshinda adui yani polisi wanaobeba mitutu huku raia hata jiwe lenyewe huna
 
Mwaka 2020 atapita kwa kishindo kwa sababu
  1. Elimu ya uraia vijijini haipo. Wengi wanajua upinzani ni vita, CCM ni amani.
  2. Kuna mtaji wa umasikini miongoni mwa watanzania. Itakuwa rahisi kuendelea kurubuniwa.
  3. Mikutano ya kisiasa ya vyama vya upinzani imepigwa pini hadi 2020
  4. Dola, mahakama na vyombo vya ulinzi viko chini ya atakayekuwa anapigania kiti chake.
  5. Tume ya uchaguzi itakuwa hii hii. Itafanya yale yale ya lubuva.
Wananchi wakiamua hakuna linaloshindikana. Unayosema wewe hata Gambia yalisemwa hivyo hivyo, lakini Yahya Jameh alitolewa madarakani. Sasa hivi mawasiliano yapo juu sana, watu wengi wanaelemika juu ya umuhimu wa kiongozi na kufanya uchaguzi uliosahihi, kwa hiyo usibaki na mentality kama hiyo tena kwani haitawork 2020.
 
Mtanyooka tu, na kuzoea tu

Na bado, mlizoea yale sasa ni hapa kazi tu

JPM oyeeeeeee
Makonda oyeeeee
 
e19f9d141872ee4473b7a81dd8d2cfdb98fdd226655e7dadbd213f8ad3817086.jpg
 
Acheni unafiki kwani alipokuwa anamteua nape kuwa waziri mlimpangia nyie? Wacha achape kazi bana. JPM hoyeee. Endeleza Vita ya madawa ya kulevya naona wengi hawaipendi kabisa kwa kisingizio cha kuwa clouds fm imevamiwa. Toweni tafsiri ya neno uvamizi na kisha je kiongozi wa serikali akitembelea sehemu ni uvamizi?.
 
Tatizo watanzania tuliowengi tu wanafiki sana na huwa tunalalama sana mitandaoni tu....Kwa jinsi nchi inavyooenda tungekuwa kama hata majirani zetu ungekuta watu washajaa barabara zote za kila mkoa....Na cha ajabu 2020 utashangaa atashinda kwa 80%.....hii ndo Danganyika....
Mambo mengine bora uwe mpole tu. Nape pamoja na kuwa ni Mhe. kaomba kitambulisho kaoneshewa mtutu, sasa wewe mwenzangu na mimi ukakae barabarani unajitaka kweli?
 
halafu sijui kwa nini kila akiongea ni lazima atufokee...yaani fulu kufokafoka
 
Back
Top Bottom