Bonde la Baraka
JF-Expert Member
- Sep 22, 2016
- 4,580
- 7,943
Rais Magufuli , pamoja na ugumu wa maisha kwa wananchi na watumishi wa serikali lakini bado tunatumaini kwamba una nia njema.
Kuna mtumishi tangu tarehe 16/05/2017 alipopata posho (lunch) hajaonekana kazini mpaka leo yapata wiki moja sasa. Akipigiwa simu na wafanyakazi wenzake hapokei na leo kaizima kabisa, huyu mtu leo akiupokea mshahara basi ni mtihani tena, maana lazima aongeze tena siku kadhaa mbele. Meneja kampigia simu hampati.
Rais naomba uendelee kupembua hawa watumishi , naamini watumishi kama hawa wako ndani ya taasisi nyingi za umma na ndio wanaokwamisha juhudi za nchi hii kufikia adhma ya kujitegemea. Meneja ama mkurugenzi ana mamlaka ya kudhibiti pahala pamoja tu, lakini wewe ukitamka neno linakuwa amri na sheria kwa nchi nzima, na tutakaobaki tuboreshee maslahi maana hali ya maisha hailingani na maisha kwa sasa.
Thanks.