Magufuli hakujiandaa kuwa rais, atatuangusha tu

Huu ndo mjadala unaopendeza, unatoa hoja unarudishiwa hoja sio matusi utafikiri tupo vijiweni.
 
Atakapoanza kampeni tarehe 22 mwezi huu ndipo mtajua kuwa jamaa alikuwa amehifadhi nondo a.k.a madini yake na atakuwa akiyatoa hadi nyie watu wa chadema na ukawa mtabadili uamuzi na mtampigia kura wenyewe. Kwani si hata mkapa alipopitishwa na ccm mlikuwa mnamdharau hivi hivi lakini aliposhika tu nchi je mafanikio tuliyaona au hatukuyaona? Psychologically binadamu wamegawanyika katika makundi haya mawili ya kitabia " extroverts " na " introverts " ambapo extroverts ni waropokaji, wazungumzaji na wataka sifa na publicity na hapa lowassa wenu ndiyo mahala pake lakini introverts huwa ni wataratibu, wana uhakika, wanajiamini na huwa na upeo mkubwa na akili nyingi na hapa magufuli ndiyo mahala pake.
Kwa hiyo Mkapa alileta maendeleo? Mimi nilisikia aliuza mashirika na benki kwa bei ya kutupa, akafanya biashara akiwa ikulu, akanunua rada kwa bei ya juu, engineer wa EPA, kajibinafsishia mgodi wa kiwira, akajiuzia nyumba za serikali, akaanzisha kampuni ya biashara akiwa ikulu, akawaua wapemba baada ya kuwapora ushindi wao mwaka 2001 akitengeneza wakimbizi wa kitanzania kwa mara ya kwanza katika historia.

Mashinery atakayoitumia Magufuli ili kutawala(CCM) hata ufanyaje haiwezi deliver, it is rotten to the core huwezi aminisha watu kuwa itaweza engineer mabadiliko positively labda negatively, jawabu ni rahisi piga chini CCM introverts wakajenge Lumumba
 
Waliishatafuta muda mrefu mafisadi wa kuwasupport hivyo tayari wana mtaji wa urais na wanajua ni namna gani watarejesha kwa wafadhiri wao wakiupata urais.

Kama kuna mtu hakujiandaa huyo ndiye anafaa kuwa Rais maana hana deni na mtu.Ogopa sana kwenye ncgi zetu maskini kuwa na Rais aliyeununua urais.

Mnaposema amenunua uraisi hivi mliona risiti au ni hearsays tu?
 
unavyo tolea mfano mkapa kuhusu mafanikio ni sawa mafanikio yalikuwepo sana kwann ucmtolee mfano huyu aliko sasa hivi??????
 
Jiongeze kiakili, hayo makundi yaliyojiandaa ndio hatari kwa nchi yako,endelea kushangilia kibwege wakati wenzako wako kwenye biashara ya kununua nchi.

Tuliishajifunza makundi yaliyomnunulia urais Kikwete yalivyosumbua ili yalirudishe pesa zao,baada ya kukosana na Kikwete yakahamia huku na sasa kwa nguvu kibwa zaidi wamewekeza kwa Lowassa na Mtanzania mzalendo eti anaona fahari kuwa na urais wa kununua.Kama una watoto pole yao.Tumepewa vichwa ili tufikiri na sio kufugia nywele.

Hivi kwa nini iwe like moja tu? Nilitaka kuongeza nyingine imekataa!
 
Mambo mengine ya ajabu sana mkuu, miaka takribani nane watu wanaimba, ufisadi, ufisadi, jamani ufisadi. Kikwete na ccm yake kaamu haya ngoja tufanye maamuzi ya kijasiri Dodoma, Maana kilichofanywa Dodoma lazima kuwa na Roho ya jasiri kwelikweli.

Sasa waimba kupinga ufisadi ndio namba moja kukumbatia ufisadi. Sikutegemea hata siku moja kuwa tuna baadhi ya wanasisa bogus wa kiwango cha juu kiasi hiki tunacho kishuhudia sasa.
Kwa hiyo unataka kutuaminisha aliyekatwa ndiye fisadi ndani ya CCM? Kwa miaka takriban nane ambayo alikuwa nje ya serikali ufisadi ulikoma?

Alihusika na ESCROW, mabehewa mabovu TRC? EPA,uuzaji wa nyumba za serikali? Ikulu wako hasa msemaji wake Salva Rweyemamu hujibu mapema sana tuhuma zinazohusisha Ikulu ili akina Tomaso tujiridhishe mbona kakaa kimya baada ya EL kusema mamlaka ya juu(JK) ndiyo ilihusika kulazimisha mkataba wa RICHMOND usainiwe,sasa tumemjua mwenye dili hebu tuaminishe katika tuhuma lukuki za ufisadi zilizotokea hapa nchini na EL. Kama huna basi kaa kimya
 
Dunia hii ina maajabu mengi sana!
Kuna siku rangi zitabadirishwa majina yake, bluu itaanza kuitwa nyekundu, nyekundu itaitwa njano, njano itaitwa kijani!
Jua litaitwa mvua na mvua itakuwa jua!
 
Kila ninapomsikia Magufuli akisema Sitawaangusha nabaki kucheka tu
Sote tunajua Magufuli anataka kuwa rais kwa 'ajali' tu..hana dira wala maono ya kiongoz mkuu wa nchi zaid ya kusubiri ilani ya CCM kama anavyosema kila siku..kwa kukosa dira binafsi ni wazi atatuangusha tu kwa sababu HAKUJIANDAA
Sheria inamzuia kuanza Kampeni. Subiri muda wa Kampeni uanze.
 
Fisadi Kikwete anataka kutuwekea boya ili limlinde kwa ufisadi aliofanya na mwanaye Riziwani. Bahati nzuri Mungu akatupa Watanzania jembe liitwalo Edward Ngoyai Lowassa
 
Upo sahihi kabisa, sasa wanachotaka ni kuwapa promotion wezi ili kujenga utamaduni kwenye nchi kuwa unaweza ukaiba/kufisadi utakavyo alafu wakati wa uchaguzi ukamwaga pesa na Watanzania walivyo wajinga watakushangilia na utashinda.

Hii ndio imefanya ufisadi ushamiri,na leo waliokuwa wanapaswa wawe wazalendo eti wamegeuka wapiga debe wa wezi walewale, hii haitaishia hapa,itawatafuta wenyewe wanaoshangilia leo, itabidi tukubaliane kama taifa baada ya hapa kuwa ufisadi sasa ni ruksa,tusisikie tena kelele za watu kulialia juu ya ufisadi maana kwa matendo yao wanaonyesha wanapenda watu wanaofanya hayo.

Watu ata hawajiulizi yule mtu waliyekuwa wanamsifu humu kama makini na mzalendo, Dr Slaa,kwanin kagoma?wanaishia kama watoto wadogo kujijibu kwa majibu marahisi..uchu wa urais, kweli ni rahisi sana kuyatawala mazuzu.

Kenyatta aliwahi kumtania Nyerere kuwa anatawala maiti zisizojitambua,kwa hili naanza kumuunga mkono Jomo Kenyatta, hawa watu sio wazima.

Ndugu yangu usitu tusi watanzania tafadhali sana.....hata huyo kenyata mtoto wake alituhumiwa kuwa ni muuaji ktk fujo za 2008 na pia familia yake ni FISADI lkn wakenya wakayawoka hayo pembeni then wakachagua mtu ambaye atawasogeza parefu kutoka hapo walipo
 
Jiongeze kiakili, hayo makundi yaliyojiandaa ndio hatari kwa nchi yako,endelea kushangilia kibwege wakati wenzako wako kwenye biashara ya kununua nchi.

Tuliishajifunza makundi yaliyomnunulia urais Kikwete yalivyosumbua ili yalirudishe pesa zao,baada ya kukosana na Kikwete yakahamia huku na sasa kwa nguvu kibwa zaidi wamewekeza kwa Lowassa na Mtanzania mzalendo eti anaona fahari kuwa na urais wa kununua.Kama una watoto pole yao.Tumepewa vichwa ili tufikiri na sio kufugia nywele.

Vizuri sana umeweza kugundua Kuwa kikwete pia aliwekwa kwa hela kwahiyo ushindi wake ulikuwa wa kutumia hela yani ushindi wa kununua kama umsemavyo huyu wa ukawa

Sasa unawaambia nini wana ccm kuhusu rais wao alie madarakani Kuwa alinunua urais na alipaswa kulipa madeni ya waliomnunulia urais huo

Huoni Kuwa unazunguka palepale kwa kusema eti huyo anaetaka urais kwa kununua atalipa madeni

Au ndio upungufu wa muono fikra na kujielewa kwako???
 
Magufuli kuna wakati anaongea as if he is under the gun point! Hana collocation kabisa na vision!
 
Msitutoe kwenye hoja za msingi. Awe amejiandaa au hakuandaliwa, matatizo yanayolalamikiwa na wananchi wengi hayajaletwa na Magufuli, yameletwa na mfumo mbovu wa CCM. Yeyote anayesimama kutetea mfumo huo hatapata kitu mwaka huu. Hiyo ndiyo point. Msitupotezee muda kujadili kuandaliwa au kutoandaliwa. Hiyo siyo ajenda ya wapiga kura.
 
Kwa hiyo unataka kutuaminisha aliyekatwa ndiye fisadi ndani ya CCM? Kwa miaka takriban nane ambayo alikuwa nje ya serikali ufisadi ulikoma?

Alihusika na ESCROW, mabehewa mabovu TRC? EPA,uuzaji wa nyumba za serikali? Ikulu wako hasa msemaji wake Salva Rweyemamu hujibu mapema sana tuhuma zinazohusisha Ikulu ili akina Tomaso tujiridhishe mbona kakaa kimya baada ya EL kusema mamlaka ya juu(JK) ndiyo ilihusika kulazimisha mkataba wa RICHMOND usainiwe,sasa tumemjua mwenye dili hebu tuaminishe katika tuhuma lukuki za ufisadi zilizotokea hapa nchini na EL. Kama huna basi kaa kimya

Hakuwa fisadi pekee ni mmoja wao, ndiposa maandiko matakatifu ya nasema rushwa hupofusha na wewe imekupofusha

Unataka kutumia muendelezo wa rushwa kama dekio la kumsafisha mmoja wao. Hizo skandali ulizo taja ni baada ya Nyerere kufa. Huyu superstar wa ufisadi hata Nyerere alikufa akiwa na records zake.
 
MAFUNGUO HANA MVUTO MBELE YA WANANCHI HANA USHAWISHI WOWOTE NI VIGUMU SANA KUIONA MAGOGONI LABBA APITE PALE MBELE NA GARI YAKE YA TINTED RAISI HUWA HAOKOTWI BALI LAISI ANAANDALIWA MAFUNGUO KAOKOTA DODO WE UMAFIKIL ANGEIPATA MH MEMBE HII NAFASI UNGEONA CHECHE ZAKE NA UNGE AMINI KWELI HUYU MTU ALIKUWA ANAUTAKA URAIS SIO HUYO FUNGUO WENU....poleni sana kwakupewa kiongoz asiye na mvuto kwa taifa hii ni hasara kubwa sana ya CCM
 
Msitutoe kwenye hoja za msingi. Awe amejiandaa au hakuandaliwa, matatizo yanayolalamikiwa na wananchi wengi hayajaletwa na Magufuli, yameletwa na mfumo mbovu wa CCM. Yeyote anayesimama kutetea mfumo huo hatapata kitu mwaka huu. Hiyo ndiyo point. Msitupotezee muda kujadili kuandaliwa au kutoandaliwa. Hiyo siyo ajenda ya wapiga kura.

Tunataka mtoke muwaambie wananchi huyo ambaye mlizunguka nchi nzima mkiwaaminisha kuwa ni fisadi kageuka vipi ghafla kuwa mgombea wenu wa urais? Malaika wa safari ya uhakika, looh! Duniani kote maajabu haya ya unafiki wa kisiasa ulikomaa yanapatika Tanzania tu.

Hatutaki kusikia hizo hoja zenu dhaifu za kuokoka kisiasa. Wapinzani wa siasa Tanzania mmegekuka kuwa kichekesho eti sasa kuna waongofu wa kisiasa na wanapatikana kambi ya upinzani.

Kuokoka kuko makanisani tu. Acheni utapeli wa kisiasa.
 
MAFUNGUO HANA MVUTO MBELE YA WANANCHI HANA USHAWISHI WOWOTE NI VIGUMU SANA KUIONA MAGOGONI LABBA APITE PALE MBELE NA GARI YAKE YA TINTED RAISI HUWA HAOKOTWI BALI LAISI ANAANDALIWA MAFUNGUO KAOKOTA DODO WE UMAFIKIL ANGEIPATA MH MEMBE HII NAFASI UNGEONA CHECHE ZAKE NA UNGE AMINI KWELI HUYU MTU ALIKUWA ANAUTAKA URAIS SIO HUYO FUNGUO WENU....poleni sana kwakupewa kiongoz asiye na mvuto kwa taifa hii ni hasara kubwa sana ya CCM

Na ndio maana mlimuundia wizara ya kitowewo kwa kuwa mlijua ni tishio kwa upm wenu na bado aka perform, mkatoka serikalini mkamuacha akiwa anaendelea kufanya utumishi wake ulio tukuka kwa wananchi.
 
Atakapoanza kampeni tarehe 22 mwezi huu ndipo mtajua kuwa jamaa alikuwa amehifadhi nondo a.k.a madini yake na atakuwa akiyatoa hadi nyie watu wa chadema na ukawa mtabadili uamuzi na mtampigia kura wenyewe. Kwani si hata mkapa alipopitishwa na ccm mlikuwa mnamdharau hivi hivi lakini aliposhika tu nchi je mafanikio tuliyaona au hatukuyaona? Psychologically binadamu wamegawanyika katika makundi haya mawili ya kitabia " extroverts " na " introverts " ambapo extroverts ni waropokaji, wazungumzaji na wataka sifa na publicity na hapa lowassa wenu ndiyo mahala pake lakini introverts huwa ni wataratibu, wana uhakika, wanajiamini na huwa na upeo mkubwa na akili nyingi na hapa magufuli ndiyo mahala pake.

La Brujita kumbe tuko pamoja, asante cz umenisemea....its like u were in my thought
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom