Magufuli hakujiandaa kuwa rais, atatuangusha tu

Magufuli hakujiandaa kuwa rais, atatuangusha tu

Mtaka yote

Senior Member
Joined
Nov 30, 2014
Posts
136
Reaction score
103
Kila ninapomsikia Magufuli akisema Sitawaangusha nabaki kucheka tu.

Sote tunajua Magufuli anataka kuwa rais kwa 'ajali' tu..hana dira wala maono ya kiongozi mkuu wa nchi zaidi ya kusubiri ilani ya CCM kama anavyosema kila siku.Kwa kukosa dira binafsi ni wazi atatuangusha tu kwa sababu HAKUJIANDAA.
 
Kwani kampeni za uchaguzi zimeanza?

Kigezo gani kinakufanya udhani hajajiandaa kuwa Rais wa Tanzania wakati alijipeleka mwenyewe kwenda kuchukua fomu ya ugombea Urais kupitia CCM.

Ni nani unadhani amejiandaa katika wagombea Urais?

Kama wapo/yupo, umetumia kigezo gani kufikia kwenye hitimisho?
 
Si tu kuwa hajajiandaa bali pia hakuandaliwa kuwa rais, kila mmoja wetu anajua jinsi alivyookota hiyo nafasi ya ugombea barabarani baada ya nafasi hiyo kuachwa na walioandaliwa ambao ni Lowassa na Membe, kazi ipo!
Mkuu,
Hawa kina Lowassa na Membe waliandaliwa na nani?
 
Atakapoanza kampeni tarehe 22 mwezi huu ndipo mtajua kuwa jamaa alikuwa amehifadhi nondo a.k.a madini yake na atakuwa akiyatoa hadi nyie watu wa chadema na ukawa mtabadili uamuzi na mtampigia kura wenyewe. Kwani si hata mkapa alipopitishwa na ccm mlikuwa mnamdharau hivi hivi lakini aliposhika tu nchi je mafanikio tuliyaona au hatukuyaona? Psychologically binadamu wamegawanyika katika makundi haya mawili ya kitabia " extroverts " na " introverts " ambapo extroverts ni waropokaji, wazungumzaji na wataka sifa na publicity na hapa lowassa wenu ndiyo mahala pake lakini introverts huwa ni wataratibu, wana uhakika, wanajiamini na huwa na upeo mkubwa na akili nyingi na hapa magufuli ndiyo mahala pake.
 
Kila ninapomsikia Magufuli akisema Sitawaangusha nabaki kucheka tu
Sote tunajua Magufuli anataka kuwa rais kwa 'ajali' tu..hana dira wala maono ya kiongoz mkuu wa nchi zaid ya kusubiri ilani ya CCM kama anavyosema kila siku..kwa kukosa dira binafsi ni wazi atatuangusha tu kwa sababu HAKUJIANDAA

Lowassa ana dira gani binafsi?
 
unaona mkuu? vijana wa siku hizi siasa hawajui wanabaki kupost fikra zao tu zisizo na mashiko yoyote. Wapiga kura wa maana na wauhakika wametulia tuliii wanasubiri sera za wagombea, wengine wamepumzika usiku sasa, wamebaki wapayukaji tu
Mkuu,
Mimi nashangaa sana hizi hoja za kusema fulani hajajiandaa kuwa Rais wa Tanzania lakini hawatuambii ni kigezo gani wametumia kufikia hitimisho lao.

Mtu yoyote anayetimiza vigezo vya kisheria vya ugombea Urais na akachukua fomu za Urais atakuwa amejiandaa kuwa Rais.

Kampeni zikianza ndiyo tutafahamu maono ya wagombea Urais.
 
Maghufuri amemfanya mwenyekiti wa CCM taifa augue utapiamulo ghafla ni mali ghafi mbofu hana mvuto mzito na mwizi
 
Ulitaka ajiandae kwa kuwa nunua ili akiingia ikulu afanye kazi ya kulipa madeni ya fedha alizokopa na kukusanya ili awanunue.

Kujiandaa kuwa Rais wa Tanzania ni kuwa na hela za kununua wapiga kura, oh sorry nimechanganya kununulia zabibu.
Mgombea uraisi kaishiwa nguvu kabisa amebaki kukoda macho hajui apunge mkono acheke aitishe alinselema apige ngoma maskini ni mteuliwa wa kwanza kuperish kabla hata ya kampeni, ikifika kampeni si ndio atazikwa kabisa manake watu wana mikanda yake laivu
 
Mkuu,
Hawa kina Lowassa na Membe waliandaliwa na nani?

Waliishatafuta muda mrefu mafisadi wa kuwasupport hivyo tayari wana mtaji wa urais na wanajua ni namna gani watarejesha kwa wafadhiri wao wakiupata urais.


Kama kuna mtu hakujiandaa huyo ndiye anafaa kuwa Rais maana hana deni na mtu.Ogopa sana kwenye ncgi zetu maskini kuwa na Rais aliyeununua urais.
 
Wewe hukuona au hujui kuwa Lowassa na Membe wana watu ambao walikuwa wanapigana ucku na mchana kuhakikisha kuwa jamaa zao wanaingia Ikulu? Au hayo makundi uliyokuwa unasikia kuwa wanayo unadhani yanaundwa na kina nani?

Jiongeze kiakili, hayo makundi yaliyojiandaa ndio hatari kwa nchi yako,endelea kushangilia kibwege wakati wenzako wako kwenye biashara ya kununua nchi.

Tuliishajifunza makundi yaliyomnunulia urais Kikwete yalivyosumbua ili yalirudishe pesa zao,baada ya kukosana na Kikwete yakahamia huku na sasa kwa nguvu kibwa zaidi wamewekeza kwa Lowassa na Mtanzania mzalendo eti anaona fahari kuwa na urais wa kununua.Kama una watoto pole yao.Tumepewa vichwa ili tufikiri na sio kufugia nywele.
 
hakujiandaa???? wewe ndo alikuambia kuwa hakujiandaa???
 
Wewe hukuona au hujui kuwa Lowassa na Membe wana watu ambao walikuwa wanapigana ucku na mchana kuhakikisha kuwa jamaa zao wanaingia Ikulu? Au hayo makundi uliyokuwa unasikia kuwa wanayo unadhani yanaundwa na kina nani?

uliona peke yako, wewe ndo ulienda mchukulia form
 
Ulitaka ajiandae kwa kuwa nunua ili akiingia ikulu afanye kazi ya kulipa madeni ya fedha alizokopa na kukusanya ili awanunue.

Kujiandaa kuwa Rais wa Tanzania ni kuwa na hela za kununua wapiga kura, oh sorry nimechanganya kununulia zabibu.

Pamoja sana.

Sijawahi kuona watu wajinga kama hawa, yaan watu wazima wanasifu kuandaa timu ya kununua urais?kuandaa wachuuzi wa kuununua urais wa nchi yao wao ndio wanaona sifa? wapuuzi sana hawa watu.

Wakati mwingine unaweza kujilaumu kuwa nchi moja na watu kama hawa.Labda kama wana umri chini ya miaka 15,maana JF sikuhizi ata watoto wapo.
 
unaona mkuu? vijana wa siku hizi siasa hawajui wanabaki kupost fikra zao tu zisizo na mashiko yoyote. Wapiga kura wa maana na wauhakika wametulia tuliii wanasubiri sera za wagombea, wengine wamepumzika usiku sasa, wamebaki wapayukaji tu

Wewe unavyoita wenzio wapayukaji ni jambo gani la msingi ulilopost kwenye hii thread? Ngoja nikuulize swali dogo tu: Wakati wa kampeni Magufuli atatakiwa kutumia rasilimali kama vile fedha, ndege za kawaida, chopa, magari, meli, boat pamoja na Watu (wapambe), unadhani atapata wapi vitu hivi ili aweze kufika kila uchochoro wa nchi hii kutafuta kura? Ni kutoka CCM? Serikali? Nani watakaomuidhinishia rasilimali hizo? Ndorobooooo!
 
Waliishatafuta muda mrefu mafisadi wa kuwasupport hivyo tayari wana mtaji wa urais na wanajua ni namna gani watarejesha kwa wafadhiri wao wakiupata urais.


Kama kuna mtu hakujiandaa huyo ndiye anafaa kuwa Rais maana hana deni na mtu.Ogopa sana kwenye ncgi zetu maskini kuwa na Rais aliyeununua urais.

Kweli mkuu.Hawa watu watashangaa sana muda wa kura.Kuna mambo yanastuwa watu.Hizo fedha zinatoka wapi?
 
Jiongeze kiakili, hayo makundi yaliyojiandaa ndio hatari kwa nchi yako,endelea kushangilia kibwege wakati wenzako wako kwenye biashara ya kununua nchi.

Tuliishajifunza makundi yaliyomnunulia urais Kikwete yalivyosumbua ili yalirudishe pesa zao,baada ya kukosana na Kikwete yakahamia huku na sasa kwa nguvu kibwa zaidi wamewekeza kwa Lowassa na Mtanzania mzalendo eti anaona fahari kuwa na urais wa kununua.Kama una watoto pole yao.Tumepewa vichwa ili tufikiri na sio kufugia nywele.

Kwa akili yako hiyo unayojiaminia unadhani mtu aweza simama peke yake na akafika ikulu? Si utafute angalau historia ya Mwl Nyerere ambaye sote tunaamini kuwa hakununua urais wa nchi hii uone jinsi alivyopata misaada ya hali na mali toka kwa wapambe wake ili tu akamate nchi? Mfano, umeshawahi kusikia juu ya mchango wa Kawawa na kundi lake kwa Nyerere kuwa rais wa kwanza wa nchi hii? Think out of the box!
 
Back
Top Bottom