Magufuli hafai kuwa Rais: Siyo msafi na hajawahi kuwa msafi

Status
Not open for further replies.
Mafisadi wabaya sana. Hivi wewe kaka Ocampo four unalipwa kiasi gani kumchafua Magufuli?
wala sijapewa fedha yoyote mkuu.... mshahara wangu ndiyo nimitumia kufanya huo utafiti mdogo kwa kwenga Msasani, Mwenge, na kwenye baadhi ya barabara kama ile ya Ikwiriri kwenda Somanga..... Lowassa hata simfahamu na sitaki hata kumfahamu....
 
wala sijapewa fedha yoyote mkuu.... mshahara wangu ndiyo nimitumia kufanya huo utafiti mdogo kwa kwenga Msasani, Mwenge, na kwenye baadhi ya barabara kama ile ya Ikwiriri kwenda Somanga..... Lowassa hata simfahamu na sitaki hata kumfahamu....
Hakuna utafiti wowote uliofanya. Huna jipya ulichoandika ambacho hakijawahi kuripotiwa kwenye media. Kumbuka kumpiga mateke chura ni kumuongeza mwendo. Magufuli hachafuliwi kwa staili hiyo
 
nikuhakikishie juu ya Kebby hotel umekurupuka saana, na hii ni tabia mbaya na ya ajabu ya kuchafua watu ovyo, unaijua kebby hotel wewe!? unajua kirefu cha KEBBY? Au unataka tukuwekee kila aina ya Document kuhusu hii hotel.
 
Kwani Ocampo four ana hoja gani ya maana mpaka ajibiwe? Kaka hugochavez, umesema ukweli kuwa Rais ajaye ni Magufuli

Ni vyema mkajibu hizo hoja acheni kelele mkuu..... Naona option ya Membe munamtetea kweli kweli.... Magufuli na Membe wote ni wale wale
 
Daaah,hoja hizi jamani hazitaki jazba.Ingawa uzi ni wa Magufuli lakini kwa mbali Membe ametajwa akichimbia hela za Gadafi kwenye mahandaki.na Pinda akiwezesha hela za Escrow kuibwa.Kifupi vijana wa Lowasa wako vizuri.

Ocampo akipiga kitu hakurupuki, anapiga kwa akili sana..... Watu wanaweza kuchukulia kama Magufuli kapigwa ila angalia kagusia issue kubwa kubwa kama fedha za Ghadafi, sakata la Escrow na vibali vya sukari... Kwake yeye mesage sent
 
Ben Saanane ni mtu makini na mwenye akili sana...... Ni Moja wa watu ambao wakishusha uzi hata kama nilikuwa nakula nasitisha zoezi kwanza ili tu nisome uzi wake......
Dah! Hii ndoa ya Ocampo four na Ben Saanane imeanza lini?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom